Msaada wa kimawazo: Nijenge au ninunue gari

Msaada wa kimawazo: Nijenge au ninunue gari

Beira Baby, utavunja records mwaka huu kwa threads zako aisee! Kwa wiki nafikiri unafikisha threads "buku" hivi, hongera
 
Amani iwe nanyi wapendwa,

Husika na kichwa cha habari hapo juu,

Mimi ni mfanya biashara mwenye chini ya miaka 25 kwa sasa biashara zangu zinaenda tu fresh ukizangatia na saizi wafanyabiashara tumekuwa wachache sana sio kama zamani.

Sasa basi kuna milioni kumi na tano yangu iko bank nimeiweka yaani kila baada ya mda flani huwa naogeza milioni moja au laki kadhaa bank lakini inategemea na biashara itakavyosimama kwa mwezi au kwa week.

Nina viwanja viwili kwa sasa sina nyumba wala gari nimepanga na mishe mishe zangu huwa napiga kwa kupanda gari.

Sasa basi naomba ushauri wenu wadau, je nijenge nyumba au ninunue gari ili nirahisishe mishe mishe yangu kwa town.

Naombeni ushauri naogopa kunuua gari wakati nimepanga nahisi ndugu wataniona lofa lakin mimi mwenyewe ni sharo kinoma kamoyo kangu kanataka gari.


Nawasilisha


LONDON BABY

Ulishasema biashara zako zinaenda fresh. Jenga nyumba.
 
Achana na nyumba mkuu nunua gari, nyumba utaendanayo wapi.

Ujenge nyumba yanini wakati unahitaji chumbakimoja tu ili ulale, nunua gari kiongozi.
 
Kiukweli kk hazina nzr kbs nakushauri jenga ukisha jenga unatafuta CHUMBA kimoja unakaa ila pia ukiamua vile vyumba vyengine ukodishe pia ni sawa unatengeza mtaji ambao+ na bishara zako Unaweza kununua GARI ya maana tu
 
Kweli unahitaji msaada wa kimawazo. Utanunuaje gari huna mahali pa kuipaki?? Mwenye nyumba ukamwombe ujenge gereji ya kulaza gari au ukailaze ofisi ya ccm mtaa wa 4 kutoka nyumbani!! Yataka moyo.
Ushauri;
Jenga nyumba kwanza, weka frem nzuri mbili au tatu. Wapo watakao pangisha ka unavyo pangisha na nyingine tumia wewe. Mola akijalia, weka na sehemu ya gereji kwenye jengo lako. Utakuja ingiza gari siku moja kwako sio kwa mtu.

Hayo yote kwa hiyo 15m?
 
Back
Top Bottom