Msaada wa kimawazo: Nijenge au ninunue gari

Msaada wa kimawazo: Nijenge au ninunue gari

Amani iwe nanyi wapendwa,

Husika na kichwa cha habari hapo juu,

Mimi ni mfanya biashara mwenye chini ya miaka 25 kwa sasa biashara zangu zinaenda tu fresh ukizangatia na saizi wafanyabiashara tumekuwa wachache sana sio kama zamani.

Sasa basi kuna milioni kumi na tano yangu iko bank nimeiweka yaani kila baada ya mda flani huwa naogeza milioni moja au laki kadhaa bank lakini inategemea na biashara itakavyosimama kwa mwezi au kwa week.

Nina viwanja viwili kwa sasa sina nyumba wala gari nimepanga na mishe mishe zangu huwa napiga kwa kupanda gari.

Sasa basi naomba ushauri wenu wadau, je nijenge nyumba au ninunue gari ili nirahisishe mishe mishe yangu kwa town.

Naombeni ushauri naogopa kunuua gari wakati nimepanga nahisi ndugu wataniona lofa lakin mimi mwenyewe ni sharo kinoma kamoyo kangu kanataka gari.

Nawasilisha

LONDON BABY
Hii inategemea mkoa uliopo,mfano dar kama unakaa kibaha, then unafanyia shughuli zako posta na shughuli zako zinahitaji sana usafiri ili kuweza kuingiza kipato vyema ununue gari kulahisisha shughuli yako
 
Umesema wewe ni sharo kinoma noma na kamoyo kako kanataka gari.. umeomba ushauri huku una jibu lako umeshalichagua, hata tukushauri kwa matarumbeta na vinubi lakini mwishowe utafanya ulichochagua,,
Nunua gari maana kamoyo kanapenda japokuwa nyumba ingependeza zaidi.
 
Gari linaweza kumuongezea matumizi na matokeo yake akashindwa kuhifadhi kiwango alichotaja kwa mwezi, nauli anayotumia huenda ikawa ndogo sana kwa mwezi ukilinganisha na pesa atakayotumia kuhudumia gari kwa mwezi
 
Sababu ya usharo wako nakushaur nunua gari, kwenye gar utaweza kulala pia Ila huwezi piga misele na nyumba
 
Kama unaweza lipa kodi nunua gari ila nyumba ni muhimu zaidi, hakuna kinacholeta amani kama kuwa na sehemu maalumu ya kuish hata kama unalala njaa
 
Umesema wewe ni sharo kinoma noma na kamoyo kako kanataka gari.. umeomba ushauri huku una jibu lako umeshalichagua, hata tukushauri kwa matarumbeta na vinubi lakini mwishowe utafanya ulichochagua,,
Nunua gari maana kamoyo kanapenda japokuwa nyumba ingependeza zaidi.
Ungetoa ushaur ingependeza zaid kiongoz wangu
 
Nunua gari, hamu ya kuwa na gari haiishi, safari moja uongeza nyingine. Ila Nyumba muhimu sana
 
Hongera kwa kuwa na viwanja viwili, jenga nyumba kwanza mengine baadae. Ila kama ni gari ya kusaidia katika biashara upige mahesabu ya sawasawa
 
Wanao kushauli kujenga ni waoga wa maisha sana sana watakua watumishi hewa kaka chukua ndinga utembee na nyota ya watoto wazuri achana na nyumba ata housegirl anayo
 
Back
Top Bottom