Msaada wa kimawazo, nataka kuacha kazi

Msaada wa kimawazo, nataka kuacha kazi

mkubhi

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2015
Posts
2,216
Reaction score
3,319
Wakuu habari ya jumapili?

Mimi kikazi ni mwalimu wa somo moja la hesabu secondary.... Nimekuwa na mawazo mgongano kila kukicha na sijaweza kupata uelekeo halisi wa nini nifanye kwa kuacha kazi yangu ya ualimu...

Kipindi cha nyuma nikiwa nimehitimu form four 2009 niliweza kupanda msitu wa ekari moja na kidogo na baadae nilipo maliza chuo 2015 nikapanda msitu mwingine kama ekari moja na kidogo tena ambapo kiuhakika hayo mashamba nikiyaingiza sokoni leo naweza kupata si chini ya million kumi...

Ajira niliyonayo naona inazidi kunichelewesha kuweza kuyafikia marengo yangu... Kwa mawazo ya karibu niliyo nayo nataka niyauze hayo mashamba nianzishe biashara au project yoyote ile ili angalau niweze kujisogeza kuyafikia marengo yangu!!

Wakuu naombeni mawazo yenu nini nifanye kutoka katika hili dimbwi la umasikini kwa kuanzia na kile nilichonacho...

N.B. napokea mawazo ya aina yote!
 
Kabla ya kuacha kwanza kazi, uza hiyo misitu uwe na cash mkononi.
By the way, hakuna kitu kizuri kama ajira ya kudumu.
Wewe acha kazi, ila siku ukifagia nyumba ukakosa kuokota hata sh mia, ndipo utajua kuwa ulikuwa unapata mshahara mkubwa.
 
Walimu ufanikiwa wanapoingia katika siasa (Magufuli, Nyerere, Mwinyi, Majaliwa, nk). Jaribu siasa - 2020 siyo mbali.
 
Usiache kazi bana ukipata ajira unajiongeza unakuwa na vitega uchumi vingine ila kuna watu wengi Sana degree za ualimu hawana kazi alafu ww unataka uache ujasiriamali nisafari ndefu unaweza kufilisika .Fanya yote mawili ila usiache kazi Aseh
 
hakikisha umeimalika kiuchumi ndipo utakuwa na jibu rahisi kuacha kazi au kuendelea.
 
Thread za kuacha kazi hasa Kwa walimu zinaongezeka kila siku,hii sio sawa,na wote wanawaza biashara! Kama taifa kuna sehemu tumekosea.
 
Mkuu katika hilo jambo usiwe na haraka hata kidogo, kwanza kumbuka hayo hayo maisha uliyonayo sasa kuna maelfu ya watu wanatamani wangekua nayo. Jambo jingine usione mtu kafanikiwa katika biashara basi ukahisi ni jambo jepesi au lilitokea kwa muda mfupi hapana, uhalisia ktk biashara hauko hivyo ndugu. Muhimu fahamu unataka kufanya bishara gani hasa na itakugharimu kiasi gani, tafuta mtaji anza hiyo biashara itakaposimama ndio ufikiri kutoka kazini, wako watu wengi tu wana biashara au miradi wanaiendesha lkn bado wako na ajira zao. Katika jambo hili usifanye maamuzi kwa hisia bali angalia uhalisia zaidi. Vp kama ukiacha kazi halafu biashara yako ikafail on ur first atempt na vp kama ikikuchukua miezi au hata miaka kupata ajira nyingine? Tuliza akili vizuri ili ufanye maamuzi sahihi isije ikafika kipindi hata mia tano ya kununulia bundle ubrowse jf ukakosa.
 
kwanini watu wengi wanapenda kuajiriwa???
jibu: ajira ndio njia rahisi zaidi ya kujihakikishia unakipato kisicho na mawazo hivyo kupenda kuajiriwa ni "survival instinct" ya binadamu, after all we are just another specie of animals
 
Back
Top Bottom