Msaada wa ki-sheria.

Blood of Jesus

JF-Expert Member
Sep 19, 2016
3,734
7,101
Kwanza kabisa pokeeni salamu zangu ninyi nyote wana Jf.

Ninaomba kuuliza ikiwa sisi wananchi tunaweza tukaipeleka serikali mahakamani kuidai fidia juu ya kupewa huduma na watu walioajiriwa na serikali hiyo (serikali ya ccm) ambao baadae walionekana kuwa ni unqualified personnels- refer zoezi la uhakiki wa vyeti lililoendelea/linaloendelea nchini Tz.

Mfano daktari aliyetuhudumia kwa miaka kadhaa mitano, kumi, kumi na tano, ... Leo hii tunapoambiwa kuwa daktari huyo hafai - (ni feki) sasa maana yake si ni kwamba hata huduma yote aliyoitoa kwa kipindi hicho chote si ni feki pia? ??? Mimi niliyehudumiwa na daktari huyo siwezi kumshtaki mwajiri wa mtu huyo(ambaye ni serikali) kwa kudai fidia juu ya kupewa huduma kutoka kwa "unqualified doctor" ???

Msaada please!
 
kama unaweza kuthibitisha ulipewa huduma feki nenda.

otherwise kesi yako itakufa kifo cha mende mapema sana, utapigwa chini "with cost"
 
Bila shaka ulihudumiwa vizuri ndiyo maana ulipona. Hila kama ulipata ulemavu au madhara yoyote kutokana na kutibiwa huko unayo haki ya kufungua kesi mahakamani ili upate fidia ila hakikisha unavyo ushaidi wote .pia kumbuka lalamiko lako ni umepata madhara kutokana na matibabu uliyoyapata katika hospitali husika na si cheti cha daktari maana hiyo ni kuwajibika kwa mwajiri.
 
Back
Top Bottom