Msaada wa jinsi ya kwenda Marekani nimepata mchumba huko

Feb 28, 2019
10
6
Habari Wakuu.

Kichwa wa habari kihusike hapo juu.

Nilifanikiwa kupata mpenzi ambaye ni raia wa Marekani na kazi yake ni mwalimu na tulikutana mtandao kwenye group la masuala ya elimu ya watoto

Kutokana na kuchangia kwangu katika kundi hilo nikiwa mtanzania pekee ,kuna siku nilipost taarifa ya kuomba mtu wa kunisaidia kupata baadhi ya vitabu vya elimu ya watoto na nilisema kuwa wanitumie katika email yangu

Kweli walinitumia watu kama sita na mmoja wapo akiwa huyo mchumba lakini badae nikamuomba namba yake ya Whattsapp sababu kwa email kuwasiliana ingenilia bandia langu sana bora kwa njia hiyo maana tigo ofa kibao kwa Whattapp ,Kama zali akakubali tukaanza kuwa tunawasiliana kila siku

Kwa siku za mwanzo tulikuwa tunachati mambo ya kitaaluma tu lakini baada ya miezi miwili kupita akaanza kuniulizia habari za mahusiano yangu ikaenda tukawa wapenzi mwanzoni nilijua labda ni kama utani vile lakini mwenzangu akawa yuko very deep na akawa anaonyesha ushirikiano wa kutosha sana mpaka kuanza kuzungumzia masuala ya ndoa na sasa amekata tiketi anakuja mwezi wa nane huku na anakaa wiki mbili hivi .

Ombi .kwa muda mrefu nimekuwa nikiona humu watu wanazungumzia namna ya kuweza kwenda mbele moja ya njia walisema ni kuwa na mpenzi wa kule inasaidia

Sasa mpenzi nimepata na anakuja huku .

Sasa utaratibu upi au nia ipi nitumie niweze kwenda kule maana hata passport sina na hizo habari kiukweli nilikuwa nimejitenga nazo kabisa kuhusu masuala ya kwenda nje za nchi ,maana hata kenya sijawahi kwenda . Naomba mnisadie kunipa mbinu na mawazo wakuu.

NB. Kuuliza sio ujinga jamani .
 
Ogelea..

you may not start conversation with the following recipient;Tairus
 
Akija week mbili hizi hakikisha akiondoka anachukia baashi ya vyakula! Halafu akifika atakuandikia barua kukualika ukamuone! Na akiri atakutunza na kama account take imenona unaenda
 
Tafuta passport kwanza hayo mengine ya safari yatajisumbukia yenyewe...
Hata. barabarani madereva wakipata ajari traffic akifika kabla ya yote huwa anaomba leseni kwanza
 
Mwanangu Golden chance hiyo .
Hizi wiki piga sana tizi .; Mchuzi wa pweza kwa sana bila kusahau na Pturulu.

Katuwakilishe vyema jombaa .
 
Back
Top Bottom