Msaada wa haraka, Uyui ni shida

Msaada wa haraka, Uyui ni shida

amadiora

Senior Member
Joined
Jun 5, 2014
Posts
149
Reaction score
24
Waungwana hii wilaya ipo TABORA just km 25 kutoka town njia ya Nzega, yaani kiutendaji Mungu ndo anajua halafu maafisa yaani baada ya mungu wanafuata wao, hasa idara ya elimu.

Walimu wanafanya kazi mazingira magumu mno walimu wasio wazawa kilio chao ni kuhama kila kukicha, mwalimu ana kaa miaka 7 hajapanda daraja, akifatilia anaambiwa utumish wamesimamisha madaraja.

Wilaya, mikoa mingine wanapanda mfan walimu walioanza 2007 wamepanda 2014 wakati mikoa mingine walipanda 2010. Jamani hii ni haki?

Tusaidieni kwa michango yenu, ikiwezekana tupeni no za utumishi makao makuu, kama Uzi huu wanausoma wafatilie
 
Ualimu ni 'WITO'........! hayo ndio madhara ya kuingilia FANI......! uko kata na shule gan? Ni PM.
 
Acha tu kazi ndugu yangu...utafute shughuli nyingine ya kufanya maadamu nguvu unazo na akili pia itakusaidia....
 
Nipo Kata ya BUKUMBI yaani ni shida hakuna nyumba za walimu sehemu ya kupanga ipo umbali wa kilomita 7 kutoka shuleni, usafiri ni baiskeli hadi unafka shuleni.

Kwa mwanafunzi akikutana na lori njia wakati wa kwenda shuleni hasa siku ya Usafi Alhamisi yaani ahesabu adhabu maana atakuwa tayari kachafuka, barabara ni vumbi tupu.

Kwa kweli walimu ni mateso kwa hii kata.
 
Back
Top Bottom