Msaada wa haraka niende bachelor of physics au veterinary medicine

chokaa nyeusi

Member
May 9, 2019
46
125
wadau mada kma inavyojieleza niende kusoma kozi ipi kati ya hizo mbili na manufaaa yake huko mbeleni.leo ndo mwisho wa kuthibitisha.......mawazo yenu tafadhali kwani nimekwama
 

Masiya

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
6,506
2,000
Mimi hapo ningechagua BVM(SUA) pamoja na mazaga zaga yake yote. Unaweza ukaajiriwa au uka jiajiri. La msingi ni kujua tu huko hakuna lele mama, kunahitaji utulivu na bidii kuanzia siku ya kwanza hadi mwisho.
Physics ni nzuri kama una matarajio makubwa yaani usome hadi si chini ya MSc na ikiwezekana PhD kabisa vinginevyo utapotelea hapa kati kati.
 

Watu8

JF-Expert Member
Feb 19, 2010
53,133
2,000
Unataka kuwa nani?

Maana hizi ni discipline mbili tofauti....
wadau mada kma inavyojieleza niende kusoma kozi ipi kati ya hizo mbili na manufaaa yake huko mbeleni.leo ndo mwisho wa kuthibitisha.......mawazo yenu tafadhali kwani nimekwama
 

Manjagata

JF-Expert Member
Mar 7, 2012
5,541
2,000
Kuchagua bvm umejiamini nini hasa? Njoo tu utatukuta mitaani sisi tuliopita hapo Vet! Ila uwe kamili kichwani, vinginevyo semester ya kwanza tu hutobozi! Ulishawahi kusikia muscles 250? Hizo zote tunataka uzikariri! Ulishwahi kuisikia kitu inaitwa biochemistry? Uishawahi kusikia kitu inaitwa oral examination? Njoo umejipanga kijana!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom