Msaada wa haraka kwa huyu mchumba wangu

Msaada wa haraka kwa huyu mchumba wangu

Obama wa Bongo

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2012
Posts
5,448
Reaction score
4,980
Habari zenu! wanaJF
Leo kwa mara ya kwanza ndio na post kwenye hili jukwaa! uwa napita tu,sababu mambo yangu ya mahusiano yalikuwa shwari mpaka jana usiku nilivyoanza kuhisi nina matatizo makubwa!

Nina mchumba wangu ambaye tangu tuanze mahusiano tulipanga kuanza kufanya mapenzi mpaka tutakapo halalishwa yaani kufunga ndoa(kwa kifupi mimi nimelelewa mazingira ya kidini sana), na matarajio yetu yalikuwa tuoane dec 2014, mimi ni mtumishi wa umma nipo dar na yeye yupo sekta binafsi alikuwa nje ya dar! sasa nikamshauri arudi DAR,kwa ajili ya kujiendeleza kielimu ,alikubali na anaendelea na shule, sasa jana usiku kanipigia simu analia eti hawezi kusubiri muda wote huo anataka tuanze kufanya mapenzi sasa hivi na anadai weekend hii lazima alale kwangu! kwani amechoka kuumia kwa muda mrefu kaamua kuwa mkweli?

Hili jambo linaanza kunitia mashaka kama kweli hapa patakuwa na ndoa imara maana hana uvumilivu kabisa, au kunakuzinguana na kutokana na imani yangu pamoja na malezi niliyokulia siwezi kumkubalia kufanya huu upuzi kabla ya wakati!

Mpaka sasa nataka nimkalishe chini hiyo siku atakayo kuja na kama akishindwa kunielewa ni bora huo uchumba ufe kabisa japo uwa anajifanya kulilia na kudeka ukimuuzi kidogo

Naomba mawazo yenu wanaJF Lakini yawe yakujenga sio utani na kashfa!

Nawasilisha
 
Ngoja kwanza nikae pembeni nichungulie majibu
 
Sasa wewe........hebu ngoja kwanza.......nitafakari hii hoja yako.......
 
Mkuu,

Hili suala linajibiwa tofauti kabisa tegemeana na sex ya mtu. Yani majibu ya suala hili hili ni tofauti kwa yale kwa mwanamke na yale kwa mwanaume.

Nimesoma sana kati kati ya mstari na sitaki nifanya conclusion ya kimakosa. Naomba nijue wewe ni Mwanaume ama Mwanamke?
 
Nilikuwa napita tu ktk uchochoro huu, kumbe kuna watu wanajadili mambo mazito namna hii.
 
Ha ha ha ha ha Obama wa Bongo usiogope sana kusikia hayo maana wenzako huko tayari wameanza kumpa mchecheto wa mahaba a.k.a mapenzi na hawezi kuvumilia tena maana chipsi na kuku na vyakula vingine anavyokula vinachochea hamu pia sasa kama anapata kinachomchochea zaidi ya mwili wake pekee basi ujue ukichelewa utakuta tayari watu wanamega.
Kwa kuwa hutaki kumega mpaka muoane basi fanya taratibu hizo haraka iwezekanavyo ili ule hilo tunda unalotunziwa bila kuwa na wasiwasi.
Nafurahi kuona watu tunajali matatizo ya watu,AshaDii,Preta na Bhululu natumai mtakuja na ushauri mzuri.
 
He/ she is right. There is no very good reason kwa nini hapana. Labda uwe unamatatizo unaogopa asije gundua ili akakimbia. Mmekaa mda gani katika mahusiano mpaka sasa.? Sijui imaani yako inasema nn.kapimeni mkiwa poua muendelee na mchakato as yo wishes
 
Kaka nitupime mie nikusaidie kum-pooza kiu yake...laa sivyo ataliwa na wajingawajinga wa shulen anakosoma...sorry lakini..did she said she's virgin????...kama hajawahi kuguswa na mwanaume toka azaliwe iweje aulilie uume asioujuwaaaaaa???..keshaonja tunda huyo so anataka kupanda mti kabsaaa avune matundaaaa....

Lakini na weweeee...mtu sio bikra na may be zote mbili hazipo unamtakaje asubirie mpaka 2014??...kwani huo ni uchaguzi wa raisi mpaka 2015???...mpe kitu roho inataka or else mlete watu tukusaidie kumpa kitu roho inapenda.
 
Kuna mwenzio kasomesha na anataka kuachwa, sasa endelea kuendeleza kielim na kungoja siku ya ndoa ,watakugegedea watoto wa mjini.
 
pole sana, kuwa makini inawezekana huyo mchumba wako ame sex na mtu mwingine na pengine anahisi amepata mimba sasa anataka ukisha sex nae , akuambie kua wewe ndiye mwenye hio mimba, mchumnguze vizuri.
 
habari zenu! wanaJF
Leo kwa mara ya kwanza ndio na post kwenye hili jukwaa! uwa napita tu,sababu mambo yangu ya mahusiano yalikuwa shwari mpaka jana usiku nilivyoanza kuhisi nina matatizo makubwa!

nina mchumba wangu ambaye tangu tuanze mahusiano tulipanga kuanza kufanya mapenzi mpaka tutakapo halalishwa yaani kufunga ndoa(kwa kifupi mimi nimelelewa mazingira ya kidini sana), na matarajio yetu yalikuwa tuoane dec 2014, mimi ni mtumishi wa umma nipo dar na yeye yupo sekta binafsi alikuwa nje ya dar! sasa nikamshauri arudi DAR,kwa ajili ya kujiendeleza kielimu ,alikubali na anaendelea na shule, sasa jana usiku kanipigia simu analia eti hawezi kusubiri muda wote huo anataka tuanze kufanya mapenzi sasa hivi na anadai weekend hii lazima alale kwangu!kwani amechoka kuumia kwa muda mrefu kaamua kuwa mkweli?
hili jambo linaanza kunitia mashaka kama kweli hapa patakuwa na ndoa imara maana hana uvumilivu kabisa,au kunakuzinguana na kutokana na imani yangu pamoja na malezi niliyokulia siwezi kumkubalia kufanya huu upuzi kabla ya wakati!

mpaka sasa nataka nimkalishe chini hiyo siku atakayo kuja na kama akishindwa kunielewa ni bora huo uchumba ufe kabisa japo uwa anajifanya kulilia na kudeka ukimuuzi kidogo
naomba mawazo yenu wanaJF Lakini yawe yakujenga sio utani na kashfa!
nawasilisha

Yaani leo ni March 2013, aendelee kusubiri mpaka Dec 2014 ndio aendelee kupata utamu wa mshadede? Mbona unatesa mwenzio? Mpe kitu roho inapenda. Ina maana na wewe bado bikira pia? Hujawahi kufanya mapenzi na mwanamke yeyote?

On a serious NOTE: Be very careful, usijekuta kashanasa mimba huko, sasa anataka kukulazimisha mfanye mapenzi ili akuchomekee akwambie hiyo mimba ni yako!
 
aisee,

hapa ushauri ni utata mtupu ndugu yangu kwani kwa kuangalia sababu nyingi ni ngumu kufanyia maamuzi. Kwa mfano kwa kadri ya religious perspective, social perspective etc sex before marriage kimaadili siyo sawa hata kidogo.

Ila kutokana na ashki ya miili yetu na pengine udadisi wa kutaka kufanya kile ulichozuiwa kufanya wengi wetu tumejikuta tunafanya sex before marriage

Ndio huo ugumu hasa wa watu kukushauri hasa ukiangalia kwamba watu wengi wanaamini na kukubali kwamba sex b4 marriage ni ishara ya mmonyonyoko wa maadili tena ni dhambi kwa wale wa imani, at the same time a significant number of couples wamefanya sex b4 maariage against 'ufahamu' wao huo wa 'ubaya' wa sex b4 marriage

infact katika jitihada za 'kuhalalisha' sex b4 marriage habari ya mujini ni kwamba watu wengi wanakubali na kuzingatia hoja ya kufunga ndoa pale mdada anapobeba mimba; kwamba kila upande utakuwa umethibitisha pasipo shaka kwamba kila mmoja wao ana function vizuri.....

Kwangu mimi ushauri ntakaokupa ni wewe mwenyewe kupima aina ya maisha unayotaka kuishi, imani yako na uhusiano wako na Mungu wako, umuhimu wa huyo mchumba wako kwako pamoja na namna unavyoheshimu na kutekeleza maazimio na maamuzi yako ya maisha, ndipo utaweza kuja na jibu kamili. This rests squarely kwako mwenyewe mkuu, sisi wengine hakika kichi kikombe ni ngumu kukinywea

Enjoy.....
 
Yaani leo ni March 2013, aendelee kusubiri mpaka Dec 2014 ndio aendelee kupata utamu wa mshadede? Mbona unatesa mwenzio? Mpe kitu roho inapenda. Ina maana na wewe bado bikira pia? Hujawahi kufanya mapenzi na mwanamke yeyote? On a serious NOTE: Be very careful, usijekuta kashanasa mimba huko, sasa anataka kukulazimisha mfanye mapenzi ili akuchomekee akwambie hiyo mimba ni yako!
thanks !kaka hilo nalo neno maana siku hizi simuelewi elewi huyu mtoa thread uwaanashinda siasani leo mmu inaonekana yamemsibu!
 
habari zenu! wanaJF
Leo kwa mara ya kwanza ndio na post kwenye hili jukwaa! uwa napita tu,sababu mambo yangu ya mahusiano yalikuwa shwari mpaka jana usiku nilivyoanza kuhisi nina matatizo makubwa!

nina mchumba wangu ambaye tangu tuanze mahusiano tulipanga kuanza kufanya mapenzi mpaka tutakapo halalishwa yaani kufunga ndoa(kwa kifupi mimi nimelelewa mazingira ya kidini sana), na matarajio yetu yalikuwa tuoane dec 2014, mimi ni mtumishi wa umma nipo dar na yeye yupo sekta binafsi alikuwa nje ya dar! sasa nikamshauri arudi DAR,kwa ajili ya kujiendeleza kielimu ,alikubali na anaendelea na shule, sasa jana usiku kanipigia simu analia eti hawezi kusubiri muda wote huo anataka tuanze kufanya mapenzi sasa hivi na anadai weekend hii lazima alale kwangu!kwani amechoka kuumia kwa muda mrefu kaamua kuwa mkweli?
hili jambo linaanza kunitia mashaka kama kweli hapa patakuwa na ndoa imara maana hana uvumilivu kabisa,au kunakuzinguana na kutokana na imani yangu pamoja na malezi niliyokulia siwezi kumkubalia kufanya huu upuzi kabla ya wakati!

mpaka sasa nataka nimkalishe chini hiyo siku atakayo kuja na kama akishindwa kunielewa ni bora huo uchumba ufe kabisa japo uwa anajifanya kulilia na kudeka ukimuuzi kidogo
naomba mawazo yenu wanaJF Lakini yawe yakujenga sio utani na kashfa!
nawasilisha

Naheshimu maamuzi yako ambayo kimsingi ni ya kiimani zaidi. Japo sikuhizi vijana wa mjini wanasema hakuna kuuziana Mbuzi kwenye gunia...ndio challenge zenyewe hizo.

Nadharia zangu hizi....


  • Yawezekana bishosti anapata hamasa kutoka kwa rafiki zake na yeye anahisi ana-miss bigtime...2014 bado mbaali muno...Jibu...mkalishie kitako ukimuelezea faida za kiimani za kutokula tunda la sumu mpaka pale mtakaporuhusiwa na kwa nini ni muhimu yeye na wewe kufanya hii kama agano muhimu la kuonyesha umoja wenu na utayari.
  • Yawezekana kabisa na yeye anataka kufanya yale wengi wanayo-amini kwamba 'the cookies' +food is the way to the man's heart. Na hivyo huwezi kumthamini na kumjali+kumpenda kiasi cha kumuwowa ikiwa hata cookie yake hujaionja. Pengine wamzuga tu...Muhakikishie utayari wako na kuwa yeye ndio Cleoptra wa enzi zako.
  • Anataka kujihakikishia kwamba game unaimudu kabla hajakusajili rasmi - Hapa sijui unatokaje, onyesha maconfidence na kuwa unayatawala masuala likiwamo hili.
  • Anataka kupata ball -Siku hizi kuna mtindo wadada kupata mtoii then kuwolewa baada ya kushusha kiddo....so inwezekana hii fashion na ye pia imemptia....Mpe uhakia kwamba ile game ya ufunguzi tu in 2014 kitu nyavuni na atapata ball...
 
Back
Top Bottom