Msaada wa haraka kwa huyu kijana wa four aliyepata matokeo jana tare 18.02.2013.

Wild fauna

JF-Expert Member
Apr 22, 2012
461
189
Heshima mbele!
Wakuu baada ya matokeo ya kidato cha nne kuna dogo hapa amepata division four ya point 28. Sasa inawezekana kwa alama hizo akaenda chuo cha ualimu? Naomba waliosoma chuo grade A wamsaidie huyu kijana kama alama zake zinamruhusu kupata chuo.
Nawasilisha
 
Heshima mbele!
Wakuu baada ya matokeo ya kidato cha nne kuna dogo hapa amepata division four ya point 28. Sasa inawezekana kwa alama hizo akaenda chuo cha ualimu? Naomba waliosoma chuo grade A wamsaidie huyu kijana kama kuna uwezekano akapata chuo.
Nawasilisha
Daah!!!!yaani sijakuelewa tufike mahali tuwe serious kwa hiyo div.four point 28 awe mwalimu aje atufundishie vijana ili kupitia ualimu wake tupate madaktari,marubani na wahandisi huko ndiko tunalipeleka taifa la TZ,halafu matokeo yamekuwa mabaya tunaanza kutafuta mchawi,CCM iache kuchezea mustabali wa taifa letu.
 
Heshima mbele!
Wakuu baada ya matokeo ya kidato cha nne kuna dogo hapa amepata division four ya point 28. Sasa inawezekana kwa alama hizo akaenda chuo cha ualimu? Naomba waliosoma chuo grade A wamsaidie huyu kijana kama alama zake zinamruhusu kupata chuo.
Nawasilisha


Mtafutie Certificate asome CBE,Ustawi wa Jamii,IFM etc ili akili ikue then ataunga diploma hadi degerr..sio lazma wote tupite njia moja ya form five-six,or ualimu..there is away better than these two ways we are used to!!!
 
Ualimu hawezi kupata maana kuanzia mwaka jana wameanzia kuchukua Mwisho wenye Divion IV ya 27 kwa GRADE A. ila anaweza kwenda CBE, IFM, USTAWI na kama yupo sciende na ana D tatu za PHYSICS, CHEMISTRY, BIOLOGY anaweza kwenda kusoma chet kwenye vyuo vya afya, kilimo, uvuvi. Kama mpo vizur kwa ushaur bora aende college akaanze na cheti pale IFM, CBE then aingie diploma hadi degree.


N.B
angalizo muulize anapenda nini kati ya kuresit, VETA na hivi vyuo vingne maana usikute yeye anapenda kufanya biashara au ufund au anataka kusoma chuo cha usafirishaji awe dereva. Hivyo basi kabla hamjamuamulia muulize akipendacho ukiona hajielewi mpe hizo option achague mwenyewe.
 
Arudie mtihani akifaulu ndiyo aende ualimu, UALIMU SI KIMBILIO LA WALIOSHINDWA MTIHANI

Heshima mbele!
Wakuu baada ya matokeo ya kidato cha nne kuna dogo hapa amepata division four ya point 28. Sasa inawezekana kwa alama hizo akaenda chuo cha ualimu? Naomba waliosoma chuo grade A wamsaidie huyu kijana kama alama zake zinamruhusu kupata chuo.
Nawasilisha
 
mteli dogo acheki kitu kingine cha kufanya, work hard for ur best alternative utaona success za ajabu. Nazidi kupata maono dogo aache kufosi jamani kitabu kinahitaji ujikane nafsi!
 
anaenda ualimu ili aje kumfundisha nani?? hii mifumo mibovu ndio inayopingwa kila siku.. Kuna Stadi za kazi mzee elimu utatuharibia kabisa
 
div iv ya 28 hawachukui,isipokuwa 27 ndo wanaenda!kama upo vizur mpeleke akasome certificate yoyote kama bandari,veta,CBE n.k then bdae ataendelea had diploma na digrii.
 
nimeipenda hii....! umefikiria kitu cha msingi sana...... maana isije ikawa wanamlazimisha kusoma kumbe yeye anataka ku-act bongo movie....
yap! thats true my dear! ndio maana siku hizi kama unaona mbali usiwekeze sana kwenye elimu kama mtoto haelekei huko ,wewe jitahidi mtoto wako awe celebrate uone atakavyo ingiza mkwanjaa! kama akicheza movie moja ana kula 30 million sawa na pension ya mtumishi aliyefanya kazi miaka 30!akiwa footballer anakula 150000 dollar per week!

ila sisi siku hizi tunaanda watoto kuwa mameneja !
 
Mkuu wangu "prakatatumba"
dogo ana D 5, ya physics,chemistry, geograhpy,kiswahili na history na anayo C ya Biology.
 
Dogo asikate tamaa afuate ushauri waliotoa wana jf kuna vyuo vingi vinavyotoa certificate ila kwa ushauri zaidi aende akasomee certificate ya general agriculture au animal science ili akimaliza asubilie ajira cause ajira za tanzania kipindi hiki ni sawa na ligi kuu ya uingereza all the best
 
Kama uko freshi mpeleke Uganda anapokelewa kwa mikono saba na 4 yake trust me nacho kuambia kuna watu washafanya hvyo mwaka jana saiv yuko zake alevel bila shida
 
Back
Top Bottom