Msaada wa Haraka Juu ya Huyu Mtoto

Kaudunde Kautwange

JF-Expert Member
Nov 15, 2011
1,625
1,619
Habari zenu wananchi!!

Nina mtoto wangu ambaye ametahiriwa wiki moja iliyopita, jana tukampeleka kwa dokta ili kusafisha kidonda.

Dokta akamcheki, kisha akatukabidhi kwa nurse ili amfungue, kwani alidai kidonda kimeshapona, baada ya kumfungua kulikuwa na ule wekundu wa damu.

Nurse akachukua pamba na dawa nyekundi ki muonekano, kisha akaanza kumsafisha dogo, tena kwa kusugua hasa, baada ya hapo akasema dogo tayari ameshapona tena akasema kama tumeenda na kaptula tumveshe.

Lakini mimi niligoma asiveshwe kwanza, maana dogo bado alikuwa anahisi maumivu, tumetoka hapo hospital dogo akaanza kulia kwamba anahisi maumivu.

Leo asubuhi nimeamka na kumkagua nimekuta amevimba kiasi, nahisi ni kwa sababu ya kule kusuguliwa.

Je, nifanyeje ili uvimbe urudi, maana dokta anasema ni hali ya kawaida, lakini dogo kama anahisi maumivu, pia dokta alisema hakuna haja ya kumpa dawa ya kukausha kidonda, so akatumbia tumpe panadol tu.

Msaada Jamani, nifanyeje uvimbe upungue, na maumivu yapungue?
 
Kama dokt kasem hakuna tatizo jaribu kusubiri ila angalia mabadiliko kama utaona hali sio nzuri na kidonda hakielekei kupona na kinazidi kuvimba mpeleke hospital nzuri maana hiyo sehem sio ya kuifanyia masihala,,
 
kwanini wanamsugua mmh
Jitahidi pasiingie maji wala uchafu na awe anavaa magauni hata kama ni wa kiume
uwe unapasafisha asubui na jioni
 
Spirit inasaidia sana, chukua pamba tia spirit kdg then safisha ila ucsugue sana na wala ucbandue ngoz zinazoanza kutoka, acha kumvalisha diapers this time pia uckitie maji kidonda, pole sana
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom