Msaada wa dawa kwa anaejua!

Msaada wa dawa kwa anaejua!

Maelezo yake yamejitosheleza kua ni bawasili akuma kingine wala tatizo linalohusu kutokwa na kinyama,muwasho au damu kwenye njia ya aja kubwa
 
Wakuu wa JamiiForums natumai hamjambo wote humu!kama kuna mwenye changamoto kama mimi basi Mungu ampe uponyaji.Amina! Kwa miezi ya karibuni nimekuwa nikisumbuliwa na kinyama kinashuka kutoka njia ya haja kubwa hata sijui ni

Kuna mdada niliwah kufanya nae kaz ofis moja.
Alikuwa na bawasiri.
Aisee . Kwanza choo kinafunga had siku 5.
na siku akienda haja anakaa lisaa lizima chooni.
Kwahiyo alikuwa na costipation na anasema inamsumbua kwa muda mrefu na ndio ikapeleka kupata hiyo bawasiri.

Sasa sina uhakika. Je costipation inapelekea kupata Bawasiri?

Dokta min -me . Bawasili au hiyo sijui rectal inasababishwa na nini?.
 
Kuna majani yapo mengi maeneo ya songweTdm wanayatumia Kama uzio wa mipaka
Nimesahau jina lake km Kuna member yupo huko atusaidie ni dawa nzuri

Unachuma majani yake mabichi unatwanga unabandika eneo husika
Week 1 tu umepona
TRUST ME.
 
Kuna majani yapo mengi maeneo ya songweTdm wanayatumia Kama uzio wa mipaka
Nimesahau jina lake km Kuna member yupo huko atusaidie ni dawa nzuri

Unachuma majani yake mabichi unatwanga unabandika eneo husika
Week 1 tu umepona
TRUST ME.
Mungu akujalie mkuu uyakumbuke,ikiwezekana na picha.Asante
 
Hospitali ukishindwa paka kitunguu swaumu ila vumilia maumivu yake tu
 
Pole sana Bro.

nenda hosp ujue kwanza ni nn hiko ambacho hakiko sawa. Na ufanye nn kukitibu au kupunguza.

Ila mostly Like itakuwa bawasiri.
Na kama ni hiyo zipo dawa na masharti ya chakula gan ule.
Na kinapotea na kupona.
Asante sana mkuu
 
Huo ugonjwa unawapata wanawake sana kwa kupenda vitu vya kukanga kaanga ambavyo huoelekea constipation ,, baada ya kutibiwa zingatia kula mboga mboga na maji ya.kutosha. kula mangano mgano nayo ni changamoto
 
Mtyaza/Mgoro.
Kwa maelezo yake inaweza kuwa ni hiyo.

Dawa ni aloevera za porini, kikwetu tunaita masongalele, unapaka ule utovu wake, Inarudi ndani wenyewe.
 
Mtyaza/Mgoro.
Kwa maelezo yake inaweza kuwa ni hiyo.

Dawa ni aloevera za porini, kikwetu tunaita masongalele, unapaka ule utovu wake, Inarudi ndani wenyewe.
Yes yes yes. Alo vera!!
Hii ninaushuhuda nayo, bro wangu alikuwa na shida ya kama hiyo

Japo yeye ilikuwa n bawasiri ya ndani.

Ila alikaa sawa kabisa.
 
Yes yes yes. Alo vera!!
Hii ninaushuhuda nayo, bro wangu alikuwa na shida ya kama hiyo

Japo yeye ilikuwa n bawasiri ya ndani.

Ila alikaa sawa kabisa.
Yess
Alovera inatibu bawasiri, Mgoro, hata vijinyama km sunzua.
 
Masongalele ndo yapi hayo mkuu
Mgoro nimekumbuka kwetu Songea. Akapake masongalele ule utovu wake. Atapona.
Mtyaza/Mgoro.
Kwa maelezo yake inaweza kuwa ni hiyo.

Dawa ni aloevera za porini, kikwetu tunaita masongalele, unapaka ule utovu wake, Inarudi ndani wenyewe.
Asante sana mkuu kama ni aloevera za porini ninazo!nashukuru nitaitumia
 
Wakuu wa JamiiForums natumai hamjambo wote humu!kama kuna mwenye changamoto kama mimi basi Mungu ampe uponyaji.Amina! Kwa miezi ya karibuni nimekuwa nikisumbuliwa na kinyama kinashuka kutoka njia ya haja kubwa hata sijui ni ugonjwa gani?wakati kama nimesimama muda merefu au kutembea kwa muda ndo kinashuka hadi kufikia kukirudisha kwa mkono.Tafadhali sana kwa anaejua dawa ya kumaliza tatizo hili anjulshe!Asanten sana!
From ChatGPT…
Dalili unazoeleza zinafanana sana na ugonjwa unaoitwa Rectal Prolapse (kuporomoka kwa utumbo wa mwisho kupitia njia ya haja kubwa).

Dalili zake mara nyingi huwa:

Kitu au kinyama kinatoka nje ya njia ya haja kubwa
  • Hutokea zaidi ukisimama muda mrefu, ukitembea sana, au wakati wa kujisaidia
  • Wakati mwingine lazima ukirudishe ndani kwa mkono
  • Unaweza kupata maumivu kidogo, kuwashwa, au ute kutoka
  • Wengine hupata constipation au kushindwa kuzuia choo
Sababu zinazoweza kuchangia

Kujikamua sana wakati wa choo (constipation ya muda mrefu)
  • Misuli ya nyonga (pelvic floor) kuwa dhaifu
  • Umri kuongezeka
  • Kuzaa mara nyingi (kwa wanawake)
  • Kukaa muda mrefu na tatizo la tumbo
Je, kuna dawa?

Kwa kweli mara nyingi tatizo hili halitibiki kabisa kwa dawa pekee. Matibabu yanaweza kuwa:
  1. Dawa na ushauri wa lishe
    • Kula vyakula vyenye nyuzinyuzi nyingi (fiber) kama mboga, matunda, nafaka
    • Kunywa maji mengi
    • Dawa za kusaidia choo kisitoke kwa shida

  2. Mazoezi ya kuimarisha misuli ya nyonga
    • Mazoezi yanaitwa Kegel exercise

  3. Upasuaji (kwa baadhi ya watu)
    • Kama tatizo ni kubwa au linaendelea mara kwa mara, daktari anaweza kupendekeza upasuaji mdogo kurekebisha utumbo.

Muhimu sana
Ningekushauri uende hospitali ukaonane na daktari wa upasuaji au gastroenterology haraka ili wakuchunguze. Usione aibu – ni tatizo linalotokea kwa watu wengi.

Mambo ya kufanya kwa sasa
  • Epuka kukaa muda mrefu chooni au kujikamua sana
  • Kula fiber nyingi
  • Kunywa maji mengi
  • Epuka kubeba vitu vizito sana
✅ Habari njema: wengi wakipata matibabu sahihi wanapona vizuri kabisa.

Kama unataka, naweza pia kukuambia:
  • Tofauti kati ya rectal prolapse na bawasiri (hemorrhoids)
  • Ni hospitali gani unaweza kupata vipimo vya tatizo hili karibu nawe.
Maswali kama haya siku hizi ingia ChatGPT or Gemini ai au any, ila ujiongeze kuuliza maswali zaidi utapata majibu mazuri kuliko daktari
 
Ukikosa Alovera tumia Utomvu wa Mapapai especially mabichi ila yawe yamekomaa vizuri atapona kabisa
 
Back
Top Bottom