Msaada wa charging system yangu ya galaxy S3

Msaada wa charging system yangu ya galaxy S3

kangaya

Member
Joined
Oct 14, 2014
Posts
51
Reaction score
3
Wakuu samsung galaxy S3 yangu inasumbua ku-charge..nikichomeka kwenye charger moto unaingia kidogo kama sekunde nne halafu inaacha kuingiza moto. Nimenunua charger mpya na battery mpya bado tatizo ni lile lile
 
Hapana si tatizo la charger,S3 nyingi sana zina tatizo hilo ukipeleka kwa fundi atabadilisha system yake ya kuingizia chaji gharama ni kama Tsh 10000.
 
asanteni..nilifata ushauri wenu na nimefanikiwa!
 
Mimi huwa nashangaa watu wanasema simu imekufa system charge , halfu akampelekea fundi akabailisha kwa elfu 10.

Kuna tofauti kubwa sana kati ya (1.) CHARGING SYSTEM au CHARGIN PCB na (2.) USB port, hiyo simu yako inawezekana ina tatizo kwenye hiyo USB port na sio charging system au kama kimtaani wanavyoita SYSTEM CHARGE,.
 
Mkuu samahani unaweza kufafanua haya maelezo,, maana yanaweza kutusaidia wengi..

naomba tofauti kati ya charge system na usb port kwenye android while tunajua kwenye andoid tundu linalotumika kwa charge system ndo hiloo hilo la usb port.. Unaweza kufafanua hapa mkuu, au weeh ulikuwa unamaanisha vipi mkuu?
 
Charge ways.ni njia mbili tu.zinazobaki ni za data.ili tupate kwa lugha ya mtaani tunasema charging system. Au usb port.na inawezeka charge ikaingiza simu isijae hapo kunakua na tatizo ktk hiyo njia ya data.....0754 60 45 67.piga au whatsapp.tuongee
 
Attachments

  • 1440796301654.jpg
    1440796301654.jpg
    22 KB · Views: 89
Mkuu samahani unaweza kufafanua haya maelezo,, maana yanaweza kutusaidia wengi..

naomba tofauti kati ya charge system na usb port kwenye android while tunajua kwenye andoid tundu linalotumika kwa charge system ndo hiloo hilo la usb port.. Unaweza kufafanua hapa mkuu, au weeh ulikuwa unamaanisha vipi mkuu?

Charging system /charging unit/charging pcb ni saketi ya ndani kabisa kwenye simu ambayo hii ndio inayoControl jinsi umeme unavyotoka kwenye charge/adapter kuingia kwenye simu na battery wakati wa kuchaji simu.

USB port ni hilo tundu ambapo unapochomeka charger/adapter , tundu hilo inaweza kuwa micro USB 2.0 au USB 3.0 Kwa simu kubwa kubwa kama vile Galaxy NOTE 3. Mara nyingi tundu hili ndilo linasababisha matatizo ya kuchaji simu yako endapo kuna pini zilizoachia (dry joints) au kama ile plastic ya ndani ya port imepata crack/pengo au imevunjika.

Matatizo haya mara nyingine tunayasababisha wenyewe kwa -:
1. Kutumia chaja zisizo na ubora, zingine zinabana sana lakini tunaziingiza kwa kulazimisha...
2. Makosa wakati wa kuchomoa chaja, ukiTWIST chaja wakati wa kuichomoa huchangia kulegeza au kusababisa dry joints..
3. Kudondosha simu wakati unachaji, hii ni hatari sana na inaweza kung'oa USB port kabisa.
4. Kuegemeza simu vibaya wakati umechomeka USB cable/charger, yaani unakuta ile cable ndio egemeo la simu.
 
charging system /charging unit/charging pcb ni saketi ya ndani kabisa kwenye simu ambayo hii ndio inayocontrol jinsi umeme unavyotoka kwenye charge/adapter kuingia kwenye simu na battery wakati wa kuchaji simu.

Usb port ni hilo tundu ambapo unapochomeka charger/adapter , tundu hilo inaweza kuwa micro usb 2.0 au usb 3.0 kwa simu kubwa kubwa kama vile galaxy note 3. Mara nyingi tundu hili ndilo linasababisha matatizo ya kuchaji simu yako endapo kuna pini zilizoachia (dry joints) au kama ile plastic ya ndani ya port imepata crack/pengo au imevunjika.

Matatizo haya mara nyingine tunayasababisha wenyewe kwa -:
1. Kutumia chaja zisizo na ubora, zingine zinabana sana lakini tunaziingiza kwa kulazimisha...
2. Makosa wakati wa kuchomoa chaja, ukitwist chaja wakati wa kuichomoa huchangia kulegeza au kusababisa dry joints..
3. Kudondosha simu wakati unachaji, hii ni hatari sana na inaweza kung'oa usb port kabisa.
4. Kuegemeza simu vibaya wakati umechomeka usb cable/charger, yaani unakuta ile cable ndio egemeo la simu.

doh asante asante sana mkuuu..
Haya maelezo yame nifunguaa sanaa...nimekuelewe vizuri sanaa.. I appreciate....
Nimejifunza kuwa samtimea unaweza ona simu yako haipeleke moto pale utakapo tumia as usb port... Bt kama utatumia charge yake og..ina weza ika function vizuri.... Daah mkuu saluti...
ymollel
 
Last edited by a moderator:
Sometimes huwa uchafu. Mimi siyo fundi. Unaweza chokonoa hilo tundu la kuchajia na mswaki, kabla ya kupeleka kwa fundi. It worked for me. Please toa feedback. Maelekezo haya rahisi niliyatoa google kwenye forum ya watumiaji.
 
ni kweli mkuu.. nishawahi kufanya hii kitu while natumiaa samsung NoTe 3.. kuna mtu aliniambiaaa... nitumie soft & new toothbrush...
tena akanishauri nikanunue peacock ( ile dawa ambayo huwa wanatumia mabinti) wanaitumiaga kupaka kichwa au kuchora chora kwenye miili yao..
sasa ukinunua ile peacock... ndani kunakuwa na kam swaki kadogo sana....
kale kamswaki ndo kanafaa , maana kako soft sanaa....

""umenikumbusha mkuu... nilitafuta hiyo peacock bila kupenda.. na tatizo langu liliishaa baada ya kusafisha... kwenye ile port ya charge kwenye note yangu""

maana nilibadilisha charge nyingi sanaa.. bila mafanikio... bt kwa njia hiyoo niliweza bila kubadili system chargebya simu yangu...
 
Back
Top Bottom