Mtoto wa Kishua
JF-Expert Member
- Oct 15, 2009
- 834
- 156
Mkuu ile modem ukiinunua na wakikwambia umeunganishwa na banjuka unachotakiwa kufanya ni kwamba kama hautumii net uhakikishe ume-disconnect vinginevyo hata ukichomoa modem bila kudisconect connection system yao itaendelea ku count muda coz wao wanacharge kwa muda unaokuwa online na sio bundle kama wengine. BTW pole sana mkuu.
TTCL Banjuka ni uwizi mtupu. Usije ukajaribu kwani itakufilisi. Unaweza kutumia hadi 10,000/- kwa siku kwa ku-surf dakika 30 tu.
TTCL ni wezi, lakini nadhani kampuni zote za simu ni wezi kwani Airtel watakupa 2500/- kwa mwezi lakini spidi yake ni kama kobe anayevutwa na konokono kupanda mlima.
Vodacom ndo kabisa hata neti hupati. Zantel walianza vizuri kabla na wao hawajajiunga na genge la majambazi sasa pengine wenzetu wa Dar watatueleza jinsi Sasa-Tel inavyofanya kazi maana haipatikani mikoani.
Hivi fibre optic zimesaidia nini hasa Tanzania? Maana huduma za internet ni mbovu, slow na very expensive sasa kuliko zamani.
Moja
Sasatel wanatumia CDMA (Carrier detection media access) ambayo inakuibia muda bila ww kujua coz ukitumia Tsh 500 masaa 24 bila kudownload sasa utakua unafanya nini.
Pili
Bidhaa za Sasatel i mn hardware zao si za kuaminika
Tatu
Hawako tayari kumsaidia mteja anapopata tatizo
Kufuatia lile tangazo lao la Banjuka na TTCL nime nunua Modem pamoja na kununua vocha ya sh 50.000 , sikwenda na laptop yangu, walicho kifanya ni kuni ingizia vocha , na kujaribu kuhakikisha kuwa imeingia kwa ku nipigia simu yangu hapo hapo, sikupokea nikakata.
Ajabu kufika home kucheki salio nakuta 37,000 , nikatumia net kwa saa moja tuu , nikaondoka, narudi sasa hivi nakuta salio ni 27,000 .
Sasa najiuliza je nilitakiwa ku register kwenye Banjuka package au nikwamba ukisha nunua hii modem ni automatically umeingia kwnye banjuka, maana hawakuniambia kama kuna namna ya ku register na service hi ya banjuka ambayo unaweza tumia kuanzia 500 mbaka 1000 kwa saa ,kutegemeana na wakati unaoingia kwnyemtandao. Nimejaribu kuwapigia TTCL lakini hakuna jibu simu inaita tuu.
Nafikiri ukishanunua modem ya ttcl, inakuwa automatically imeunganishwa na banjuka au inakuaje wakuu?