Ttcl banjuka ni majizi! Say no for ttcl broadband! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ttcl banjuka ni majizi! Say no for ttcl broadband!

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by mpingauonevu, May 3, 2012.

 1. mpingauonevu

  mpingauonevu JF-Expert Member

  #1
  May 3, 2012
  Joined: Feb 27, 2012
  Messages: 617
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 45
  Nilipoteza modem yangu ya airtel. Nikashauriwa nikanunue ya TTCL maana banjuka ni bei rahisi.

  Nikaenda kulipa 29,900. wafanyakazi wa pale wakanishauri niweke voucher ya 10,000 ili nitumia mwezi mzima. nikawaambia ngoja niweke 5000 wakakubali. huwezi amini nimetumia kwa JF tu! narudia JF tu! hakuna kudownload wala nini 5000 ikakata ndani ya siku mbili. nikasema labda kuna mahali nakosea, nikaongeza tena 5000! siku mbili sina kitu. JF tu! sijaangalia fesibuku wala email!

  Ilipokata nikawapigia customer care ya TTCL wakaniambia iko sawa kwamba dakika nilizotumia ni sawa na eti ni tsh17 kwa sekunde! nikawaambia sawa kwani mimi natumia mda wote? wakaniambia iko sawa na nimesajiliwa vizuri banjuka per second. Nikaongeza tena 5000! Yaani hii hata sikutumia JF hela imelambwa jamani! nikawapigia tena customer care nikawaambia waniambie ni nani niende nikamtupi modem usoni! maana nimechoshwa na WIZI NA UTAPELI WAO!

  PLEASE WANA JF NAOMBA SAPOTI TUBANDIKE POSTERS ZA KUSEMA NO KWA TTCL BROADBAND MAANA NI WIZI UTAPELI NA uJAMBAZI! SAY NO FOR TTCL BANJUKA! BANJUKA MY FOOT!!!!!!!!!!!!!!!
   
 2. Mu-sir

  Mu-sir JF-Expert Member

  #2
  May 3, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 3,633
  Likes Received: 471
  Trophy Points: 180
  Ngoja nikwambie mkuu hii utalaumu sana lakini mimi nimetumia sana hii banjuka ni kwamba kila ukimaliza mambo yako lazima uhakikishe umedisconnect vinginevyo ukiacha itaendelea kupungua tu kwa sababu wanahesabu muda na sio bundle kama mitandao mingine. Pole sana mkuu kwa hilo.
   
 3. MVUMBUZI

  MVUMBUZI JF-Expert Member

  #3
  May 3, 2012
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 4,970
  Likes Received: 664
  Trophy Points: 280
  Hawakukupa maelezo ya kutosha. BANJUKA iko hivi ni unlimited download ila kwa saa wana chargi 1000 kuanzia asubuhi hadi saa 12 jioni. Kuanzia 12jioni hadi saa 3 ni 800 kwa saa na kuanzia saa 3 usiku hadi 12 asubuhi ni shs 500.

  Ni kwamba wanahesabu dakika provided iko connected. within hiyo saa 1 unayochagiwa 1000 au 800 au 500 kama spidi ni nzuri unaweza kudowload unlimited hata 1GB au zaidi inategemea spidi na u- sharp wako. Kwa hiyo ujanja wa kutumia BANJUKA ni kuwa makini na muda ukimaliza shughuli zako disconnect la sivyo hela inaisha.

  Hapa JF natumia TCCL BANJUKA na iko vema kabisa
   
 4. NusuMutu

  NusuMutu JF-Expert Member

  #4
  May 8, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 423
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  wale ttcl kenge tu,mi huu mwezi wa 5 sasa nimeomba nifungiwe l├Čne(landline) nimeandika barua na kujaza fom zao nikafuatlia kama mara3 wanadai oh.,mara nyaya ziko bandarini mara sijui nini ilimradi ujinga ujinga tu.nimeamua kuachana nao
   
 5. a

  akrb Senior Member

  #5
  Aug 11, 2012
  Joined: Mar 6, 2012
  Messages: 103
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  hapo sijaelewa vzuri,wanachaji buku kwanzia asubuhi hadi saa 12 au buku kwa kila saa utakayoi2mia??
   
 6. N

  Nyauuu Member

  #6
  Aug 13, 2012
  Joined: Jan 27, 2012
  Messages: 46
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Kuanzia saa 1 asubuhi hadi saa 12 jion wanakata 1000 kwa saa kuanzia saa moja jion hadi saa 2:59 wanakata 800 kwa saa na kuanzia tatu hadi 12:59 wanakata 500 kwa saa. kibaya ni kwamba watakata sawa kwa mwenye speed nzuri na mwenye speed mbovu ilimradi umeunga computer yako kwenye mtandao! Haya ndio maisha ya kitanzania bwana ubabaishaji kuanzia mjengoni, jumba jeupe mpaka kwa actor wa kijiji!
   
 7. Nyenyere

  Nyenyere JF-Expert Member

  #7
  Aug 13, 2012
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 8,567
  Likes Received: 1,930
  Trophy Points: 280
  Kumbe bora ya ZANTEL unlimited siku tatu kwa shs. 6000.
   
Loading...