Biashara ambazo mwanafunzi wa chuo kikuu anaweza kufanya bila kuathiri masomo yake

QUALIFIED

JF-Expert Member
Jun 13, 2012
756
225
Habari JF,

Jamani nahitaji msaada wa biashara gani nifanye ambayo haitahitaji muda wangu mwingi, ukizingatia mimi bado mwanafunzi. Eneo ninaloishi ni Dar.

Mtaji nilionao ni milioni 1.5.

Tafadhali msaada wa mawazo.

=================
nashukuru mzima ameuliza
Habari wakuu...

Mimi ni mwanafunzi wa chuo kikuu mwaka wa pili kutokana na sababu mbalimbali imenibidi kufikilia kufanya biashara ila hadi sasa nimefikiria kufanya biashara nyingi sana ila lengo la biashara nayo niliyopanga kufanya ni ile ambayo haitaingiliana sana na masomo yangu pindi niwapo chuoni...

Kwa nini nimekuja hapa katika jukwaa hili?
-jambo la kwanza naomba mnoshauri biaahara ipi ninaweza fanya na mbinu ya ufanisi katika kufanikisha biashara hiyo?

================================================
Ngoja nikushauri kitu mdogo wangu coz sisi tumepia vyuoni kama wewe,unaweza ukadharau hii biashara but amini nakuambia unaweza ukawa kila siku unatoka na 20,000/

Tafuta Kibegi cha mgongoni nenda kwenye maduka ya jumla nunua pipi zile za kisista duu yani pipi kijiti au hata ivory,gum like Batook,n.k,vocha za kukwangua na kurusha,biskuti,karanga,tambi na hata ubuyu.then uwe unazunguka campus amini utauza sana coz maeneo mengi ya chuo biashara hizi hazipo ndani ya maeneo ya chuo(hawaruhusu machinga kuingia chuoni).sasa kwa vile watu ni wavivu kuvuka kutembea kufata pipi au biskuti au vocha we utatumia advantage hiyo kupiga salio.

Biashara za kipuuzi ndo zinalipa sana bora tu usiwe na aibu,uzuri wa biashara hii ni kwamba haiitaji usimamizi ofisi ni mgongoni mwako,haili muda wako wa masomo,unaweza kuifanya hata darasani wakati lecture inaendelea,haina usumbufu wa TRA,easy to carry,watu wakishakuzoea ndo nafasi yako nzuri ya kupiga hatua 1000 ahead!

kila la heri!!
Habari za leo mpenzi msomaji wa AMKA MTANZANIA, karibu tena kwenye kipengele hiki cha ushauri wa changamoto mbalimbali zinazotuzuia kufikia mafanikio. Kwa wiki chache zilizopita kulikuwa na makala ya ushauri kwa wanafunzi wanaoanza chuo kikuu pia tumewahi kuweka makala za ushauri kwa wahitimu wa vyuo vikuu. Leo tutatoa ushauri mwingine kwa wanafunzi wanaoendelea na masomo yao ya vyuo vikuu na vyuo vingine vya elimu ya juu.
Kabla ya kuingia kwenye ushauri huo kwanza tupate maoni ya msomaji mwenzetu;

Habari za kazi , nina kupongeza kwa makala nzuri na za kuelemisha , nina ombi moja kwako utoe makala ya biashara gani au ujasiriamali gani mwanafunzi wa chuo Kikuu anaweza kufanya huku anaendelea kusoma ?
Hayo ndio yalikuwa maoni ya msomaji mwenzetu aliyetaka kujua ni biashara gani au ujasiriamali gani mwanafunzi wa chuo anaweza kufanya.
Kuna maswali matatu muhimu ya kujiuliza katika swala hili;

[h=1]Swali la kwanza, je inawezekana kufanya biashara au ujasiriamali ukiwa mwanafunzi wa chuo?[/h]

Kwa kuwa mimi ni mmoja wa watu ambao naamini hakuna kinachoshindikana ikiwa mtu atakuwa na nia ya dhati, jibu ni ndio, inawezekana. Japokuwa inawezekana sio rahisi, inahitaji kujitoa kweli na kujituma katika sehemu zote mbili, masomo na biashara.

[h=1]Swali la pili, je mwanafunzi wa chuo kikuu ana muda wa kutosha kufanya masomo na biashara pia?[/h] Kabla ya kusema ndio au hapana tuangalie kwanza muda uliopo. Kwa Tanzania vyuo vina mihula miwili na kila mhula una siku 120 au 140 kwa wenye mihula mirefu.

Hivyo kwa mihula miwili ni siku karibu 300 na hivyo mwanafunzi anabaki na miezi miwili kwa mwaka ambayo hana masomo kabisa. Tukija kwenye muda wa siku, katika masaa 24, darasani anatumia masaa yasiyozidi 8, kulala yasiyozidi 8, kujisomea mwenyewe hayazidi 4 na kupumzika masaa 2. Jumla hapo ni masaa 22 na hivyo kubaki na masaa 2 kwa siku. Hapo bado hatujahesabu siku za mwisho wa wiki ambapo mwananfunzi anaweza kupata masaa zaidi ya 5.

Hivyo basi muda upo na mwanafunzi anaweza kupata masaa yasiyopungua mawili kila siku ya wiki na yasiyopungua matano kila siku ya mwisho wa wiki. Masaa haya yasiyopungua 20 kwa wiki yanamtosha kuwekeza kwenye biashara bila ya kuathiri masomo yake.

Swali la tatu; ni biashara gani anazoweza kufanya mwanafunzi wa chuo kikuu?
[/h] Baada ya kuona kwamba inawezekana kufanya biashara huku unasoma na baada ya kuona unaweza kupata muda wa kutosha kufanya biashara na kusoma pia swali la msingi ni je ufanye biashara gani?

Kuna biashara nyingi sana unazoweza kufanya kulingana na kile unachopenda wewe na hata vipaji vyako. Kwa kifupi nikushirikishe baadhi ya biashara ambazo mwanafunzi wa chuo kikuu anaweza kufanya kwa muda huo alionao.

1. Biashara ya mtandao(network marketing).
Hii ni biashara ambayo mwanafunzi anaweza kuifanya kwa muda mchache kila siku au kila wiki na baada ya mwaka au miaka miwili akawa ametengeneza mafanikio makubwa. Hii ni biashara ambayo unatengeneza mtandao wa watumiaji wa bidhaa au huduma na hivyo wanaponunua biashaa au huduma hiyo wewe unalipwa kamisheni.

Kuna makampuni mengi yanafanya biashara hii kwa hapa kwetu Tanzania, zifuatilie vizuri kampuni hizi na chagua ni ipi unayoweza kuingia na kufanya biashara. Mbali tu na kufanya biashara pia utajifunza biashara katika ulimwengu halisi.

ANGALIZO; Ukiwauliza watu kuhusu biashara hii watakukatisha tamaa sana kwa sababu wengi wa waliofanya biashara hizi wameshindwa kwa sababu mbalimbali, wewe unaweza kama ukiamua.

2. Ujasiriamali wa taarifa(information entrepreneur).
Hii ni biashara ambayo unatoa taarifa mbalimbali ambazo zinaweza kuwasaidia watu na hatimaye wakawa tayari kukulipa au ukafaidika kwa njia nyingine. Kuanza biashara hii unachagua ni aina gani ya taarifa ambazo unapenda kufuatilia au kutoa kisha unaanzisha blog ambayo utakuwa unatoa taarifa hizo.

Ukitoa taarifa nzuri utapata watembeleaji wengi na hatimaye unaweza kuwauzia bidhaa au huduma nyingine au kuuza nafasi za matangazo kwenye blog yako hiyo na ukapata kipato kizuri.
Kujifunza jinsi ya kuanzisha blog na kufanya biashara hii pata kitabu; Jinsi ya kutengeneza fedha kwenye mtandao kwa kutumia blog.

3. Endeleza vipaji vyako.
Kila mmoja wetu ana vipaji au vitu fulani anavyopendelea kufanya. Unaweza kutumia muda huu wa chuo kuendeleza vipaji vyako na kuangalia ni jinsi gani unaweza kuwafanya watu wakulipe kupitia kipaji chako, Unaweza kuwa na kipaji cha kuimba, kuigiza, mitindo, kuandika na kadhalika. Weka muda maalumu wa kuendeleza kipaji chako kila siku. Kwa mfano kwa wanaopenda kuandika nashauri utenge saa moja kila siku kwa ajili ya kuandika tu, kwa njia hii utaboresha uandishi wako.

4. Fanya biashara inayohusiana na TEHAMA
Teknolojia ya habari na mawasiliano(IT & ICT) bado inakua kwa kasi sana. Kama unapenda kutumia kompyuta au mtandao unaweza kufanya biashara nzuri sana inayohusisha IT. Unaweza kujifunza vitu kama kutengeneza picha(graphic design), kutengeneza website, kutengeneza program za kompyuta na hata za simu(mobile app). Ukishajua kutengeneza vitu hivi na ukawa mbunifu unaweza kutengeneza biashara nzuri na kubwa sana.

5. Uchuuzi wa kawaida.
Unaweza pia kufanya biashara nyingine ndogo ndogo kwa maeneo ya chuoni au unakoishi. Angalia ni bishaa au huduma gani wanafunzi wanazihitaji ila wanazikosa au hawazipati kwa kiwango kizuri kisha ingia kwenye biashara hiyo na toa huduma nzuri sana. Utatengeneza biashara nzuri na yenye faida.

Mtaji wa kuanzia unatoa wapi?
[/h] Hili ni swali ambalo baadhi wameshajiona kwamba hawawezi kufanya biashara hizo kwa sababu hawana mtaji. Biashara zote nilizozungumzia hapo zinaanza na mtaji kidogo sana na nyingine kama ujasiriamali wa taarifa unaweza kuanza bila hata ya mtaji ni wewe na kopmyuta yako tu. Lakini zile zinazohusisha mtaji kidogo unaweza kuupata kama ukifuata ushauri niliotoa kwa wanafunzi wanaoanza chuo kikuu.

Hizo ndizo baadhi ya biashara ambazo mwanafunzi wa chuo kikuu anaweza kufanya. Kumbuka sio biashara hizo tu ndio zinawezekana, bali hizo ni chache ambazo nina uhakika zinawezekana. Hivyo kama una wazo lako jingine la biashara bado unaweza kulifanyia kazi.
Pia biashara hizo sio rahisi, ila kama umedhamiria kweli na ukajituma kweli inawezekana.

Na utakapoanza maisha hayo ya kusoma na kufanya biashara kuna vitu unatakiwa uache, baadhi ni, kuangalia tv, movie, mipira, kuperuzi mitandao muda wote n.k

ZIADA; Ushauri niliotoa hapa hauwezi kuwa sawa kwa kila mtu na wewe kama mwanafunzi wa chuo kikuu unaweza kuangalia ni kipi kinaweza kufanya kazi kwako na kisha kukibopresha zaisi kulingana na mazingira uliyopo.

Kama unaendelea kupata shida kujua ni biashara gani unaweza kufanya katika mazingira uliyopo tafadhali wasiliana nami kwa email amakirita@gmail.co au 0717396253.
Nakutakia kila la kheri katika mafanikio ya masomo yako na biashara yako.
TUPO PAMOJA.

Kama una changamoto ambayo inakuzuia kufikia malengo yako unaweza kuitoa kwa kubonyeza maandishi haya na kujaza fomu. Changamoto yako inaweza kuwa moja makala zijazo kila siku ya jumatatu. Kama unahitaji ushauri wa haraka wasiliana na mimi kwa kwa email amakirita@gmail.com au simu 0717396253/0755953887.
ZAMA NDANI

MIRADI MIDOGO MIDOGO 15 YENYE KUZALISHA KIPATO KIKUBWA KWA AJILI YA WAJASIRIAMALI
WANAFUNZI NA WANACHUO
STUDENTS WITH A MISSION

1.MLM: Hi ndio biashara moja ambayo wanafunzi wengi ulaya wanapiga pesa sana sasa hivi imefika Tanzania na Kenya: Nchini Nigeria mamilionea wengi vijana wametokea katika mtandao huu. Kenya pia na SA vijana wengi wamejikita katika biashara hii

NAMNA YA KUANZA: Kwa kifupi biashara hii unahitajika kuwa mwanachama wa kampuni inayo sambaza bidhaa kwa mtindo wa MLM, ndipo ununue bidhaa katika bei ya chini uzitumie au uuze kwa rejareja. Na kisha ualike watu wengine wengi nao wawe wanachama wa kampuni hiyo ya MLM, kila mwanachama unaye mwalika utalipwa kiasi flani cha pesa yake ya manunuzi ya bidhaa. Mtaji wa kuanzia katika kampuni hizi ni SIFURI had Million 10. KAMATA FURSA

KWA NINI WANAFUNZI/WANACHUO? Haihitaji mtaji mkubwa incase huna, haihitaji muda mwingi, hauhitajiki leseni wala huhitaji mwuza duka. Kuna uwezekano mkubwa wa wewe kufanya biashara na dunia nzima katika sekunde moja kama utafuata mbinu utakazofundishwa. Makapuni yanayojihusisha na biashara hizi yamejikita katika bidhaa za afya, urembo, kilimo na sasa muda wa Maongezi.

UWEZEKANO WA KIPATO: SIFURI hadi BILLIONEA ndani ya siku 30 hadi miaka mitano. Utaweza kuona kama mwanafunzi ukiingia katika biashara ya MLM mwaka wa kwanza na ukatumia boom lako vizuri utakapokuwa unamaliza chuo utakuwa unatengeza pesa sawa na mtu aliyeaajiriwa au umemzidi kabisa.
SECRET BEHIND SUCCESSFUL PEOPLE: Kuzungusha mtaji mara nyingi, kualika watu wengi kwa kadri inavyowezekana. Kama mwanachuo au mwanafunzi hili ni jambo rahisi una marafiki wengi sana mliosoma na mnaosoma nao pamoja.
Kwa maelekezo zaidi tembelea facebook page STUDENT WITH A MISSION

2. MOBILE MONEY: MPESA, EAZY PESA, TIGO PESA NA AIRTEL MONEY, Hii inajulikana sana but ili upige pesa vizuri inabidi uwe na float nzuri hapo chuoni kwako kuanzia 1,000,000 hadi 10,000,000 kwa siku. Na kama upo karibu na benki au super dealer iyo itakuwa safi. Faida ni kubwa mfano mtaji wa 300,000 sehemu ya mtaani tu inakupa 45,000 hadi 120,000 kwa mwezi.

Mungu akupe nini? Gunia la chawa. Biashara hii ni rahisi sana kwa mwanafunzi maana unatembea na duka lako, muuzaji wewe wateja unao kila saa darasani, lecture room, discussion, disco na nyumba za ibada. KAMATA FURSA

3. MUDA WA MAONGEZI (AIRTIME): KAMATA FURSA HII, sio ile ya zamani ambayo unauza vocha za kukwangua hapa ni muda wa Maongezi. Ukisha kuwa na mobile money basi wewe jiunge na RIFARO Africa utapiga pesa kama upo ZANTEL, TIGO na AIRTEL. Kifupi ni kwamba maradi wa kwanza apo juu MLM unauunganisha na huu wa 3. Lazima utapiga hela. Unahitaji matji kidogo tu wa SH150,000 tu. Kwa maelezo zaidi google Rifaro Africa au whatsapp or text me +255 752 693 692 starting with a word student with a mission

4. UANDISHI WA VITABU au DOCUMENTARY: Haya vijana wa IT na wale watundu wa simu na computer, wale mnaopenda umbea na udaku sasa umbea na uduku uweke kitabuni kwa staili tofauti. Andika story za maisha, umeshazisikia ama wewe mwenyewe au zile za kufikirika, weka kwenye laptop yako au flash disk uza kwa wachapishaji.

Inaweza kuwa short story au series ili mradi iwe ya kuvutia. Jifunze namna rahisi ya kutengeneza documentary za kuvutia kisha rusha facebook na mitandao ya kijamii wafanya biashara watakutafuta kwa ajili ya kutengeneza matangazo yao mbalimbali ya kibiashara ili wayatumie facebook na whatsapp.

5. UTUNZAJI BUSTANI wewe kijana wa SUA wewe inakuhusu nenda mjini tafuta watu wanohitaji kutunziwa bustani zao za nyumbani hasa UKOKO, unda team za vijana wasimamie mara kwa mara. Hii biashara inalipa sasa ivi town. Wewe kazi yako ni mipango tuu aka Manager. Mbolea za maji safi kabisa ambayo unaweza weka mfukoni sasa zipo Tanzania, lita moja inatosha ekari 2 na ushee

6. BETTING MKEKA: Vijana hapa sina la kuongeza mana wengi mnapiga hela weeend kama hamna akili nzuri, kuna betting website mbili Tanzania ambazo zipo juu (1) MERIDIAN (2) MBET na moja haiko online (3) PREMIER BETTING. Kama unataka kupunguza risk ya kupoteza cheza online betting ingawa premier betting nayo ni bomba vijana mnaijua. ONYO betting ni addictive na unaweza poteza boom lako usipokuwa makini, be responsible.

7. DALALI: Chagua eno lako moja la udalali hasa hasa unalolijua sana, kama magari, computer, simu, viwanja yaani vile vitu watu wanavitafuta na vina bei kubwa. Tumia blogs, face book, jamii forum na matangazo madogo magazetini kuuza. Hapa unaweza piga pesa ndefu ya kutosha mwaka wa masomo

8. MC: Nasema kama wewe ni mdakuzi na m mbeya wacha kuumiza shingo na kichwa kwa umbeya wako, tengeneza hela kuwa MC mataji kidogo unahitajika nguo za kazi, mike ya kisasa na music system. Anza na vipati vidogo vidogo kama birthday parties, mikutano midogo, send offs na hatimaye utajikuta upo harusini, mikutano mikubwa ya injili na international meeting

9. NM Network marketing, hii sawa na udalali ila hapa unauza vitu vyako matandaoni tu, yaani matangazo yako yote yapo mtandaoni, wateja wako wote wako mtandaoni. Wewe unacheza na simu na laptop, au tablate au hizo computer za chuo. Tembea na mooderm muda ukifika wa kuuza unaunga modern unapiga kaz le say 1 hour per day inatosha, wenye shida watakutafuta. Kama huna bidhaa ya kuuza nitafute nikuelezee bidhaa lukuki za kuuza huko mitandanoni.

10. BLOGGER: Sasa unaweza ku blogg kwa raha zako au kublog kwa kuuza products ikiwa utakuwa umechagua moja kati ya miradi hii hapa 1,4,5,7,8,9,11,14,15 basi ili uuze usiku na mchana huna budin kuwa na blog ya kukutangazia bidhaa zako dunia nzima 24/7. Hapo utakuwa umevuka mbali sana. Wale amabo muko tayari msisite kuwasiliana name kwa ajili yah ii shuhulu ya blogging mana kuna blogs ambazo ni bure.

11. PROOF READING: Wale wataalamu wa ngwini hata hii page zangu 2 nilikuwa nahitaji mtu wa kuzikosoa ili zisomeke vizuri alafu nakulipa. Sasa ukitafuta mtandaoni hupati hata mmoja MKO WAPI? Fungua jitangaze buree huko mitandaoni matangazo madogo zoom ni buree. Mtaji hapa ni elfu20 tu ya kununua dictionary ya TUKI na ile ya oxford pocket size

12. PROJECT WRITE UP, BUSINESS PLANNING AND RESEARCH Uandisgi wa miradi ya kibiashara, ya kijamii (projects) na utengenezaji wa bajeti, ma inginia, wahasibu, sosiolojia na walimu hii inawahusu sana. Anza na miradi idogo midogo kama ya biashara yako mwenyewe angalia mtandaoni wanaandaje miradi na je unaweza kutetea mradi wako ukapewa hela? Tafuta maresearch mbalimbali jiunge nao hata kwa bure ili upate uzoefu mwisho utazipiga mwenyewe.

13. ELECTRONICS TECHNICIAN: Wanafunzi wa IT narudi tena kwenu, sim BUNI BIDHAAu za wanafunzi wenu, TV na music system nani anatengeza? Kwa nin msitengeneze wenyewe?

14. PRODUCT DESIGN BUNI BIDHAA: Hapa mi ndio napenda mfano sabuni ya kuogea inayozuia mbu wasikungate, kifaa kinachogundua mwongo mahakamani. Unda bidhaa, iamagine, imagine, ota, ota, ota. Unda bidhaa uza kwa wenye pesa

15. TUTION: Hapa sina la kuongeza, lakini pia jaribu MOBILE TUTIONING kupitia whatsapp. Malipo yatafanyika kwa Mobile Money.

Nina uhakika katika haya machache kuna lako umelipata, ukiwa hujapata rudia kusoma siku nyingine, rudia tena na tena. MNAKARIBISHWA WOTE KATIKA DARASA LETU LA UJASIRIAMALI LA WHATSAPP LA WANAFUNZI NA WANACHUO TU TUMA NENO STUDENT WITH A MISSION KWENDA 0752 693 692.

blog STUDENT WITH A MISSION
pia facebook tafuta students with a mission au Anko J
 
emalau

JF-Expert Member
Apr 25, 2009
2,723
2,000
Business start with idea, if you don't have idea there is no way we can help you. Waswahili wanasema aliyenacho uongezewa, sasa wewe huna hata wazo la biashara fulani unataka sisi tuanzie wapi?
 
CHASHA FARMING

Verified Member
Jun 4, 2011
6,866
2,000
True kama ulivyo Jibiwa hapo, The best Aidea hutoka kwaoko mwenyewe na si kokote kule, Na jambo jingine ambalo Wabongo wengi hatujui ni hili la Biashara

- Biashara yoyote inahitaji Care kubwa sana na especially hizi biashara Ndogo ambazo ndo zinaanza, Makampuni makubwa kama IPP na kazalika hyahitaji Mengi kuwa mtendaji wa kila siku kwa sababu tiyali ni kampuni kubwa na imeisha jitawanya vya kutosha na ku sub contact

- Biashara nyingi za wabongo hufa kwa sababu ya Kuongozwa kwa Limoti Contro, Mtu anafungua Biashara yake yeye yuko Bise ofisini anabakia kupiga simu kuulizia leo wamekuja wateja wangapi, mara leo imepanda ikashuka,

- Wewe kama initiator wa Aidea ni lazima uwe kwenye Biashara yako full time make wewe ndo mwenye wazo la Biashara na wewe ndo unamikakati ya wapi unataka kuwa miaka mitano ijayo
1. Mfanya kazi hawezi jua wewe una mikakati gani kwa miaka kumi ijayo
2. Mke hawezi jua
3. Rafiki, shemeji, Dada, kaka hawawezi jua

Na biashara nyingi sana hufa kwa sababu hii ya Kuongoza kwa LIMOTI CONTRO ni lazim wewe usimamie Biashara yako kwa sababau your the one who know everything about your Business Aidea,

So mkuu hakuna Biashara yoyote ile hapa Duniani ambayo haipaswi wewe muanzilishi kuisimamia, zote zinatakiwa kusimamiwa na mwazilishi mpaka hapo zitakapo kuwa zimeweze kusimama, haiwezekani mtu anaanzisha Biashara leo Mchana, kesho ameisha weka Mfanya kazi/shemeji/mke/mme/mdogo wake na kazailika na yeye amesepa yuko bise, AMINI USIAMINI BIASHARA YA AINA HII NI LAZIMA IFE TU
 
Bamukunda

JF-Expert Member
Jul 3, 2011
391
500
Biashara nzuri ya kufanya kwa sasa wakati ukiwa mwanafunzi ni kusoma kwa bidii. Vingine uvifikirie baada ya kumaliza masomo. Mshika yote kwa pupa hukosa yote. Ukicheza na shule utayakumbuka maneno yangu kama dada yako.
 
CHASHA FARMING

Verified Member
Jun 4, 2011
6,866
2,000
Biashara nzuri ya kufanya kwa sasa wakati ukiwa mwanafunzi ni kusoma kwa bidii. Vingine uvifikirie baada ya kumaliza masomo. Mshika yote kwa pupa hukosa yote. Ukicheza na shule utayakumbuka maneno yangu kama dada yako.
Acha kutisha watu, kwani kusoma ukiwa unafanya kazi na kusoma ukiwa unafanya Biashara kuna tofauti? wewe utakuwa mhanga wa MFUMO WA KUJIRIWA,

Ni vizuri sana kufanya BIASHARA UKIWA CHUONI kwa sababu hata ukimaliza CHUO hutakuwa na Mawazo ya wapi ni pate kazi, kuna watu huchanganyikiwa mara tu wanapo maliza paper make MAISHA YA CHUO unakuwa umeisha yazoea, na kule CHUONI umeme ulikuwa wa Bure kabisa, Maji ya kumwaga, Unadanganya ndugu wanatuma pesa, so ukimaliza huna wa kumdanganya,

So ni vyema sana kuanza maandalizi ya kujiajiri ukiwa Chuoni, ila kinacho hitajika ni mikakati mizuri tu na si kingine

ZeMarcopolo

JF-Expert Member
May 11, 2008
13,584
2,000
Kwakweli kwa kipindi cha shule hata kama ukiamua kufanya biashara basi iwe ni kispoti tu, lakini usiipe attention sana, utalost. Kwa mtaji wa 1.5mil ukimpa mtu akusimamie kuna risk kubwa zaidi, biashara inayohitaji sehemu ya kukodi hata ikiwa elfu 50 kwa mwezi, pango tu litakula 0.6mil kwa mwaka. Kwa hiyo nakushauri ufanye biashara ya kuuza vocha za kurusha mf. tigo rusha. Nunua simu ya sh. elfu 50 maalum kwa ajili ya kuwauzia wanafunzi wenzako vocha. Katika biashara ya vocha hakuna kupata hasara, ukubwa wa faida hutokana na idadi ya wateja lakini hasara hakuna kabisa. Usiuze vocha za kuscratch kwa sababu hapo unaweza kuibiwa na ukapata hasara.
 
Nzagamba Yapi

Senior Member
Sep 1, 2011
167
0
Tafuta kijiwe cha chips,kinalipa sana,tenga 1M kwa kijiwe kimoja hii inajumuisha vifaa eneo na mtaji,kwa siku tegemea 20,000X30 hukosi laki sita so kila baada ya miezi 2 utakuwa na uhakika wa kufungua kijiwe kimoja kwa mwaka utakuwa unavijiwe 5 na uzoefu wa kutosha uhakika wa laki 1 na zaidi kwa siku utakuwepo so 3M kwa mwezi uhakika unamaliza chuo una kigari chako na mtaji wa kufanya mengine makubwa

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
makeda

JF-Expert Member
Sep 4, 2012
246
225
Qualified mi nakushauri ungenunua haya mascreen makubwa hamia uswahilini uwe unawaingiza watu kuangalia movies,documentary na vitu vyote educative.jihadhari usiweke. Movie za pono utaua biashara mana watu hawatopenda uharibu watoto wao.
Au nunua haya magari yanayoendeshwa na watoto kwa remote unawapandisha watt kwa elfu au mia tano,kila weekend ukiisimamia biashara yako si haba,ila uwe patient usitake utajiri wa gafla.
Nafikiri yale magari yanayoendeshwa kwa remote unaweza yapata kati ya laki nne au zaidi inategemea,ukibahatisha promotion si chini ya laki mbili.
Km kuna mawazo ya ziada yatapatikana ntakuwekea tena.kila lakheri.
 
ZeMarcopolo

JF-Expert Member
May 11, 2008
13,584
2,000
Tafuta kijiwe cha chips,kinalipa sana,tenga 1M kwa kijiwe kimoja hii inajumuisha vifaa eneo na mtaji,kwa siku tegemea 20,000X30 hukosi laki sita so kila baada ya miezi 2 utakuwa na uhakika wa kufungua kijiwe kimoja kwa mwaka utakuwa unavijiwe 5 na uzoefu wa kutosha uhakika wa laki 1 na zaidi kwa siku utakuwepo so 3M kwa mwezi uhakika unamaliza chuo una kigari chako na mtaji wa kufanya mengine makubwa

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
Ndoto za alinacha...
 
CHAI CHUNGU

JF-Expert Member
Feb 20, 2012
7,129
2,000
habari JF,
jaman nahitaji msaada wa biashara gan nifanye ambayo haitaitaji mda wangu mwingi ukizingatia mi bado mwanafunz? Eneo nnaloishi ni dar
Mtaji nlonao ni 1.5 mill. Please msaada wa mawazo
Hiyo pesa unayohapo sasa hivi?
Njoo hapa mtaa wa MESSI UTAONA BAR IMEANDIKWA RONALDO,ingia ndani utamuona jamaa kavaa tshert imeandikwa Van Parse mezani kuna chupa17 za bia na mademu wa4 ndio mimi ili nikufundishe matumizi ya pesa kwanza kisha utajua namna ya kuitafuta.
Usichukue ela nyingi saaaaaaana!we chukua kitu kama laki6 tu,bcoz mm hapa nina kama v em v3 hivi vya kutumia leo.
 
kasopa

JF-Expert Member
Aug 29, 2010
302
195
Huu niushauri tosha kabisa kama ni mtuwakazi hiyo ndokazi hakuan hasara hapo na muda wake unakufaa mchana shule jioni biashara
Tafuta kijiwe cha chips,kinalipa sana,tenga 1M kwa kijiwe kimoja hii inajumuisha vifaa eneo na mtaji,kwa siku tegemea 20,000X30 hukosi laki sita so kila baada ya miezi 2 utakuwa na uhakika wa kufungua kijiwe kimoja kwa mwaka utakuwa unavijiwe 5 na uzoefu wa kutosha uhakika wa laki 1 na zaidi kwa siku utakuwepo so 3M kwa mwezi uhakika unamaliza chuo una kigari chako na mtaji wa kufanya mengine makubwa

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
Bamukunda

JF-Expert Member
Jul 3, 2011
391
500
Pole ndugu kwani inaonekana ni mgumu kuelewa. Akili mkichwa

Acha kutisha watu, kwani kusoma ukiwa unafanya kazi na kusoma ukiwa unafanya Biashara kuna tofauti? wewe utakuwa mhanga wa MFUMO WA KUJIRIWA,

Ni vizuri sana kufanya BIASHARA UKIWA CHUONI kwa sababu hata ukimaliza CHUO hutakuwa na Mawazo ya wapi ni pate kazi, kuna watu huchanganyikiwa mara tu wanapo maliza paper make MAISHA YA CHUO unakuwa umeisha yazoea, na kule CHUONI umeme ulikuwa wa Bure kabisa, Maji ya kumwaga, Unadanganya ndugu wanatuma pesa, so ukimaliza huna wa kumdanganya,

So ni vyema sana kuanza maandalizi ya kujiajiri ukiwa Chuoni, ila kinacho hitajika ni mikakati mizuri tu na si kingine

chigwiye

JF-Expert Member
Oct 28, 2010
353
0
Uza bia baba,a.k.a biere, carveja na vivywaj barid,hiyo inalipaga tu arimradi hukopeshi na ina wateja kbao iwe mdororo wa uchumi au high.Issue ni strategic place tu
 
Makirita Amani

JF-Expert Member
Jun 6, 2012
1,460
2,000
Habari za leo mpenzi msomaji wa AMKA MTANZANIA, karibu tena kwenye kipengele hiki cha ushauri wa changamoto mbalimbali zinazotuzuia kufikia mafanikio. Kwa wiki chache zilizopita kulikuwa na makala ya ushauri kwa wanafunzi wanaoanza chuo kikuu pia tumewahi kuweka makala za ushauri kwa wahitimu wa vyuo vikuu. Leo tutatoa ushauri mwingine kwa wanafunzi wanaoendelea na masomo yao ya vyuo vikuu na vyuo vingine vya elimu ya juu.
Kabla ya kuingia kwenye ushauri huo kwanza tupate maoni ya msomaji mwenzetu;
Habari za kazi , nina kupongeza kwa makala nzuri na za kuelemisha , nina ombi moja kwako utoe makala ya biashara gani au ujasiriamali gani mwanafunzi wa chuo Kikuu anaweza kufanya huku anaendelea kusoma ?
Hayo ndio yalikuwa maoni ya msomaji mwenzetu aliyetaka kujua ni biashara gani au ujasiriamali gani mwanafunzi wa chuo anaweza kufanya.
Kuna maswali matatu muhimu ya kujiuliza katika swala hili;
[h=1]Swali la kwanza, je inawezekana kufanya biashara au ujasiriamali ukiwa mwanafunzi wa chuo?[/h]
Kwa kuwa mimi ni mmoja wa watu ambao naamini hakuna kinachoshindikana ikiwa mtu atakuwa na nia ya dhati, jibu ni ndio, inawezekana. Japokuwa inawezekana sio rahisi, inahitaji kujitoa kweli na kujituma katika sehemu zote mbili, masomo na biashara.
[h=1]Swali la pili, je mwanafunzi wa chuo kikuu ana muda wa kutosha kufanya masomo na biashara pia?[/h] Kabla ya kusema ndio au hapana tuangalie kwanza muda uliopo. Kwa Tanzania vyuo vina mihula miwili na kila mhula una siku 120 au 140 kwa wenye mihula mirefu. Hivyo kwa mihula miwili ni siku karibu 300 na hivyo mwanafunzi anabaki na miezi miwili kwa mwaka ambayo hana masomo kabisa. Tukija kwenye muda wa siku, katika masaa 24, darasani anatumia masaa yasiyozidi 8, kulala yasiyozidi 8, kujisomea mwenyewe hayazidi 4 na kupumzika masaa 2. Jumla hapo ni masaa 22 na hivyo kubaki na masaa 2 kwa siku. Hapo bado hatujahesabu siku za mwisho wa wiki ambapo mwananfunzi anaweza kupata masaa zaidi ya 5.
Hivyo basi muda upo na mwanafunzi anaweza kupata masaa yasiyopungua mawili kila siku ya wiki na yasiyopungua matano kila siku ya mwisho wa wiki. Masaa haya yasiyopungua 20 kwa wiki yanamtosha kuwekeza kwenye biashara bila ya kuathiri masomo yake.
[h=1]Swali la tatu; ni biashara gani anazoweza kufanya mwanafunzi wa chuo kikuu?[/h] Baada ya kuona kwamba inawezekana kufanya biashara huku unasoma na baada ya kuona unaweza kupata muda wa kutosha kufanya biashara na kusoma pia swali la msingi ni je ufanye biashara gani?
Kuna biashara nyingi sana unazoweza kufanya kulingana na kile unachopenda wewe na hata vipaji vyako. Kwa kifupi nikushirikishe baadhi ya biashara ambazo mwanafunzi wa chuo kikuu anaweza kufanya kwa muda huo alionao.
1. Biashara ya mtandao(network marketing).
Hii ni biashara ambayo mwanafunzi anaweza kuifanya kwa muda mchache kila siku au kila wiki na baada ya mwaka au miaka miwili akawa ametengeneza mafanikio makubwa. Hii ni biashara ambayo unatengeneza mtandao wa watumiaji wa bidhaa au huduma na hivyo wanaponunua biashaa au huduma hiyo wewe unalipwa kamisheni. Kuna makampuni mengi yanafanya biashara hii kwa hapa kwetu Tanzania, zifuatilie vizuri kampuni hizi na chagua ni ipi unayoweza kuingia na kufanya biashara. Mbali tu na kufanya biashara pia utajifunza biashara katika ulimwengu halisi.
ANGALIZO; Ukiwauliza watu kuhusu biashara hii watakukatisha tamaa sana kwa sababu wengi wa waliofanya biashara hizi wameshindwa kwa sababu mbalimbali, wewe unaweza kama ukiamua.
2. Ujasiriamali wa taarifa(information entrepreneur).
Hii ni biashara ambayo unatoa taarifa mbalimbali ambazo zinaweza kuwasaidia watu na hatimaye wakawa tayari kukulipa au ukafaidika kwa njia nyingine. Kuanza biashara hii unachagua ni aina gani ya taarifa ambazo unapenda kufuatilia au kutoa kisha unaanzisha blog ambayo utakuwa unatoa taarifa hizo. Ukitoa taarifa nzuri utapata watembeleaji wengi na hatimaye unaweza kuwauzia bidhaa au huduma nyingine au kuuza nafasi za matangazo kwenye blog yako hiyo na ukapata kipato kizuri.
Kujifunza jinsi ya kuanzisha blog na kufanya biashara hii pata kitabu; Jinsi ya kutengeneza fedha kwenye mtandao kwa kutumia blog.
3. Endeleza vipaji vyako.
Kila mmoja wetu ana vipaji au vitu fulani anavyopendelea kufanya. Unaweza kutumia muda huu wa chuo kuendeleza vipaji vyako na kuangalia ni jinsi gani unaweza kuwafanya watu wakulipe kupitia kipaji chako, Unaweza kuwa na kipaji cha kuimba, kuigiza, mitindo, kuandika na kadhalika. Weka muda maalumu wa kuendeleza kipaji chako kila siku. Kwa mfano kwa wanaopenda kuandika nashauri utenge saa moja kila siku kwa ajili ya kuandika tu, kwa njia hii utaboresha uandishi wako.
4. Fanya biashara inayohusiana na TEHAMA
Teknolojia ya habari na mawasiliano(IT & ICT) bado inakua kwa kasi sana. Kama unapenda kutumia kompyuta au mtandao unaweza kufanya biashara nzuri sana inayohusisha IT. Unaweza kujifunza vitu kama kutengeneza picha(graphic design), kutengeneza website, kutengeneza program za kompyuta na hata za simu(mobile app). Ukishajua kutengeneza vitu hivi na ukawa mbunifu unaweza kutengeneza biashara nzuri na kubwa sana.
5. Uchuuzi wa kawaida.
Unaweza pia kufanya biashara nyingine ndogo ndogo kwa maeneo ya chuoni au unakoishi. Angalia ni bishaa au huduma gani wanafunzi wanazihitaji ila wanazikosa au hawazipati kwa kiwango kizuri kisha ingia kwenye biashara hiyo na toa huduma nzuri sana. Utatengeneza biashara nzuri na yenye faida.
[h=1]Mtaji wa kuanzia unatoa wapi? [/h] Hili ni swali ambalo baadhi wameshajiona kwamba hawawezi kufanya biashara hizo kwa sababu hawana mtaji. Biashara zote nilizozungumzia hapo zinaanza na mtaji kidogo sana na nyingine kama ujasiriamali wa taarifa unaweza kuanza bila hata ya mtaji ni wewe na kopmyuta yako tu. Lakini zile zinazohusisha mtaji kidogo unaweza kuupata kama ukifuata ushauri niliotoa kwa wanafunzi wanaoanza chuo kikuu.
Hizo ndizo baadhi ya biashara ambazo mwanafunzi wa chuo kikuu anaweza kufanya. Kumbuka sio biashara hizo tu ndio zinawezekana, bali hizo ni chache ambazo nina uhakika zinawezekana. Hivyo kama una wazo lako jingine la biashara bado unaweza kulifanyia kazi.
Pia biashara hizo sio rahisi, ila kama umedhamiria kweli na ukajituma kweli inawezekana.
Na utakapoanza maisha hayo ya kusoma na kufanya biashara kuna vitu unatakiwa uache, baadhi ni, kuangalia tv, movie, mipira, kuperuzi mitandao muda wote n.k
ZIADA; Ushauri niliotoa hapa hauwezi kuwa sawa kwa kila mtu na wewe kama mwanafunzi wa chuo kikuu unaweza kuangalia ni kipi kinaweza kufanya kazi kwako na kisha kukibopresha zaisi kulingana na mazingira uliyopo. Kama unaendelea kupata shida kujua ni biashara gani unaweza kufanya katika mazingira uliyopo tafadhali wasiliana nami kwa email amakirita@gmail.co au 0717396253.
Nakutakia kila la kheri katika mafanikio ya masomo yako na biashara yako.
TUPO PAMOJA.
Kama una changamoto ambayo inakuzuia kufikia malengo yako unaweza kuitoa kwa kubonyeza maandishi haya na kujaza fomu. Changamoto yako inaweza kuwa moja makala zijazo kila siku ya jumatatu. Kama unahitaji ushauri wa haraka wasiliana na mimi kwa kwa email amakirita@gmail.com au simu 0717396253/0755953887.
 
Mouramo

Member
Aug 28, 2013
39
0
Safi netwotking marketing ni safi kwa wanafunzi tunao na wanatoka kw haya maisha njoo ujiunge ORIFLAME
Hii ni networkin marketing pekee ambayo ni easy to join na kukua in one month unaweza kukua hata kwa cheo cha manager kujiunga elfu 9 tu unapata catalogue yako na price list
 
ANKOJEI

JF-Expert Member
Nov 11, 2010
702
250
ZAMA NDANI

MIRADI MIDOGO MIDOGO 15 YENYE KUZALISHA KIPATO KIKUBWA KWA AJILI YA WAJASIRIAMALI
WANAFUNZI NA WANACHUO
STUDENTS WITH A MISSION1.MLM: Hi ndio biashara moja ambayo wanafunzi wengi ulaya wanapiga pesa sana sasa hivi imefika Tanzania na Kenya: Nchini Nigeria mamilionea wengi vijana wametokea katika mtandao huu. Kenya pia na SA vijana wengi wamejikita katika biashara hii

NAMNA YA KUANZA: Kwa kifupi biashara hii unahitajika kuwa mwanachama wa kampuni inayo sambaza bidhaa kwa mtindo wa MLM, ndipo ununue bidhaa katika bei ya chini uzitumie au uuze kwa rejareja. Na kisha ualike watu wengine wengi nao wawe wanachama wa kampuni hiyo ya MLM, kila mwanachama unaye mwalika utalipwa kiasi flani cha pesa yake ya manunuzi ya bidhaa. Mtaji wa kuanzia katika kampuni hizi ni SIFURI had Million 10. KAMATA FURSA

KWA NINI WANAFUNZI/WANACHUO? Haihitaji mtaji mkubwa incase huna, haihitaji muda mwingi, hauhitajiki leseni wala huhitaji mwuza duka. Kuna uwezekano mkubwa wa wewe kufanya biashara na dunia nzima katika sekunde moja kama utafuata mbinu utakazofundishwa. Makapuni yanayojihusisha na biashara hizi yamejikita katika bidhaa za afya, urembo, kilimo na sasa muda wa Maongezi.

UWEZEKANO WA KIPATO: SIFURI hadi BILLIONEA ndani ya siku 30 hadi miaka mitano. Utaweza kuona kama mwanafunzi ukiingia katika biashara ya MLM mwaka wa kwanza na ukatumia boom lako vizuri utakapokuwa unamaliza chuo utakuwa unatengeza pesa sawa na mtu aliyeaajiriwa au umemzidi kabisa.
SECRET BEHIND SUCCESSFUL PEOPLE: Kuzungusha mtaji mara nyingi, kualika watu wengi kwa kadri inavyowezekana. Kama mwanachuo au mwanafunzi hili ni jambo rahisi una marafiki wengi sana mliosoma na mnaosoma nao pamoja.
Kwa maelekezo zaidi tembelea facebook page ‘STUDENT WITH A MISSION’

2. MOBILE MONEY: MPESA, EAZY PESA, TIGO PESA NA AIRTEL MONEY, Hii inajulikana sana but ili upige pesa vizuri inabidi uwe na float nzuri hapo chuoni kwako kuanzia 1,000,000 hadi 10,000,000 kwa siku. Na kama upo karibu na benki au super dealer iyo itakuwa safi. Faida ni kubwa mfano mtaji wa 300,000 sehemu ya mtaani tu inakupa 45,000 hadi 120,000 kwa mwezi. Mungu akupe nini? Gunia la chawa. Biashara hii ni rahisi sana kwa mwanafunzi maana unatembea na duka lako, muuzaji wewe wateja unao kila saa darasani, lecture room, discussion, disco na nyumba za ibada. KAMATA FURSA

3. MUDA WA MAONGEZI (AIRTIME): KAMATA FURSA HII, sio ile ya zamani ambayo unauza vocha za kukwangua hapa ni muda wa Maongezi. Ukisha kuwa na mobile money basi wewe jiunge na RIFARO Africa utapiga pesa kama upo ZANTEL, TIGO na AIRTEL. Kifupi ni kwamba maradi wa kwanza apo juu MLM unauunganisha na huu wa 3. Lazima utapiga hela. Unahitaji matji kidogo tu wa SH150,000 tu. Kwa maelezo zaidi google Rifaro Africa au whatsapp or text me +255 752 693 692 starting with a word “student with a mission”

4. UANDISHI WA VITABU au DOCUMENTARY: Haya vijana wa IT na wale watundu wa simu na computer, wale mnaopenda umbea na udaku sasa umbea na uduku uweke kitabuni kwa staili tofauti. Andika story za maisha, umeshazisikia ama wewe mwenyewe au zile za kufikirika, weka kwenye laptop yako au flash disk uza kwa wachapishaji. Inaweza kuwa short story au series ili mradi iwe ya kuvutia. Jifunze namna rahisi ya kutengeneza documentary za kuvutia kisha rusha facebook na mitandao ya kijamii wafanya biashara watakutafuta kwa ajili ya kutengeneza matangazo yao mbalimbali ya kibiashara ili wayatumie facebook na whatsapp.

5. UTUNZAJI BUSTANI wewe kijana wa SUA wewe inakuhusu nenda mjini tafuta watu wanohitaji kutunziwa bustani zao za nyumbani hasa UKOKO, unda team za vijana wasimamie mara kwa mara. Hii biashara inalipa sasa ivi town. Wewe kazi yako ni mipango tuu – aka – Manager. Mbolea za maji safi kabisa ambayo unaweza weka mfukoni sasa zipo Tanzania, lita moja inatosha ekari 2 na ushee

6. BETTING MKEKA: Vijana hapa sina la kuongeza mana wengi mnapiga hela weeend kama hamna akili nzuri, kuna betting website mbili Tanzania ambazo zipo juu (1) MERIDIAN (2) MBET na moja haiko online (3) PREMIER BETTING. Kama unataka kupunguza risk ya kupoteza cheza online betting ingawa premier betting nayo ni bomba vijana mnaijua. ONYO betting ni addictive na unaweza poteza boom lako usipokuwa makini, be responsible.

7. DALALI: Chagua eno lako moja la udalali hasa hasa unalolijua sana, kama magari, computer, simu, viwanja yaani vile vitu watu wanavitafuta na vina bei kubwa. Tumia blogs, face book, jamii forum na matangazo madogo magazetini kuuza. Hapa unaweza piga pesa ndefu ya kutosha mwaka wa masomo

8. MC: Nasema kama wewe ni mdakuzi na m – mbeya wacha kuumiza shingo na kichwa kwa umbeya wako, tengeneza hela kuwa MC mataji kidogo unahitajika nguo za kazi, mike ya kisasa na music system. Anza na vipati vidogo vidogo kama birthday parties, mikutano midogo, send offs na hatimaye utajikuta upo harusini, mikutano mikubwa ya injili na international meeting

9. NM – Network marketing, hii sawa na udalali ila hapa unauza vitu vyako matandaoni tu, yaani matangazo yako yote yapo mtandaoni, wateja wako wote wako mtandaoni. Wewe unacheza na simu na laptop, au tablate au hizo computer za chuo. Tembea na mooderm muda ukifika wa kuuza unaunga modern unapiga kaz le say 1 hour per day inatosha, wenye shida watakutafuta. Kama huna bidhaa ya kuuza nitafute nikuelezee bidhaa lukuki za kuuza huko mitandanoni.

10. BLOGGER: Sasa unaweza ku blogg kwa raha zako au kublog kwa kuuza products ikiwa utakuwa umechagua moja kati ya miradi hii hapa 1,4,5,7,8,9,11,14,15 basi ili uuze usiku na mchana huna budin kuwa na blog ya kukutangazia bidhaa zako dunia nzima 24/7. Hapo utakuwa umevuka mbali sana. Wale amabo muko tayari msisite kuwasiliana name kwa ajili yah ii shuhulu ya blogging mana kuna blogs ambazo ni bure.

11. PROOF READING: Wale wataalamu wa ngwini hata hii page zangu 2 nilikuwa nahitaji mtu wa kuzikosoa ili zisomeke vizuri alafu nakulipa. Sasa ukitafuta mtandaoni hupati hata mmoja MKO WAPI? Fungua jitangaze buree huko mitandaoni matangazo madogo zoom ni buree. Mtaji hapa ni elfu20 tu ya kununua dictionary ya TUKI na ile ya oxford pocket size

12. PROJECT WRITE UP, BUSINESS PLANNING AND RESEARCH – Uandisgi wa miradi ya kibiashara, ya kijamii (projects) na utengenezaji wa bajeti, ma inginia, wahasibu, sosiolojia na walimu hii inawahusu sana. Anza na miradi idogo midogo kama ya biashara yako mwenyewe angalia mtandaoni wanaandaje miradi na je unaweza kutetea mradi wako ukapewa hela? Tafuta maresearch mbalimbali jiunge nao hata kwa bure ili upate uzoefu mwisho utazipiga mwenyewe.

13. ELECTRONICS TECHNICIAN: Wanafunzi wa IT narudi tena kwenu, sim – BUNI BIDHAAu za wanafunzi wenu, TV na music system nani anatengeza? Kwa nin msitengeneze wenyewe?

14. PRODUCT DESIGN – BUNI BIDHAA: Hapa mi ndio napenda mfano sabuni ya kuogea inayozuia mbu wasikung’ate, kifaa kinachogundua mwongo mahakamani. Unda bidhaa, iamagine, imagine, ota, ota, ota. Unda bidhaa uza kwa wenye pesa

15. TUTION: Hapa sina la kuongeza, lakini pia jaribu MOBILE TUTIONING kupitia whatsapp. Malipo yatafanyika kwa Mobile Money.

Nina uhakika katika haya machache kuna lako umelipata, ukiwa hujapata rudia kusoma siku nyingine, rudia tena na tena. MNAKARIBISHWA WOTE KATIKA DARASA LETU LA UJASIRIAMALI LA WHATSAPP LA WANAFUNZI NA WANACHUO TU TUMA NENO – ‘’STUDENT WITH A MISSION’’ KWENDA 0752 693 692.

blog https://studentwithamissionwordpresscom.wordpress.com/

pia facebook tafuta students with a mission au Anko J
 
nashukuru mzima

JF-Expert Member
Jul 11, 2017
219

Top Bottom