Msaada/ushauri juu ya wapangaji wangu

Majimengi22

Member
Aug 30, 2016
9
2
Jamani mimi nina ya kupangisha nina wapangaji 7 japokuwa nyumba sio ya kisasa saaana lakini nina tatizo moja. Kuna baadhi ya wapangaji wamepanga hapa kwa muda mrefu sana sasa tumekuwa kama ndugu lakini tatizo sasahivi hawataki kunipa kodi kama inavyotakiwa.

Na mimi nawaonea huruma sijui aibu siwezi kuaambia wahame. Sasa tatizo limekuja mtaro wa kuzuia maji umeharibika wamenipgia simu wameniambia wanahitaji nitengeneze huo mtaro na pesa hawajanipatia bado nawadai pesa nyingi.

Wengine wamekaa huu mwez wa 4 hawajatoa kodi... NIFANYE NINI JAMANI.
 
Jamani mimi nina ya kupangisha nina wapangaji 7 japokuwa nyumba sio ya kisasa saaana lakini nina tatizo moja. Kuna baadhi ya wapangaji wamepanga hapa kwa mda mrefu sana sasa tumekuwa kama ndugu lakini tatizo sasahivi hawataki kunipa kodi kama inavyotakiwa... Na mimi nawaonea huruma sijui aibu siwez kuaambia wahame... Sasa tatizo limekuja mtaro wa kuzuia maji umeharibika wamenipgia simu wameniambia wanahitaji nitengeneze huo mtaro na pesa hawajanipatia bado nawadai pesa nyingi... Wengine wamekaa huu mwez wa 4 hawajatoa kodi... NIFANYE NINI JAMANI.
 
Uliwapangisha kwa mkataba?

Wafuate sheria za Mkataba ikiwemo kulipa kodi
 
umesema una nyumba ya kupangisha na wapangaji saba..
~Bila shaka unalipia Mapato,MAJI taka na ukarabati Mdogo mdogo

~angalia madhumuni ya kuwa na hiyo nyumba ni kama 'assets' kwako au ni 'liability'

Ushauri: kama hiyo nyumba ni assets kwako na iko centre na hujambembeleza mpangaji aje apange kwako na vipato wanavyo;WATIMUE wote...

'baba mwenye nyumba ukiwa zezeta wapangaji wako lazima wakutie madole'
 
Ukute kila ukikwama wanakutoa mdogo mdogo halafu huzipigii hesabu we unataka kodi yako tu.. lazima wagome
 
Yaani unakuja kututangaza kama unatudai ela yenye ni ya mwezi mmoja acha zako nitenda kuwaambia wapangaji wenzangu tabia yako
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom