Msaada: Usaili Ubalozi wa Marekani!

Msaada: Usaili Ubalozi wa Marekani!

Ndugu wanajamii, kuna jamaa yangu ana mpango wa kufanya safari mwezi Disemba kwenda U.S.A kumtembelea rafiki yake. Katika kuomba kibali ametakiwa kwenda kufanya Usaili ubalozini kwao sasa hafahamu ni kitu gani kinaulizwa! Tafadhali mwenye kujua hili naomba msaada ili ajue nini cha kuanzia kujiandaa!

Vipi mkuu, jamaa yako alifanikiwa kupata kinyago cha mpapure ?
 
Mshomba, raia wa US wakitaka kuja huku hawaombi kwenye balozi zao bali kwenye balozi yetu washingto, ama consulate office yetu pale New York.

Ushaur mwingine kwa muuliza swali, ni vizuri huyo rafiki yako wa America awe ni Mmarekani mwenzao, ama kama ni taifa lingine awe yuko established kieleweke, ama kama ni watu wetu wa ubalozi pia. Siri nyingine jaribu sana kuomba visa ya muda mfupi kuliko kuomba ya miezi, say uzoefu unaonyesha hata ukiomba visa ya wiki mbili chances are watakupa ya miezi mitatu. Lakini kama walivyosema wengine hakuna kanuni, it is highly personalised depending on the chemistry between you and the interviewer, jaribu kuwa factual zaidi kuliko kuleta hadithi. Kwa mfano kama unajiweza ni vizuri uombe visa ya matembezi ukaseme ninahamu tu ya kuifahamu amerika kuliko kutaja watu ambao hawako strong kwa maana kwamba hawako serikalini kule ama raia wa kudumu kule. Kuwa mwangalifu kama jamaa yako anabangaiza na karatasi hazijakaa vizuri unaweza ukamponza pia. Otherwis inawezekana kabisa kupata, nenda usiwe na hofu, kama passport yako in a visa za nchi nyingine itakuweka mahali pazuri
 
Hapo hakuna visa ndugu yangu. We unasema rafiki? Mie uncle wangu kabisa ninekwama. Nimepeleka hati ya nyumba leseni ya biashara cheti cha ndoa vyeti vya kuzaliwa watoto wawili mkataba mnono wa kazi bank statement iliyonoga na clearance ya polisi. Wakasema simply 'anko wako kakaa US miaka 6 sasa ni bora yeye aje kutembelea ndugu zake na sio weww kwebda huko' jamaa fedhuli kisha akaita mutu ingine...mie nikapewa kapaspoti kangu.

Wacha uongo, kunyimwa visa kunatokana na mambo mengi. Kwanza jinsi unavyojieleza usitake kutoa information ambazo hujaulizwa. Jibu swali na kumbuka ulijibu nini kipindi cha nyuma anaweza kuuliza swali hilo mara mbili au zaidi yaani mwanzo wa mahojiano na katikati kama vile amesahau. Jitahidi kuwa fluent katika lugha ya mahojiano kama huwezi omba uwe na mkalimani. Muda utakaokaa kule, Je, wewe unafanya kazi gani hivi sasa, wakati haupo utakuwa kwenye likizo au vipi? Kumbuka likizo za Tanzania ni za miezi wakati huku Alaska likizo inaweza kuwa wiki moja, siku moja wiki mbili nk. ni adimu kupata likizo ya mwezi mzima, yaani unachukua wiki moja mwezi huu then baada ya miezi mitatu unachukua wiki mbili nk. Wengi wananyimwa viza kwa kuchukua likizo zao kwa mkupuo ati mwezi mzima, wanakuwa na mashaka.

Ukiomba wiki moja au mbili mara nyingi utapata kwa sababu wanaona uko more genuine huwezi kuzamia. Kumbuka vile vile wenzetu wanatumia video camera tangu unaingia kwenye mahojiano hadi unaondoka kuwa mwangalifu .... ... uwe na heshima kwenye nchi za watu. Usifikiri kama Tanzania jinsi wanavyowaabudu wageni. (Maana yake ukiwa pale ubalozini ni kwao fahamu uko nchi ya watu wengine).

Je, utakapokuwa kule utakuwa na fedha kiasi gani kwa matumizi? Usipeleke statement inayoonyesha wewe una mpunga mwingi lakini uelewa wako ni sifuri .... ...mashaka . ... ..kama kwenye account yako kwa mfano kuna kama $5000.00 halafu uvaaji wako ni wa mashaka mashaka na huna confidence sahau kupata VISA. Do not over hype your status.

Vile vile kumbuka Tanzania wengi wanasema .... .. I am on leave .... ..... waambie I am on holiday for 10 days, or I will be on holiday for ... .. ... .... Ooops BTW kumbuka usimwambie ntu JF watukutu wengi. khe khe khe khe kheeeeeeeeeeee happy days the VISA is yours ... ..
 
hawa jamaa wanabana ile mbaya kwenda kwao

hivi kweli kwenye ubalozi wetu huko usa kunakufanyiwa usaili kwa wamarekani wanaotaka kuja bongo? au ndiyo tunakwenda kuwa tangazia waje bongo
 
hivi kweli kwenye ubalozi wetu huko usa kunakufanyiwa usaili kwa wamarekani wanaotaka kuja bongo? au ndiyo tunakwenda kuwa tangazia waje bongo

Hakuna hicho kitu!
Wamarekani wanapata visa on arrival!
Nenda kwenye website ya ubalozi wa tz utaona kuwa european woote visa ni kilipia hela mbuzi tu wakifika airport wanapewa kiulainii!
Hakuna cha enterview wala uharo!

Sisi bado ni watumwa kwa taarifa yako!
 
Na vip kuhusu lugha gongana wakati wa mahojiano haiwezi ikawa mojawapo ya tatizo ukizingatia english ya majority
ambayo ni ya ku unga unga, Napenda kuwakilisha.
 
Hapo hakuna visa ndugu yangu. We unasema rafiki? Mie uncle wangu kabisa ninekwama. Nimepeleka hati ya nyumba leseni ya biashara cheti cha ndoa vyeti vya kuzaliwa watoto wawili mkataba mnono wa kazi bank statement iliyonoga na clearance ya polisi. Wakasema simply 'anko wako kakaa US miaka 6 sasa ni bora yeye aje kutembelea ndugu zake na sio weww kwebda huko' jamaa fedhuli kisha akaita mutu ingine...mie nikapewa kapaspoti kangu.


Kwani ni lazima kwenda huko Marekani? Mimi huwa nikipita nje ya balozi na kuwakuta watanzania wamepigwa foleni na wamejikunyata kisawasawa huwa ninahuzunika sana? Ni muhimu sana kwenda huko kwao??? Huu ni utumwa na ukoloni mamboleo, tutengeneze kwetu hapa bongo pawe pazuri na pavutie!
 
Maswali yatalenda hapa - anakwenda kufanya nini? Atakaa muda gani? Nani anagharamia safari yake? Ushahidi kuwa atarudi. Ajiandae kuonyesha document za kusupport majibu yake - Mfano proof kuwa utarudi (ties to Tanzania) barua ya kazi, properties na familia. Nani atagharamia safari - bank statement (at least three months) kuonyesha unayo pesa, pia mwenyeji wake US akileta barua kuonyesha atakaa wapi akiwa US itasaidia otherwise kama utakaa hoteli bank statement itabidi ionyeshe pesa ya kutosha na arrangement za hoteli. Interview zinatofautiana kutegemea na mtu utakayekuiterview na wewe mwenyewe. Anaweza asiulize kuona document yoyote na ukapewa visa au ukanyimwa.
Intiiiooo IniBiiii

Copy that ....!ebhana cna cha kuongeza hapo....!msikilize huyu jamaa...!
 
Acha kujidanganya wewe kinachotakiwa ukamilishe makaratasi, nenda basi umevaa msalaba halafu hauna bank statement huone kama utapata viza.

Teh teh teh teh teh!

Hawa hesabu zao ni kuwa wamarekani wanawapenda wakristo!
Wamesahau kuwa wale jamaa hawana dini.
 
Vp kuhusu VISA ya SOMALIA?..Nipe dodoso fupi kuhusu interview zao..nasilisha wakuu..
 
Ukitapata mwaliko kutoka US na huyo mtu akaji Commit kugharamia safari yako hapo ni lazima upate visa.
 
hivi kweli kwenye ubalozi wetu huko usa kunakufanyiwa usaili kwa wamarekani wanaotaka kuja bongo? au ndiyo tunakwenda kuwa tangazia waje bongo

si sie kila siku tunasema waje watalii so tumejirahisisha ile mbaya aisee......
 
Somalia nenda tu interview kukwepa na kurusha gruned kama ukiwa fit karijbu somal land

Hio ni kazi ya wanamme!
Sio nyie mkiskia baruti tu! Mnalala mbele!
Teh teh teh teh!
Si ndo maana ccm imeshawajulia!
Mkianzisha hivo vi mikutano vyenu tu!
Wanamtuma afande Rika!
Anakuchomekeeni ka baruti kadogo tu!

Mavi ndoo!
Teh teh teh!

Msomali mpaka akimbie labda uje na B52 BOMBER JET!

Tunawaita "watoto wa baba"
 
Ukitapata mwaliko kutoka US na huyo mtu akaji Commit kugharamia safari yako hapo ni lazima upate visa.

Askudanganye mtu!
Halafu huko mnataka kwenda kufanya nini!?
Mi nimeona vijana waliondoka waungwana!
Wanerudi na vihereni maskioni na vidole juu!
Sijui waliwapa chakula gani huko wakalegea kiasi hicho!
Manake hayo mataifa teule balaa!
Uliberali mpaka kwenye nyumba ya bwana!
 
Askudanganye mtu!
Halafu huko mnataka kwenda kufanya nini!?
Mi nimeona vijana waliondoka waungwana!
Wanerudi na vihereni maskioni na vidole juu!
Sijui waliwapa chakula gani huko wakalegea kiasi hicho!
Manake hayo mataifa teule balaa!
Uliberali mpaka kwenye nyumba ya bwana!

Tehe tehe tehe! Naona unawapa chembe kidevu mkuu kahtaan
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom