Msaada: Usafiri mzuri from Dar to Geita

Msaada: Usafiri mzuri from Dar to Geita

geita ipo mkoa gan?

Geita ni mkoa, inapakana na mikoa ya mwanza upande wa mashariki, kagera - magharibi, shinyanga kusini na ziwa victoria upande wa kaskazini.
 
Panda noah zipo nyingi tu hapa runzewe,i hope na ww upo hapa hapa runzewe..!!
 
geita ni mkoa mpya kutoka mwanza na unapakana na mwanza,shinyanga,kagera na kigoma,karibu usukumani usihofu kwa kiluga mtaani jifunze tu!
 
uhurumoja

msisahau kufunga mkanda ukiwa kwenye basi...
uwe na hela ya ziada maana basi linaweza kuharibika njiani.
usibebe mizigo mingi maana ndio kwanza unaenda kwa mara ya kwanza.
Pia umwombe Mungu awasafirishe salama maana ajali siku hizi ni tishio.
 
Last edited by a moderator:
Karibu geita ndugu ila jiandae kupauka na vumbi,
 
Duu, Geita, Geita....

Mwenzetu unaendaKO Geita. Kuna mananasi matamu sijapata kuona. Kunako majaliwa ntarudi tena hivi karibuni.

Mabasi yapo mengi na hasa kwa kupitia Mwanza. Unanunua ticket na unaTUMBUKIAMO.
 
uhurumoja

Mabasi kutoka Dar/Moro hufika hapa Mwanza kuanzia saa nne usiku. Nakushauri ukifika tu Mwanza ulale maeneo karibu na stendi ya Nyegezi (mahala utakaposhukuia).

Mahala hapa pana Guest za kutosha maeneo ya karibu yake na gharama zake ni kuanzia 18,000/= single per day. Asubuhi ukiamka panda basi la kuelekea Kagera na ushukie Geita mjini,nauli yake ni 5000 tu.

NB; hapa Mwanza stendi utakutana na ma agents wa NSSF (usiku) wakidai kukupokea na kukutafutia malazi wewe mwalimu mpya,epukana nao. Safari njema na Karibu Geita.
 
Last edited by a moderator:
Acha ushamba wewe usafiri mzuri ni ndege tu. Achana na hayo mabasi mabovu yenye umri wa miaka 30 na masereva walevi wa milungi. Hakuna usafiri hapo. Panda ndege mpk mwanza then unachuku tax kwenda geita derever tax anaendesha unser your control



kwa hiyo anayeendesha tax anaitwaje? je una uhakika hatumii ulivyovitaja? je muuliza swali hajui kwamba kuna usafiri huo? yawezakana angesema atumie treni ungemshangaa.anyway hizo ni fikra zako
 
Asanteni sana ipi ni njia bora kati ya dar mwanza geita au dar geita moja kwa moja# kama naenda dar mwanza kisha mwanza geita itachukua Mda gani na kufika geita na moja kwa moja itachukua mda gani
 
Panda Lushanga,fikia KM Hotel ipo jirani kabisa na stendi chumba 25,000/=,karibu sana Geita mkuu
 
Ukipangiwa Geita mjini,njoo PM nikupe ramani ya vyumba usihangaike na madalali,vipi una kadi ya Chadema?
 
Ukipangiwa Geita mjini,njoo PM nikupe ramani ya vyumba usihangaike na madalali,vipi una kadi ya Chadema?Muhimu sana hiyo
 
Nakuhakikishia Mr eddy kutoingia majaribuni kwa makahaba hao vipi nikiwa maeneo hayo naweza kutumia mitandao yote ya simu au panabagua baadhi hii ni kwa eneo lote la geita#nitarajie nini niwapo maeneo hayo.

Suala la mtandao kwa Geita town hakuna shida labda ukipangiwa Izumacheli
 
Back
Top Bottom