Msaada: Usafiri mzuri from Dar to Geita

uhurumoja

JF-Expert Member
Mar 2, 2014
5,077
8,907
Habari ndugu,

Natarajia kusafiri kuelekea Geita siku ya Jumanne, naomba kujua basi zuri kwa safari na pia nauli yake na jambo lolote la kutakiwa kujua niwapo kwenye safari hiyo.

Sijawahi kabisa kwenda huko ila nimepangwa huko kikazi na natarajia kuanza maisha yangu huko. Sio mbaya mkinijulisha na Guest nzuri ikiwa nitafika usiku.

Asanteni sana
 
Kwa usafiri wa geita lipo bus la Lushanga na MJ express, unataka kufikia guest au hotel? kama ni hotel si vibaya ukafikia Green Leaf Hotel.
 
Asante Mr eddy natarajia kufikia sehem ambayo ni salama zaidi kulingana na mazingira ya mji sababu ni mizigo na kesho yake (j5) natarajia kuacha hapo mizigo ili kufatilia mambo ya kazini kama usajili kisha mizigo nichukue baadae kwa uzoefu wako naomba uniambie kipi bora kati ya hotel au guest
 
Pia nijulishe nauli na gharama za sehem ya kulala Sio mbaya ukaniambia na Mda ambao gari hutumia njiani mpaka kufika geita mjini.
 
Asante Mr eddy natarajia kufikia sehem ambayo ni salama zaidi kulingana na mazingira ya mji sababu ni mizigo na kesho yake (j5) natarajia kuacha hapo mizigo ili kufatilia mambo ya kazini kama usajili kisha mizigo nichukue baadae kwa uzoefu wako naomba uniambie kipi bora kati ya hotel au guest

Kama unamizigo ya thamani kama laptop ipad etc ni vyema ukafikia Green Leaf Hotel, kuhusu bei sasa hivi huduma nyingi zinapanda bei kutokana na kuporomoka kwa fedha hivyo sina bei za karibuni ila ni kati ya elfu 20 na elfu 50,

basi linaondoka ubungo saa 12 linafika kahama saa nne usiku munalala kwa bus kesho yake asubuhi linaendelea na safari. Kama hauna vitu vya thamani basi ukifikia MK hotel, Gold Leaf Hotel au ambassador resort sio mbaya ila pale kuna machangudoa wa kinyarwanda unaweza ingia mtegoni.

Njia nyingine ni kupanda basi za mwanza unalala kesho yake unapanda bus za bukoba utafika kwa mwendo wa raha.
 
Acha ushamba wewe usafiri mzuri ni ndege tu. Achana na hayo mabasi mabovu yenye umri wa miaka 30 na masereva walevi wa milungi. Hakuna usafiri hapo. Panda ndege mpk mwanza then unachuku tax kwenda geita derever tax anaendesha unser your control
 
Kwa akili yako kupanda basi ni ushamba kisa baba yako ameiba hela za serikali hazina kazi ?? Mwenzio ni mtoto wa mkulima kutoka Singida anakwenda kuanza kazi Geita. Uliambiwa kuna uwanja wa ndege Singida. Watu wanakula mlo mmoja kisa mshahara hautoshi wewe unasema kupanda basi ni ushamba ?????? Look at yourself
 
Acha ushamba wewe usafiri mzuri ni ndege tu. Achana na hayo mabasi mabovu yenye umri wa miaka 30 na masereva walevi wa milungi. Hakuna usafiri hapo. Panda ndege mpk mwanza then unachuku tax kwenda geita derever tax anaendesha unser your control
Kaka budget yangu ni ndogo sana kiasi cha kuweza kumudu hizo gharama una lolote zaidi la kunishauri kuhusu safari yangu nje ya hapo#unakaribishwa
 
Nakuhakikishia Mr eddy kutoingia majaribuni kwa makahaba hao vipi nikiwa maeneo hayo naweza kutumia mitandao yote ya simu au panabagua baadhi hii ni kwa eneo lote la geita#nitarajie nini niwapo maeneo hayo.
 
uhurumoja

Panda bus la [happy nation, kidia one expres au kisbo] hadi mwanza utalala gesti kesho yake utapanda kosta kutoka mwanza nyegezi hadi geita kupitia sengerema. mara nyingi hata mimi ndio ninaotumia kutoka dar to sengerema.
 
Last edited by a moderator:
Nakuhakikishia Mr eddy kutoingia majaribuni kwa makahaba hao vipi nikiwa maeneo hayo naweza kutumia mitandao yote ya simu au panabagua baadhi hii ni kwa eneo lote la geita#nitarajie nini niwapo maeneo hayo.

Karibu Geita mkuu hapa mitandao yote ni full coverage na ukiwa mjini yote ni 3g hapa kuna watu wa mataifa mbalimbali sababu ya mgodi wa GGM hivyo Maisha yapo juu kiasi hasa nyumba
 
Panda bus la [happy nation, kidia one expres au kisbo] hadi mwanza utalala gesti kesho yake utapanda kosta kutoka mwanza nyegezi hadi geita kupitia sengerema. mara nyingi hata mimi ndio ninaotumia kutoka dar to sengerema.
Asante mkuu nadhani hiyo itanirahisishia kiasi flani mwanza nina idea napo gharama za mwanza to geita zikoje na itachukua Mda gani kufika hapo geita kutokea mwanza.
 
Karibu Geita mkuu hapa mitandao yote ni full coverage na ukiwa mjini yote ni 3g hapa kuna watu wa mataifa mbalimbali sababu ya mgodi wa GGM hivyo Maisha yapo juu kiasi hasa nyumba
Tutapambana tu kaka vipi kuhusu swala la usalama hasa maeneo ya pembezoni mwa mji hasa ukizingatia kwa taaluma yetu unaweza angukia huko.
 
Maeneo ya pembezoni si mabaya kivile na yanafikika kwa urais pia usalama ni mzuri hasa kama utakuwa mwalimu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom