Tatizo kama hilo linasababishwa na yafuatayo:
1) Line kuwa na wateja wengi sana bila kuwa na mechanism ya kuboost umeme kwenye distribution transformer ( or Transformer capacity is too low to supply your load), ( Solution hapo ni kampuni husika kuongeza line nyingine au kuongeza uwezo wa transformer ingawa hata mteja anaweza kufanya kama ulivyofanya wewe lakini kunakuwa na limitation mfano huwezi kuboost umeme wa kiwango chochote).
2) Wateja kutumia vifaa vyenye kuchukua mkondo wa umeme (current drawn become so high,loads with reactive power or low power factor load), (solution hapo ni mteja kuwa na michanism kama zako za kutumia voltage regulators but also if the source ni ile number 1, kampuni ndo inatakiwa kughulikia).
3) Inawezekana wiring ya nyumba yako pia siyo nzuri, inabidi upime kama iko safi au la. How? Unazima kila kitu ndani, then unacheki kama mita bado inatembea ujua kuna inshu na wiring yako.
Matatizo yote hayo yawezekana siyo source ya tatizo lako, solution ya uhakika ni kureport tatizo lako kwenye kampuni inayokupatia umeme waje wasolve tatizo.
Sikushauri kukimbia tatizo kwa kuhamia line nyingine kwani utakuwa hujawatendea haki wenzako, kaeni chini mreport tatizo lenu Tanesco idara ya matengenezo au emergency group, am sure the problem will be solved na mtaishi kwa amani mtaani kwako.