Msaada: Ulimi wa mwanangu haunyanyuki

Keben

JF-Expert Member
Dec 21, 2012
725
173
-Tongue-Showing.jpg
Nina mtoto wa kiume ana miezi mitano awali kina mama moja wa mtaani aliniambia ulimi wa mwanao haunyanyuki hivyo akatwe kidogo ili asiwe bubu.

Lakini huyo mama nikampuuzia nikampeleka hospitali wamcheki lakini doctor akasema mtoto hana shina ila akaniambia nirudi akiwa ana miezi mitano maana wakati huo alikuwa na miezi minne.

Leo anamiezi mitano nikamrudisha hospitali na wanasema kweli anatatizo. Je ni kweli atakuja kuongea akikatwa? kama ni bubu mbona anasikia?
 
Ataongea fanya mambo fasta ila itapendeza wakitumia mwimba wa mti maalum badala ya wembe amabao huenda ukawa na vimelea vya tetenasi au kansa
 
. Je mtoto ananyonya vizuri ziwa la mama?

.Ukuaji wake uko vizuri? Uzito unaongezeka ipasavyo?

. Je ananyonya kwa mda mrefu huku akipumzika mara kwa mara

. Je mtoto anaonyesha dalili zakutokushiba vizuri, na kulia lia

. Je akiwa analia unaona ulimi unachomoza nje?

Kama mtoto anaendelea na ukuaji mzuri haimsumbui ningekushauri umwache hadi afikishe mwaka ndio ukamfanyie marekebisho.

Sababu wakati mwingine hii kitu hujirekebisha yenyewe na mara nyingi haisumbui kwenywe uongeaji wa mtoto.

Iwapo utaamua kumrekebisha kwa sasa, usihofu ni marekebisho madogo sana na hayata sababisha alazwe hospitali ila waweza kwenda na kurudi siku hiyo hiyo na kwa kawaida itachukua mda mfupi kupona na maisha yataendelea.

Ondoa hofu yakusikiliza maneno ya jirani kuwa mtoto atakuwa bubu, mfurahie Mwanao kwa sasa na kumbuka panarekebishika .
 
Asante yote unayouliza yako salama hofu yangu ilikuwa kwenye speech development ila mtoto anasikia vizuri
 
Asante. Yote unayouliza yako salama hofu yangu ilikuwa kwenye speech development Ila mtoto anasikia vizuri
mpeleke CCBRT watakusaidia kuna kesi nyingi sana kama hizo wamekutana nazo usipuuze jambo hilo utakuja kumlostisha mtoto kuongea
 
Huo ni udata, mpeleke wakamkate hako kanyuzi,ataongea fresh tu, nina rafiki yangu nahisi walimpuuzia kumkata utotoni jinsi anavyoongea kumuelewa inahitaji umakini au kumzoea.

Madaktari wakati mwingine usiwaamin sana, mtoto wa kaka yangu alizaliwa na udata, siku ya kwenda kumuona bibi zake waligindua hilo suala, lakini madaktari wakagoma na kusema hana tatizo, ila walimsubiri akafikisha kama wiki 2 hivi wakaenda kukakata, sasa hivi yupo fresh.
 
Huo ni udata, mpeleke wakamkate hako kanyuzi,ataongea fresh tu, nina rafiki yangu nahisi walimpuuzia kumkata utotoni jinsi anavyoongea kumuelewa inahitaji umakin au kumzoea..

Madaktar wakat mwingine usiwaamin sana, mtoto wa kaka yangu alizaliwa na udata, siku ya kwenda kumuona bibi zake waligindua hilo suala, lakin madaktar wakagoma na kusema hana tatizo, ila walimsubiri akafikisha kama wiki 2 hiv wakaenda kukakata, sasa hiv yupo fresh.
Asante mkuu ila niko Mwanza ngoja nimpeleke Bugando
 
pole sana..mie pia nilizaa mtoto mwenye shida hyo..nikampelrka muhimbili wakakataa kimkata ati haiba shida...nikakaa zaid ya miez 6 haongei kitu hata kuutoa nje alikua hawezi..nikakaza moyo kondr nikamrudisha tena muhimbili..wakaniogopesha ohh tukimkata anaweza kuwa bubu... huez amini amekaa had miaka 4 hajui kuongea..haongei kbs..nikabadili hospt nikampelrka bugando..ndo wakamkata!hyo ni tongue tie mpelek watamkata...ingawa ukichelewa anakua anaongea kimajanga sana..pole sana
 
. Je mtoto ananyonya vizuri ziwa la mama?

.Ukuaji wake uko vizuri? Uzito unaongezeka ipasavyo?

. Je ananyonya kwa mda mrefu huku akipumzika mara kwa mara

. Je mtoto anaonyesha dalili zakutokushiba vizuri, na kulia lia

. Je akiwa analia unaona ulimi unachomoza nje?

Kama mtoto anaendelea na ukuaji mzuri haimsumbui ningekushauri umwache hadi afikishe mwaka ndio ukamfanyie marekebisho.

Sababu wakati mwingine hii kitu hujirekebisha yenyewe na mara nyingi haisumbui kwenywe uongeaji wa mtoto.

Iwapo utaamua kumrekebisha kwa sasa, usihofu ni marekebisho madogo sana na hayata sababisha alazwe hospitali ila waweza kwenda na kurudi siku hiyo hiyo na kwa kawaida itachukua mda mfupi kupona na maisha yataendelea.

Ondoa hofu yakusikiliza maneno ya jirani kuwa mtoto atakuwa bubu, mfurahie Mwanao kwa sasa na kumbuka panarekebishika .

Mkuu salama,

Mkuu samahani nina tatizo naomba unisaidie.
 
View attachment 722054 Nina mtoto wa kiume ana miezi mitano awali kina mama moja wa mtaani aliniambia ulimi wa mwanao haunyanyuki hivyo akatwe kidogo ili asiwe bubu.

Lakini huyo mama nikampuuzia nikampeleka hospitali wamcheki lakini doctor akasema mtoto hana shina ila akaniambia nirudi akiwa ana miezi mitano maana wakati huo alikuwa na miezi minne.

Leo anamiezi mitano nikamrudisha hospitali na wanasema kweli anatatizo. Je ni kweli atakuja kuongea akikatwa? kama ni bubu mbona anasikia?
ndio ataongea bila shida,
 
Jana amekatwa na kwa siku ya Jana alikuwa anapata shida kidogo kunyonya na nimeambiwa nirudi baada ya wiki mbili. Asanteni kwa ushauri wenu
 
Back
Top Bottom