Hapa mistake kubwa aliifanya siku alipobakwa, maana kama angelikwenda polisi kutoa taarifa, polisi wangempeleka hospitali ambako huko angepewa dawa kwa ajili ya mambo makuu mawili ambayo ni kuzuia maambukizi ya kama zinaa, na hata HIV, na pia issue ya mimba.
Lakini kama aliogopa na hakwenda basi na atulie alee mimba na baadaye Mungu ni mwema atamjalia mtoto alee na atakuwa mfariji wake kimaisha. Akitoa mimba atajuta zaidi maisha yote maana atakuwa na ajutia/anafikilia kuwa alibakwa na pia alishaua.
Mpe pole sana, ila muambie asiue, na kama wewe ndio uliyetoa huo ushauri acha kabisa kushiriki hiyo dhambi, roho ya mtu itolewe kwa mapenzi ya Mungu tu na sio vinginevyo.