Msaada tutani: Black beauty is gone

Money Penny

JF-Expert Member
Jun 20, 2016
15,921
14,820
Kuna shogangu bwana kaibiwa mume na side chic m1, siku alipomkamata mwizi akaja kuniletea kesi ya mamba kwangu, cha ajabu ni kwamba hakuliaaaaaa! kudadeki watu wanasema mume anauma ila huyu shoga hapana hajalia hata tone.

Shogangu: basi bwana Penny, juzi kati hapa, nikawa natokea shoppers plaza mbezi beach, nakuta gari ya mume imepaki, ah! nikasema hiki si changu ngoja nikampe hi mume, kufika nagonga kioo, mume hataki kufungua alafu gari naiskia ipo on kabisa, vioo vyote tinted, kasoro cha mbele, gonga hataki kufungua kioo, ilikiwa usiki saa 2, nikaenda kusimama mbele, kucheki hamad! mume yupo na kimada pembeni, walipotoka kwenye gari naona kimada namfahamu bwana nilisomaga nae IFM, amejikobooooaaa,

Kwanza nilijua ngozi yake, baada ya kufungua mlango buana na kutoka nilichooookaaa, alikuwaga mweusi IFM kama chaji ya simu za nokia zile tochi, lkn sasa hivi mweupe kama Zari wa Diamond!

9-10 kachukiza mbayaaa, bora hata angependeza, mikononi, na miguuni kwenye magoti mkorogo umedunda mweusiii. Bota hata angeenda UK akajichubua kama akina Queen Vee Bossette na Zari lakini yeye kapiga za hapa hapa Tz. Uuuwi kama zimwi

Yaliotokea pale wana JF nahisi nitayaweka kwenye stori ya side chic vs. Main chic, hapa hapatoshi

Akawa ananiuliza ivi kuna siri gani kwenye ngozi nyeupe?! Mbona wana JF walisema kuwa mtu weupe ni winter/baridi?!

Money Penny: hata sijui mpenz wangu, kwanza sifikirii kujichubua kabisaa rangi yangu maji ya kunde inanitosha kwakweli. Huyo kimada atakuwa kama wale wamama wa zamani waliokuwa wanajipaka mikorogo miaka ya 90, ukiwaangalia sasa hivi wameharibika sana usoni utadhani vibibi vya miaka 99 kumbe wana miaka 52.

Je arena ya kujichubua imerudi?! Shetani wa mwaka 90 amerudi kwenye karne ya 21?!

Msaada wenu puleees wana JF, kujichubua ngozi skuhizi ndio trend au?!

 
Black beauty tunaojikubali tupo saana tu ila wakutafuta. Wanawake hakuna tunaloweza zaidi ya kutafuta attention ya Wanaume. Makalio ndo hayo ya mchina, maziwa ndo usiseme. Ifike mahali wanaume waseme basi inatosha, la sivyo miaka kadhaa ijayo hiyo saratani zitamaliza weengi sana
 
Mm nikiiona mwanamke kajichubua tu bas yaan namdharau sijui namuonaje kwa kweli
Anzia kumdharau na Zari wa Diamond

Black beauty tunaojikubali tupo saana tu ila wakutafuta. Wanawake hakuna tunaloweza zaidi ya kutafuta attention ya Wanaume. Makalio ndo hayo ya mchina, maziwa ndo usiseme. Ifike mahali wanaume waseme basi inatosha, la sivyo miaka kadhaa ijayo hiyo saratani zitamaliza weengi sana
Meona eee ni sheedah

Wanawake weusi ni kizazi kilicho hatarini kutoweka
Kabsaa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom