BLACK LIST(UJUMBE WENYE MAUTI)

THE SPIRIT THINKER

JF-Expert Member
Sep 9, 2019
392
555
THE SPIRIT THINKER.
UTANGULIZI

Berlin, Ujerumani

SONJA VERBRUGGE HAKUWA anafahamu kwamba leo ingelikuwa ni siku yake ya mwisho kuishi duniani. Alikuwa anatembea kwa taabu kuwapita watalii waliokuwa wamefurika kwenye barabara ya Unter den Linden.

Usikurupuke, alijiambia. Lazima uwe mtulivu.

Ile meseji ya ghafla kwenye kioo cha kompyuta yake kutoka kwa Franz ilikuwa inatisha: Kimbia, Sonja. Nenda hadi Hotelini Artemisia usitoke hadi upigiwe na-

Meseji ilikuwa imekatia njiani hivyo. Kwanini Franz hakuwa amemaliza kuandika ujumbe wote? Kulikuwa na nini? Usiku uliopita alikuwa amemsikia mume wake akiongea na mtu kwenye simu kwamba Prima lazima atulizwe. Prima alikuwa ni nani?

Sonja alikuwa ameikaribia Brandenburgische, hoteli ambayo ilikuwa ni kwaajili ya wanawake tu. Nitamsubiria Franz hapo aje kunieleza kuna nini.

Wakati alipokata kona, taa za barabarani ziliwaka nyekundu. Magari yakasimama halafu ghafla mmoja kati ya watalii waliokuwa wakitembea akamsukuma barabarani. Hapohapo gari moja lililokuwa limeegeshwa kwa mbele likaanza kuunguruma na kumgonga kiasi cha kumfanya aanguke chini. Watu wakaanza kumzunguka.

“Kafa?”

“Ist ihr etwas passiert?”

“Puet-elle marcher?”

Muda huohuo ambulance fulani ilifika na kuegeshwa jirani. Wahudumu wawili walishuka kutoka kwenye ile ambulance na kuongea, “Tutamhudumia.”

Sonja alijikuta akibebwa na kuwekwa ndani ya ambulance halafu mlango wa gari ukafungwa, na dakika chache baadae gari likachochewa moto.

Sonja alikuwa amefungwa kwenye kitanda, alijaribu kujiinua. “Mimi nipo sawa. Sijaumia.” Alisema.

Mmoja kati ya wale wahudumu aliinama usoni kwa Sonja. “Kila kitu kipo sawa, Frau Verbrugge. Tulia.”

Sonja alimtazama yule mhudumu kwa mshtuko. “Umelifahamu vipi...?”

Lakini hakumaliza kauli yake. Alihisi sindano ikimchoma mkononi mwake, na dakika moja baadae alitulia tuli.

Paris, Ufaransa

MARK HARRIS ALIKUWA amesimama peke yake kwenye eneo la kuutazama mnara wa Eiffel, huku mvua ikimnyeshea. Muda hadi muda kulikuwa na radi ikipiga huku manyunyu ya mvua yakichuruzika. Lakini mawazo yake yalikuwa mbali. Akili yake yote ilikuwa ipo kwa Prima na habari ya kushtusha ambayo ilikuwa ipo mbioni kutangazwa kwenye ulimwengu wote.

Mvua ilikuwa imeanza kukata. Mark Harris aliinua mkono wake kuangalia saa. Wamechelewa. Na kwanza kwanini walikuwa wamesisitiza tukutane hapa, Usiku wa manane? Akiwa anajiuliza alisikia mlango wa mnara ukifunguka. Wanaume wawili walikuwa wanamfuata aliposimama.

Mark Harris aliwatambua, akajihisi amani. “Mmechelewa.”

“Hii hali ya hewa, Mark. Samahani.”

“Hata hivyo mmefika. Kwahivyo kikao cha Washington tayari kimepangwa?”

“Hili ndilo suala tunalotaka kuongea na wewe. Hata hivyo asubuhi tulijadiliana kwa kina sana namna ya kushughulikia hili suala na tukaamua...”

Wakiwa wanaongea, mwanaume wa pili aliyekuwa kimya alimzunguka Mark Harris kwa nyuma halafu mambo mawili yakatokea. Ilikuwa ni kwa kasi na ghafla kitu kizito kilitua kichwani kwa Mark, na muda kidogo alijisikia akibebwa na kutupwa chini kutokea ngazi ya 80 ya mnara wa Eiffel.

Denver, Colorado

GARY REYNOLDS ALIKUWA amekulia Kelowna huko Canada, jirani kabisa na Vancouver, na huko ndiko alikojifunzia urubani kwahivyo alikuwa mzoefu sana wa kupaisha ndege kwenye mazingira ya milima. Na leo alikuwa anapaisha ndege aina ya Cessna Citation II akiwa makini na milima iliyokuwa mbele yake.

Ndege yenyewe ilikuwa imetengenezwa kwaajili ya kupaishwa na marubani wawili, lakini leo hakukuwa na rubani msaidizi.

Gary alikuwa ametoa ripoti kuwa alikuwa anaelekea uwanja wa ndege wa Kennedy. Kwahivyo hakuna mtu yeyote ambaye angeweza kufikiria kumtafuta Denver.

Angeutumia muda wa usiku na dada yake, halafu asubuhi angeelekea kukutana na wenzake. Mipango yote ya kumuondoa Prima ilikuwa kamili na…

Sauti kwenye kiredio ilimkata kwenye mawazo yake, “Citation one one Lima Foxfort, hii ni sauti toka chumba cha maelekezo cha uwanja wa ndege wa kimataifa Denver, tunakusikiliza…”

Gray Reynolds alibofya kitufe. “Hii ni Citation one one Lima Foxfort, naomba kutua.”

“One Lima Foxfort, tuambie ulipo.”

“One Lima Foxfort. Nipo maili kumi na tano mashariki mwa uwanja. Umbali wa futi kumi na tano kutoka ardhini.”

Ukimya ukapita kidogo. Halafu sauti ikasikika. “One Lima Foxfort una ruhusa ya kushuka njia ya two-six. Narudia two-six.”

“One Lima Foxfort, nimeelewa.”

Ghafla na bila onyo lolote Gary aliisikia ndege ikitikisika ghafla, alipochungulia kupitia dirishani kulikuwa na upepo na ndani ya sekunde chache tu upepo mkali uliikumba ndege na kuizungusha. Alijitahidi kuvuta usukani, lakini haikusaidia chochote. Alikuwa kanaswa na hakukuwa na namna ya kuiondoa ndege. Alibofya kitufe kwenye kiredio.

“One Lima Foxfort. Nina dharura.”

“One Lima Foxfort, dharura yako ni nini?”

Gary Reynolds alikuwa anapiga kelele, “Nipo kwenye upepo mkali!”

“One Lima Foxfort, upo umbali wa dakika nne tu hadi uwanja wa ndege na hatuoni dalili ya upepo kwenye skrini zetu.”

“Sijali mnaona nini kwenye skrini. Nakuambia wewe…” Halafu sauti yake ikapanda. “Mayday! May..”

Kwenye jengo la uongozaji ndege uwanjani walitazama kwa mshtuko kadri alama ya radar ilivyopotelea kwenye skrini.

Manhattan, New York

ALFAJIRI, ENEO MOJA karibu na daraja la Manhattan unapopita mto wa mashariki kulikuwa na umati wa askari polisi waliovalia sare zao na wapelelezi kadhaa ambao hawakuwa na sare. Wote walikuwa wamekusanyika kutazama maiti iliyokuwa pembeni ya ukingo wa mto. Ni kama mwili ulikuwa umetupwa.

Asakari kiongozi wa zamu, Earl Greenburg, kutokea kikosi cha upelelezi wa mauaji Manhattan alikuwa amemaliza kutoa maelekezo ya awali. Hakuna mtu kuusogelea na kuugusa mwili hadi utakapopigwa picha, aliandika maneno fulanifulani kwenye notebook huku askari wengine wakijaribu kutafuta kama kuna ushahidi wowote. Mikono ya ile maiti iliyokuwa imekwatwa ilikuwa imewekwa kwenye mfuko wa plastiki.

Daktari Carl Ward, alimaliza uchunguzi wake wa awali. Alisimama na kujipangusa uchafu kwenye suruali yake. Akawatazama askari wapelelezi waliokuwa zamu. Wa kwanza, Greenburg, huyu alikuwa mzoefu. Halafu mpelelezi wa pili alikuwa ni Robert Praegitzer, mzee ambaye umri wake uliashiria ameona mengi sana.

Ward alimgeukia Greenburg, “Maiti ni mali yako kuanzia sasa.”

“Umegundua nini?”

“Chanzo cha kifo ni shingo iliyochomwa ncha kali kwenye mshipa wa Carotid. Magoti yake yamevunjika pia. Na mbavu kadhaa pia. Inaonesha kuna bwana alimshughulia kwelikweli.”

“Na muda aliofariki?”

Ward aliitazama maiti. “Ni ngumu kusema, pengine walimtupa hapa usiku wa manane. Ila nitakupa ripoti kamili mwili wake ukifika hospitali kwa uchunguzi zaidi.”

Greenburg aligeuza macho yake kuitazama maiti. Koti la kijivu, suruali ya bluu mpauko, na saa ya bei ghali kwenye mkono wa kushoto.

Greenburg alipiga magoti na kuanza kukagua mifuko ya koti ya ile maiti.

Kwenye mfuko mmoja alikuta kikaratasi, alikivuta halafu akakisoma. Kilikuwa kimeandikwa: Washington jumatatu saa nne asubuhi. Prima.

Alikiangalia kile kikaratasi bila kuelewa chochote.

Kwenye mfuko mwingine alikuta kikaratasi kingine. “Hii imeandikwa kwa kiitalia.” Alizungusha macho yake halafu akaita, “Gianelli!”

Mmoja kati ya maafisa alimwendea. “Naam, mkuu.”

Greenburg alimpa ile karatasi. “Unaweza kunitafsiria?”

Gianelli alisoma kilichoandikwa huku akitafsiri: Nafasi ya mwisho. Tukutane Pier Seventeen ukiwa na mzigo uliobakia au utajikuta unaogelea kama samaki.”

Robert Praegitzer alisema kwa mshangao. “Hili ni tukio la genge la kihalifu? Kwanini sasa walikuja kumtupa hapa? Sehemu ya wazi kama hii?”

“Swali zuri.” Greenburg alikuwa anaendelea kukagua mifuko ya marehemu. Alipata waleti na kuifungua. Ilikuwa imejaa pesa za noti nyingi. “Bila shaka waliofanya hivi hawakuwa na shida na hela zake.”

Alitoa kadi kwenye waleti, “Anaitwa Richard Stevens.”

Praegitzer alitetemeka, “Richard Stevens… Hilo jina kama tumelisoma juzijuzi tu kwenye magazeti.”

Greenburg alisema, “Mke wake ni Diane Stevens. Na anatoa ushahidi kwenye kesi ya mauaji ya Tony Altieri.”

Praegitzer alisema, “Ndiyo. Anatoa ushahidi dhidi ya capo di capos.”

Halafu wote wakageuka kuutazama mwili wa Richard Stevens.

TUMEANZIA HAPA .

HAKIKISHA UNASOMA KWA MAKINI. NA UKIPENDA KUSOMA TENA NITAFUTE NIPACHIKE TENA.

THE SPIRIT THINKER.
BLACK LIST(UJUMBE WENYE MAUTI)
SASA IANZE SEHEMU YA KWANZA.

1

1

Shauri la Anthony (Tony) Altieri lilikuwa linasikilizwa lilipo jengo la mahakama kuu iliyopo Manhattan. Chumba hicho kikubwa cha mahakama kilikuwa kimefurikwa na waandishi wa habari na watu mbalimbali waliokuja kujionea kilichokuwa kinaendelea.

Kwenye meza ya mtuhumiwa alikuwa amekaa Anthony Altieri, huku akionekana kama chura mnene aliyejikunyata. Macho yake tu ndiyo yalionesha yana uhai, na kila muda alikuwa anamtazama Diane Stevens aliyekuwa amekaa kwenye kiti cha mashahidi.

Pembeni ya Altieri alikuwa amekaa Jake Rubenstein, Wakili wa utetezi. Rubenstein alifahamika kwa mambo makuu mawili: Kwanza ni wateja wake mashuhuri, wengi wakiwa ni magenge ya kihalifu, na jambo la pili ni uwezo wa kuwanasua kwenye mitego iliyowanasa wateja wake.

Rubenstein alikuwa na umbo dogo na akili inayofanya kazi kwa kasi sana na fikra yake ndiyo iliyombeba. Alikuwa hakaririki. Mara nyingi angewashinda wapinzani wake kwa kutafuta udhaifu wao. Kuna nyakati Rubenstein alijiona kama simba anayenyatia windo lake tayari kwa kulirarua... au kama utando wa buibui ambao utanasa windo lake likikosea njia. Kuna muda alijiona kama mvuvi, anayetupa ndoano yake kwenye maji na kusubiria mpaka mashahidi wanase na kujiingiza kwenye mtego.

Alikuwa anamtazama shahidi aliyekuwa amesimama kizimbani. Diane Stevens. Rubenstein alimkadiria umri wake kuwa miaka thelathini. Muonekano wa kuvutia. Macho ya kijani na nywele nyeusi. Umbo la Diane pia lilikuwa ni zuri. Alikuwa amekamilika kuitwa mwanamke. Alikuwa amevaa suti nyeusi na Jake Rubenstein alifahamu fika kuna namna Diane angeweza kuteka akili za baraza. Angetakiwa kuwa makini na namna atakavyommudu. Nitakuwa mvuvi, aliamua.

Rubenstein alichukua muda wake alipokuwa akikisogelea kizimba cha shahidi, na alipozungumza sauti yake ilikuwa ni ya upole.

“Mrs. Stevens, Jana ulikiri kwamba mnamo mwezi wa kumi tarehe kumi na nne, ulikuwa unaendesha gari kusini mwa barabara ya Henry Hudson ambapo tairi lako moja liliishiwa upepo ukaamua kuegesha nje kidogo ya barabara kuu ilipo Fort Washington?”

“Ndiyo,” Sauti ya Diane ilikuwa laini.

“Nini kilikufanya usimame hapo na sio sehemu nyingine?”

“Kwa sababu ya ile pancha ilinibidi nipishe barabara kuu nisogee pembeni kidogo na kuna kinyumba nilikiona kwa mbele kidogo nikahisi kuna mtu ataweza kunisaidia hapo.”

“Lakini una fundi wako wa gari?”

“Ndiyo.”

“Na una namba zake?”

“Ndiyo.”

“Sasa kwanini haukumpigia simu?”

“Ingechukua muda mrefu mpaka afike.”

Rubenstein alianza kuongea kwa upole zaidi, “Sahihi, na pia kulikuwa kuna kinyumba karibu na ungeweza kuomba msaada hapo.”

“Ndiyo.”

“Kwahivyo ulisogea kilipo hiko kinyumba upate msaada?”

“Ndiyo.”

“Nje palikuwa na mwanga?”

“Ndiyo. Ilikuwa ni kama saa kumi na moja jioni.”

“Kwahivyo ulikuwa unaweza kuona vizuri?”

“Ndiyo.”

“Uliona nini, Mrs. Stevens?”

“Nilimuona Anthony Altieri.....”

“Oh. Ulikuwa umewahi kukutana naye kabla ya hapo?”

“Hapana.”

“Nini kilikufanya uwe na hakika kwamba uliyemuona ni Anthony Altieri?”

“Nilikuwa nimewahi kuiona picha yake kwenye gazeti na...”

“Kwahivyo unasema uliwahi kuona picha ambayo inafanana na mlalamikiwaji?”

“Kiukweli ile...”

“Uliona nini kwenye kijumba?”

Diane Stevens alivuta pumzi ndefu. Akaanza kuongea taratibu huku tukio alilolishuhudia likipita taratibu akilini mwake.

“Kulikuwa na wanaume wawili kwenye kile chumba. Mmoja alikuwa amekaa kwenye kiti, akiwa amefungwa. Altieri alikuwa kama anamhoji maswali huku wanaume wengine wawili wakiwa wamesimama pembeni yake.”

Sauti ya Dianne ikakwama. Alipoipata tena akaendelea. “Altieri alichomoa bunduki, akafoka maneno fulani, na... na akampiga risasi nyuma ya kichwa yule mwanaume aliyefungwa kwenye kiti.”

Jake Rubenstein akageuza macho yake kulitazama baraza. Walikuwa wamevutiwa na ushuhuda wa Diane.

“Ukafanya nini baada ya hapo sasa?”

“Nilikimbia kurudi nilipoiacha gari yangu na kupiga 911.”

“Halafu?”

“Nikaendesha gari kuondoka pale.”

“Huku tairi yako moja ikiwa haina upepo?”

“Ndiyo.”

Wakati wa kucheza na ndoano kidogo ndani ya maji. “Kwanini haukuwasubiria polisi wafike?”

Diane alitupa macho yake ilipokuwa meza ya utetezi. Alteri alikuwa akimwangalia kwa jicho la chuki iliyo wazi kabisa.

Diane alihamisha macho. “Sikuendelea kukaa pale kwa sababu nilihofia wangenikuta endapo wangetoka kwenye kile kijumba.”

“Jambo la busara.” Halafu sauti ya Rubeinstein ikawa na ukali kidogo. “Ila jambo ambalo nashindwa kuelewa ni kwamba polisi walipofika eneo la tukio na kwenda kwenye kile kijumba , sio tu hakukuwa na mtu mule, Mrs. Diane, ila hawakukuta hata ishara kwamba palikuwa na mtu mule ndani, achilia mbali mtu kuuliwa.”

“Siwezi ku...”

“Wewe ni msanii, sio?”

Swali lilimshtua Diane. “Ndiyo, nina...”

“Sanaa yako inakulipa?”

“Sio sana, lakini haihu...”

Ilikuwa ni wakati wa kuvuta ndoano. Samaki kashanasa!

“Umaarufu kidogo hauumizi, au sio? Nchi yote inakutazama kwenye taarifa ya habari na magazeti yanaandika kuhusu wewe tena kurasa za mbele kabisa...”

Diane alimtazama Rubeinstein kwa jicho la hasira. “Sijaja kutoa ushahidi kwaajili ya umaarufu. Siwezi kumtolea ushahidi mtu asiye na hatia aende ge..”

“Neno ni mtu asiye na hatia, Mrs. Stevens. Na nitawathibitishia mabibi na mbwana wa baraza la mahakama hii kwamba ndugu Altieri hana hatia. Asante. Umemaliza.”

Diane Stevens alipuuza maneno yale na kushuka kizimbani. Alipokikaribia kiti chake alikuwa anahema kwa hasira.

Alimnong’oneza mwendesha mashtaka, “Ninaweza kwenda?”

“Ndiyo. Nitakupa mtu akusindikize.”

“Haina haja. Nashukuru sana.”

Diane aliuelekea mlango na kutoka nje hadi yalipo maegesho ya magari mahakamani hapo, wakati huu maneno ya wakili wa utetezi yalikuwa yakipita kwenye akili yake. Wewe ni msanii, sio?... Umaarufu kidogo hauumizi, au sio? Ilikuwa ni udhalilishaji. Hata hivyo bado alikuwa ameridhika na namna alivyotoa ushuhuda wake. Alikuwa ameiambia mahakama kile alichokiona kama kilivyotokea. Anthony Altieri lazima afungwe gerezani kwa kipindi chote cha maisha yake. Lakini kila Diane alipolikumbuka jicho la Anthony, alihisi uoga fulani.

Alimpatia mhudumu wa eneo la maegesho tiketi ya maegesho na kuingia kwenye gari lake. Dakika mbili baadae, Diane alikuwa mtaani, akielekea kaskazini, kuelekea nyumbani kwake.

Baada ya mwendo kidogo barabarani, kwenye kona alikutana na alama ya Stop. Diane alikanyaga breki, na kulikuwa na kijana aliyevalia kitanashati alilisogelea gari lake.

“Samahani. Nimepotea njia.”

Diane alishusha kioo chake.

“Unaweza kunielekeza nawezaje kufika Holland Tunnel.” Yule kijana aliongea kwa lafudhi ya kiitalia.

“Ni rahisi. Pita hii njia...”

Diane hakumaliza kauli yake, yule kijana aliinua mkono uliokuwa umeshika bunduki ikiwa na kiwambo cha kuzuia sauti. “Shuka kwenye gari. Haraka.”

Diane alishtuka. “Sawa. Tafadhali.” Alipoanza kufungua mlango, yule kijana alirudi hatua kadhaa nyuma, na hapo ndipo Diane akakanyaga mguu wake kutia moto na gari likaondoka kwa kasi ya ghafla. Alisikia kioo cha nyuma kikipasuka baada ya risasi kukipiga, na mlio mwingine wa risasi ukigonga gari kwa nyuma.

Mapigo ya moyo wake yalikuwa yanaenda kwa kasi sana kiasi kwamba alikuwa anapumua kwa taabu.

Ni kweli Diane Stevens alikuwa amesoma makala kadhaa kuhusu wizi wa magari, lakini haikuwahi kumtokea hata mara moja. Na yule kijana alikuw a amejaribu kumuua. Je, wezi wa magari hufika hadi hatua hiyo? Diane aliichukua simu yake na kupiga 911. Ilichukua dakika mbili kabla haijapokelewa upande wa pili.

“Tisa moja moja. Una shida gani?”

Ingawa Diane alielezea kilichotokea, ila alijua hakuna matumaini. Yule kijana lazima alikuwa ameondoka zamani sana.

“Nitatuma afisa afike hilo eneo. Naomba jina lako, anuani na namba yako ya simu.”

Diane alitaja. Lakini alijua havikuwa na maana yeyote kwa muda ule. Aligeuka nyuma na kukiangalia kile kioo kilichopasuliwa na kutetemeka. Alitamani sana ampigie simu Richard na kumsimulia kilichotokea, lakini aliacha kwa sababu alijua Richard alikuwa anafanya kazi ya muhimu sana ofisini kwake. Kama angempigia na kumwambia kilichotokea, Richard angehuzunika na kuahirisha mambo yake ili aje kumfariji na hakutaka iwe hivyo. Atamwambia kilichotokea watakapokuwa pamoja nyumbani.

Ghafla wazo la kustusha kidogo likamjia. Inawezekana yule kijana alikuwa anamsubiria au ilikuwa ni bahati mbaya amekutana naye? Akakumbuka maneno ya Richard kipindi ambacho shauri lilikuwa linaanza: “Nadhani usiongee chochote, Diane. Utajitafutaia mabalaa.”

“Usijali, kipenzi. Altieri atapatwa na hatia na atafungwa milele.”

“Lakini ana marafiki na...”

“Richard, nisipofanya hivi nitaishi na hatia kubwa moyoni.”

Kilichotokea lazima ni bahati mbaya tu, Diane alijiambia. Altieri sio mjinga kiasi cha kufanya jambo lolote la kunidhuru, hasa wakati huu wa shauri lake.

Alikata kona kuelekea magharibi na kufika mpaka ilipo nyumba yake mashariki mwa mtaa namba sabini na tano. Kabla hajaingiza gari kwenye sehemu yake ya maegesho, aliangalia nyuma kupitia kioo cha pembeni. Kila kitu kilionekana kuwa sawa tu.

Nyumba yenyewe ilikuwa na sebule kubwa, yenye madirisha ya vioo yaliyotokea sakafuni hadi ilipo ceiling, na kulikuwa na sehemu ya kuota moto. Kulikuwa na masofa, viti, kabati ya vitabu na televisheni. Kuta za sebule zilikuwa zimepambwa na michoro ya rangi mbalimbali.

Ilikuwepo michoro ya Childe Hassam, Jules Pascin, Thomas Birch, Diane Hitchcok na ukuta mmoja ulikuwa na michoro ya Diane.

Ghorofa ya juu ilikuwa na chumba kimoja chenye bafu ndani kwaajili ya Diane, na kulikuwa na chumba kingine kwaajili ya wageni, na chumba kingine cha ziada ambako ndiko Diane alipatumia kwaajili ya kuchora. Baadhi ya michoro ilikuwa inaning’inia ukutani. Kwenye kiti kimoja wapo katikati ya chumba hicho kulikuwa na mchoro ambao ulikuwa haujakamilika. Jambo la kwanza alilolifanya Diane alipoingia ndani ilikuwa ni kuutoa ule mchoro kwenye kiti na kuweka karatasi ambayo haikuwa imechorwa chochote. Alianza kuchora sura ya yule kijana aliyejaribu kumuua, lakini mikono yake ilikuwa inatetemeka sana kiasi kwamba ilibidi aache.

***

MPELELEZI EARL GREENBURG alikuwa akiendesha gari yake kuelekea ilipo nyumba ya Diane Stevens huku akilalamika, “Hakuna kazi ninayochukia kama hii.”

Robert Praegitzer alisema, “Ni bora tuwaambie kuliko wasikie kwenye taarifa ya habari.” Akamtazama Greenburg. “Si unaenda kumwambia mwenyewe?”

Earl Greenburg alitikisa kichwa kukubali. Akajikuta anakumbuka kisa cha askari mmoja aliyeenda kumpatia Mrs. Adams taarifa kuwa mumewe ameuliwa.

***

DIANE ALISHTUSHWA NA sauti ya kengele mlangoni. Alisogea na kuuliza. “Nani?”

“Askari mpelelezi. Naitwa Earl GreenBurg. Ninaomba kuzungumza na wewe.”

Ni kuhusu tukio la kutaka kuibiwa gari yangu, Diane aliwaza. Polisi wamefika mapema.

Diane aliufungua mlango na Greenburg aliingia koridoni na kusimama mlangoni.

“Habari.”

“Wewe ndiye Mrs. Stevens?”

“Ndiyo, asante sana kwa kuja mapema. Nilikuwa nimeanza kuchora uso wa yule kijana, lakini...” Alitulia kuvuta pumzi. “Alikuwa na sura ya ajabu, ana macho ya kahawia na ana kidoti shavuni. Bunduki yake ilikuwa na kiwambo cha kuzuia sauti na...”

Greenburg alikuwa anamuangalia Diane kwa mshangao. “Sielewi unazungumzia nini?”

“Mwizi wa gari. Nilipiga 911 na...” Diane aliuona uso wa Greenburg. “Kwahivyo ujio wako hauhusu tukio la gari yangu?”

“Hapana,” Greenburg alisema. “Naweza kuingia ndani.”

“Karibu.”

Greenburg aliingia sebuleni.

Diane alikuwa anamtazama akiwa haelewei. “Kuna tatizo?”

Maneno sahihi ya kuongea yalikuwa hayamjii Greenburg. “Ndiyo. Pole. Ni- Nina habari mbaya. Ni kuhusu mume wako.”

“Kimetokea nini?” Sauti yake ilikuwa inakwaruzika.

“Amepata ajali.”

Diane alihisi baridi ikimpiga. “Ajali ya aina gani?”

Greenburg alivuta pumzi. “Ameuawa jana usiku. Mwili wake umekutwa chini ya daraja linalopitisha maji Yya mto Mashariki asubuhi hii.”

Diane alibaki ametoa macho, halafu akaanza kutikisa kichwa chake kukataa.

“Umekosea nyumba, afande. Mimi mume wangu yupo kazini, maabara kwake.”

Suala lilikuwa linaenda kuwa gumu kuliko Greenburg alivyotazamia. “Mrs. Stevens, mume wako alirudi nyumbani jana usiku?”

“Hapana. Lakini Richard mara nyingi huwa anakesha kazini kwake. Ni mtafiti.” Diane alikuwa anazidi kutafuta sababu za kukataa habari iliyoletwa.

“Mrs. Stevens unafahamu kwamba mume wako alikuwa anajihusisha na kundi la uhalifu?”

Diane alifoka. “Uhalifu? Umechanganyikiwa?”

“Tumekuta..”

Diane alikuwa ameanza kufoka tena. “Naomba nione kitambulisho chako.”

“Sawa.” Greenburg alivuta kitambulisho chake na kumuonesha.

Diane alikitazama na kukirudisha kitambulisho, halafu akampiga kofi kali Greenburg usoni. “Serikali inakulipa pesa bure ili uzunguke kuwatisha wananchi? Mume wangu hajafa! Yupo kazini.” Diane alikuwa anafoka.

Greenburg alimtazama machoni halafu akaona mshtuko na hali ya kuukataa mshtuko kwa pamoja. “Mrs. Stevens ungehitaji labda nitume mtu kwaajili ya kukuangalia na...?”

“Wewe ndiye unayehitaji mtu wa kukuangalia. Haya toka hapa.”

“Mrs. Stevens...”

“Toka!”

Greenburg alitoa business card na kuiweka mezani. “Kama utahitaji kuongea na mimi tena namba yangu ipo hapo.”

Alipotoka nje ya mlango, Greenburg alishukuru kwa kumaliza hicho kibarua.

Huku nyuma Diane alifunga mlango na kuvuta pumzi ndefu. Yule mjinga! Anakosea nyumba na kujaribu kunidanganya. Nitamripoti. Aliitazama saa yake. Richard atafika nyumbani muda sio mrefu. Ni muda wa kuanza kuandaa chakula cha jioni. Angepika paella - chakula pendwa cha Richard. Alienda jikoni na kuanza kuandaa paella yenyewe.

Kutokana na mazingira ya kisiri ya kazi ya Richard, Diane hakuwa na mtindo wa kumsumbua akiwa ofisini, na ingetokea Richard asipige simu basi ilikuwa ni ishara kwamba atachelewa kurudi. Ilipofika saa mbili kamili chakula kilikuwa tayari. Diane alikionja na kutabasamu. Kilikuwa kipo kama ambavyo Richard hupendelea chakula chake kiwe. Saa nne, na Richard hakuwa bado amewasili, aliichukua paella akaiweka kwenye jokofu halafu akaweka kikaratasi juu ya mlango wa jokofu: Mpenzi, chakula kipo ndani ya jokofu. Naomba uje kuniamsha tule wote.

Lazima Richard angekuwa na njaa wakati atakapofika.

Diane alijihisi uchovu wa ghafla. Alielekea chumbani na kuvua nguo na kuvaa gauni la kulalia, akapiga mswaki halafu akapanda kitandani. Ndani ya dakika chache tu, akasinzia na kulala fofofo.

Ilipofika saa tisa usiku, aliamka akiwa anapiga kelele za uchungu.

MIMI PIA BADO NAJIULIZA MASWALI NA BADO NIPO KWENYE MAFUMBO.

LABDA NITAELEWA HEBU NIISUBIRIE SEHEMU YA PILI ITAKUJA NA MAJIBU.

Police wa Ulaya wana nidhamu sana. They know what they are
 
2

THE SPIRIT THINKER.

BLACK LIST(UJUMBE WENYE MAUTI)

SEHEMU YA PILI.

Diane aliacha kutetemeka ilipofika alfajiri. Baridi aliyokuwa akihisi ilikuwa imehamia kwenye moyo na mifupa sasa. Ni kweli Richard alikuwa amekufa. Hakuna siku angewahi kumuona tena, au kusikia sauti yake, au kuhisi mwili wake ukigusana na mwili wa Richard. Na ni kosa langu. Sikupaswa kwenda kusimama mahakamani. Oh, Richard, Nisamehe... Tafadhali nisamehe... Sidhani kama nitaweza bila wewe. Ulikuwa ndiye maisha yangu, sababu ya mimi kuwepo. Na sasa sina hata sababu ya kuendelea kuwa hai.

Alitamani dunia ipasuke aingie.

Alitamani apotee tu.

Alitamani afe.

Alibaki amelala akitafakari kuhusu maisha yake ya zamani, namna alivyokutana na Richard na namna Richard alivyobadilisha maisha yake.

Diane West alikuwa amekulia Sands Point huko New York. Baba yake alikuwa ni daktari wa upasuaji na mama yake alikuwa ni mchoraji, na Diane alianza kuchora alipokuwa na umri wa miaka mitatu tu. Alienda shule ya St. Paul na alikuwa na matokeo mazuri chuoni kwa sababu alikuwa na mahusiano na mwalimu wake wa hesabu. Mwalimu wake huyo alimwambia anataka kumuoa kwa sababu yeye ndiye mwanamke pekee anayempenda duniani. Lakini baadae Diane aligundua mwalimu wake huyo alikuwa na mke na watoto watatu, hapo Diane akaamua labda huyo mwalimu wake alikuwa na matatizo ya kumbukumbu hivyo alichukuwa uhamisho kwenda Wellesley College.

Diane alivutiwa sana na michoro na muda wake mwingi aliutumia kuchora. Kufikia kipindi anahitimu, alikuwa ameanza kuuza michoro yake na wengi walimtazamia kama msanii mkubwa baadae.

Na msimu huo, jumba la maonesho ya sanaa Fifth Avenue art gallery ilimpa Diane nafasi ya kuandaa tamasha lake na tamasha lilifanikiwa kwa kiwango kikubwa. Mmiliki wa jumba hilo, Paul Deacon, alikuwa ni bwana mmoja tajiri aliyesaidia kwa kiasi kikubwa kukilea na kukikuza kipaji cha Diane.

Usiku wa tamasha eneo lilikuwa limefurikwa. Deacon alimfuata Diane, huku tabasamu kubwa likiwa usoni kwake. “Hongera! Tumekwishauza baadhi ya michoro yako. Nitaandaa tamasha lingine baada ya miezi michache, ukiwa tayari niambie.”

Diane alisema, “Asante sana, Paul.”

“Unastahili kila kitu.” Paul alisema na kumshika Diane begani halafu akaondoka.

Diane alikuwa anaweka sahihi yake kwa huyu na yule alipotokea mwanamume mmoja nyuma yake na kusema, “Napenda michirizi yako.”

Diane alishtuka. Kwa hasira aligeuka na kufungua mdomo wake kuongea jambo, lakini hakutoa sauti. Yule mwanaume alikuwa tayari ameanza kuongea.

“Inataka kufanana na Rossetti au Manet.” Yule mwanaume alikuwa anauangalia mchoro mmoja uliokuwa ukutani.

Diane alijizuia kwa wakati. “Oh.” Akamtazama yule mwanaume kwa umakini. Alionekana kuwa na umri kati ya miaka ya thelathini. Urefu wake ulikuwa ni futi sita na mwili wa mazoezi, na macho ya bluu iliyokoza. Alikuwa amevalia suti, shati jeupe na tai ya kahawia.

“Ahsante.”

“Umeanza kuchora lini?”

“Nilipokuwa mtoto. Mama yangu alikuwa ni mchoraji.”

Yule mwanaume alitabasamu. “Mbona mama yangu mimi alikuwa mpishi mzuri, ila mimi siwezi kupika? Jina lako nalifahamu. La kwangu ni Richard Stevens.”

Wakati huohuo Paul Deacon alifika akiwa na vifurushi vitatu. “Michoro uliyochagua hii hapa Mr. Stevens. Natumai utaifurahia.”

Richard alivyopokea vifurushi, Deacon aliondoka.

Diane alimtazama kwa jicho la mshangao, “Umenunua michoro yangu mitatu?”

“Ninayo miwili mingine nyumbani kwangu.”

“Ni- Nimefurahi kusikia hivyo.”

“Mimi nathamini sana vipaji.”

“Asante.”

Alisita kidogo, “Naona upo bize, kwahivyo nitakuacha- ”

Diane alijikuta akisema, “Hapana. Siko bize mbona.”

Tabasamu la Richard likaongezeka, “Basi unaweza kunisaidia jambo moja mrembo.”

Diane akautazama mkono wake wa kushoto. Richard alikuwa hajavaa pete. “Nakusikiliza.”

“Nina tiketi mbili kwaajili ya uzinduzi wa kinywaji cha Noel Coward kesho usiku, na sina mtu wa kwenda naye. Kama haupo bize- ?”

Diane alibaki anamtazama kwa muda kidogo. Alimuona anavutia, lakini, yote kwa yote, alikuwa hamfahamu. Hatari sana. Hatari kubwa sana, lakini mwisho wa siku alijikuta akisema, “Nitafurahi kukupa kampani.”

Jioni ya kesho yake ilitokea kuwa ya kufurahisha sana. Richard Stevens alikuwa ni mtu mcheshi, na kuna vitu vingi sana ambavyo wote walikuwa wanavutiwa navyo. Walikuwa wanapenda sanaa na muziki, na zaidi ya yote Diane alijikuta akivutiwa na Richard, lakini hakuwa na uhakika kama mwenzake alikuwa na hisia hizo kwake pia.

Mwishoni Richard aliuliza, “Utakuwa na nafasi kesho jioni?”

Jibu la Diane lilikuwa ni, “Ndiyo.”

Jioni iliyofuata walikuwa wanapata chakula cha jioni kwenye mgawa mmoja mtulivu uliopo SoHo.

“Niambie kuhusu wewe, Richard.”

“Sina historia ndefu. Nimezaliwa Chicago. Baba yangu alikuwa mhandisi wa michoro ya majengo na amefanya kazi nyingi karibu kila sehemu duniani, na mara nyingi tulisafiri naye. Nimeenda nchi nyingi na nimejifunza lugha mbalimbali kwa sababu kila tulipohama nchi nilihama na shule.”

“Unafanya nini? Kwaajili ya kipato”

“Ninafanya kazi KIG – Kingsley International Group. Ni taasisi kubwa ya utafiti na inahitaji watu wenye akili sana.”

“Acha basi.”

“Kweli. Tunanya tafiti za teknolojia ya hali ya juu. Kama tungelikuwa na kauli mbiu ingekuwa inasema, ‘Kama hatujapata jibu sasa hivi, tupeni hadi kesho tu.”

Baada ya chakula, Richard alimpeleka Diane nyumbani. Wakiwa mlangoni, aliishika mikono yake na kusema, “Nimeifurahia jioni ya leo. Asante.”

Na akaaondoka.

Diane alibaki amesimama akimtazama kwa nyuma. Nashukuru huyu bwana ni mkarimu na sio kama wanaume wengine.

Walikuwa pamoja kila usiku tangu jioni hiyo, na kila Diane alipomuona Richard alijihisi faraja kubwa.

Ijumaa moja, Richard alisema, “Huwa ninafundisha timu fulani mazoezi kila Jumamosi. Unaweza kuja kuangalia kidogo?”

Diane alijibu, “Nitafurahi, Kocha.”

Asubuhi ya kesho yake Diane alimtazama Richard akifanya mazoezi na timu ya wachezaji wadogowadogo. Alikuwa ni mpole na mwenye kujali, na ilikuwa ni wazi wachezaji wale walimpenda Richard.

Diane alijiwazia, Nimeanza kupata hisia za mapenzi kwa huyu mtu. Ninampenda!

Siku chache baadae, Diane alikuwa anapata chakula cha mchana na marafiki zake wa kike, na walipokuwa wanaondoka mgahawani hapo, njiani walimpita mnajimu mmoja.

Na kama utani Diane akasema, “Tujaribu kupata utabiri wa maisha yetu.”

“Sina muda, Diane. Mimi narudi kazini.”

“Mimi pia.”

“Ninatakiwa kumchukua Johnny shule.”

“Embu wewe nenda halafu utatuambia kakuambia nini.”

“Sawa.”

Na dakika tano baadae, Diane alijikuta akiwa amekaa peke yake mbele ya mwanamke yule mzee aliyejaa meno ya dhahabu mdomoni na uso uliochafuliwa kwa alama za michoro huku akiwa kajifunga tambala chafuchafu kichwani.

Huu ni upuuzi, Diane aliwaza. Kwanini nafanya huu ujinga.? Lakini alijua ni kwanini alikuwa anafanya huo ujinga. Alitaka kujua kama yeye na Richard wangekuwa na maisha ya pamoja siku za usoni.

Diane alimtazama yule mwanamke mzee ambaye alikuwa anachezacheza na karata bila kuunia uso wake juu.

“Nilikuwa nataka kujua kama...”

“Shh.” Yule mwanamke aligeuza karata moja. Ilikuwa ni karata yenye picha ya ‘Joker’ akiwa amevaa nguo zenye rangirangi huku kashika kishoka. Yule mwanamke mzee aliitazama kwa muda. “Kuna siri nyingi sana unatakiwa kuzijua.” Akageuza karata nyingine tena. “Hii ni mbalamwezi. Kuna mambo mengi unayohitaji na hauyajui.”

Diane alisita na kutikisa kichwa kukubali.

“Je, ujio wako hapa ni kuhusu mwanamume?”

“Ndiyo”

Yule mwanamke mzee akageuza karata iliyofuata. “Hii ni karata ya wapendanao.”

Diane akatabasamu. “Ni ishara nzuri?”

“Tutaona. Karata tatu zinazofuata zitatuambia.” Alipomaliza kuongea hivyo akageuza karata nyingine.

“Mwanamume aliyenyongwa.” Alisita, halafu akageuza karata nyingine. “Shetani,” alinong’ona.

“Ni ishara mbaya?” Diane aliuliza kwa upole.

Mnajimu hakutoa jibu lolote.

Diane aliendelea kumuangalia yule mwanamke mzee akifunua karata inayofuata.

Yule mwanamke alitikisa kichwa chake kuonesha huzuni. Sauti yake ilitoka kwa chini sana. “Karata ya kifo.”

Diane alisimama. “Muongo mtupu! Siamini chochote utakachokisema,” Aliongea kwa hasira.

Yule mwanamke mzee aliinua macho yake juu, na alipofungua midomo yake kuongea, sauti yake ilikuwa ni ya kutia mkazo. “Haijalishi unaamini nini. Ukweli ni kwamba mauti imekuzunguka kila unapokanyaga unyayo wako.”

TUTAENDELEA TENA MUNGU AKITIA WEPESI.

UKISOMA USIELEWE JARIBU KUBASHIRI TUKIO LIFUTALO MAANA UTAKUWA UMEWASAIDIA WASOMAJI WENGINE WAELEWE MAANA HATA MIMI BADO NAJIULIZA MASWALI,

SEHEMU YA TATU INAANDALIWA BADO........................
 
THE SPIRIT THINKER.
UTANGULIZI

Berlin, Ujerumani

SONJA VERBRUGGE HAKUWA anafahamu kwamba leo ingelikuwa ni siku yake ya mwisho kuishi duniani. Alikuwa anatembea kwa taabu kuwapita watalii waliokuwa wamefurika kwenye barabara ya Unter den Linden.

Usikurupuke, alijiambia. Lazima uwe mtulivu.

Ile meseji ya ghafla kwenye kioo cha kompyuta yake kutoka kwa Franz ilikuwa inatisha: Kimbia, Sonja. Nenda hadi Hotelini Artemisia usitoke hadi upigiwe na-

Meseji ilikuwa imekatia njiani hivyo. Kwanini Franz hakuwa amemaliza kuandika ujumbe wote? Kulikuwa na nini? Usiku uliopita alikuwa amemsikia mume wake akiongea na mtu kwenye simu kwamba Prima lazima atulizwe. Prima alikuwa ni nani?

Sonja alikuwa ameikaribia Brandenburgische, hoteli ambayo ilikuwa ni kwaajili ya wanawake tu. Nitamsubiria Franz hapo aje kunieleza kuna nini.

Wakati alipokata kona, taa za barabarani ziliwaka nyekundu. Magari yakasimama halafu ghafla mmoja kati ya watalii waliokuwa wakitembea akamsukuma barabarani. Hapohapo gari moja lililokuwa limeegeshwa kwa mbele likaanza kuunguruma na kumgonga kiasi cha kumfanya aanguke chini. Watu wakaanza kumzunguka.

“Kafa?”

“Ist ihr etwas passiert?”

“Puet-elle marcher?”

Muda huohuo ambulance fulani ilifika na kuegeshwa jirani. Wahudumu wawili walishuka kutoka kwenye ile ambulance na kuongea, “Tutamhudumia.”

Sonja alijikuta akibebwa na kuwekwa ndani ya ambulance halafu mlango wa gari ukafungwa, na dakika chache baadae gari likachochewa moto.

Sonja alikuwa amefungwa kwenye kitanda, alijaribu kujiinua. “Mimi nipo sawa. Sijaumia.” Alisema.

Mmoja kati ya wale wahudumu aliinama usoni kwa Sonja. “Kila kitu kipo sawa, Frau Verbrugge. Tulia.”

Sonja alimtazama yule mhudumu kwa mshtuko. “Umelifahamu vipi...?”

Lakini hakumaliza kauli yake. Alihisi sindano ikimchoma mkononi mwake, na dakika moja baadae alitulia tuli.

Paris, Ufaransa

MARK HARRIS ALIKUWA amesimama peke yake kwenye eneo la kuutazama mnara wa Eiffel, huku mvua ikimnyeshea. Muda hadi muda kulikuwa na radi ikipiga huku manyunyu ya mvua yakichuruzika. Lakini mawazo yake yalikuwa mbali. Akili yake yote ilikuwa ipo kwa Prima na habari ya kushtusha ambayo ilikuwa ipo mbioni kutangazwa kwenye ulimwengu wote.

Mvua ilikuwa imeanza kukata. Mark Harris aliinua mkono wake kuangalia saa. Wamechelewa. Na kwanza kwanini walikuwa wamesisitiza tukutane hapa, Usiku wa manane? Akiwa anajiuliza alisikia mlango wa mnara ukifunguka. Wanaume wawili walikuwa wanamfuata aliposimama.

Mark Harris aliwatambua, akajihisi amani. “Mmechelewa.”

“Hii hali ya hewa, Mark. Samahani.”

“Hata hivyo mmefika. Kwahivyo kikao cha Washington tayari kimepangwa?”

“Hili ndilo suala tunalotaka kuongea na wewe. Hata hivyo asubuhi tulijadiliana kwa kina sana namna ya kushughulikia hili suala na tukaamua...”

Wakiwa wanaongea, mwanaume wa pili aliyekuwa kimya alimzunguka Mark Harris kwa nyuma halafu mambo mawili yakatokea. Ilikuwa ni kwa kasi na ghafla kitu kizito kilitua kichwani kwa Mark, na muda kidogo alijisikia akibebwa na kutupwa chini kutokea ngazi ya 80 ya mnara wa Eiffel.

Denver, Colorado

GARY REYNOLDS ALIKUWA amekulia Kelowna huko Canada, jirani kabisa na Vancouver, na huko ndiko alikojifunzia urubani kwahivyo alikuwa mzoefu sana wa kupaisha ndege kwenye mazingira ya milima. Na leo alikuwa anapaisha ndege aina ya Cessna Citation II akiwa makini na milima iliyokuwa mbele yake.

Ndege yenyewe ilikuwa imetengenezwa kwaajili ya kupaishwa na marubani wawili, lakini leo hakukuwa na rubani msaidizi.

Gary alikuwa ametoa ripoti kuwa alikuwa anaelekea uwanja wa ndege wa Kennedy. Kwahivyo hakuna mtu yeyote ambaye angeweza kufikiria kumtafuta Denver.

Angeutumia muda wa usiku na dada yake, halafu asubuhi angeelekea kukutana na wenzake. Mipango yote ya kumuondoa Prima ilikuwa kamili na…

Sauti kwenye kiredio ilimkata kwenye mawazo yake, “Citation one one Lima Foxfort, hii ni sauti toka chumba cha maelekezo cha uwanja wa ndege wa kimataifa Denver, tunakusikiliza…”

Gray Reynolds alibofya kitufe. “Hii ni Citation one one Lima Foxfort, naomba kutua.”

“One Lima Foxfort, tuambie ulipo.”

“One Lima Foxfort. Nipo maili kumi na tano mashariki mwa uwanja. Umbali wa futi kumi na tano kutoka ardhini.”

Ukimya ukapita kidogo. Halafu sauti ikasikika. “One Lima Foxfort una ruhusa ya kushuka njia ya two-six. Narudia two-six.”

“One Lima Foxfort, nimeelewa.”

Ghafla na bila onyo lolote Gary aliisikia ndege ikitikisika ghafla, alipochungulia kupitia dirishani kulikuwa na upepo na ndani ya sekunde chache tu upepo mkali uliikumba ndege na kuizungusha. Alijitahidi kuvuta usukani, lakini haikusaidia chochote. Alikuwa kanaswa na hakukuwa na namna ya kuiondoa ndege. Alibofya kitufe kwenye kiredio.

“One Lima Foxfort. Nina dharura.”

“One Lima Foxfort, dharura yako ni nini?”

Gary Reynolds alikuwa anapiga kelele, “Nipo kwenye upepo mkali!”

“One Lima Foxfort, upo umbali wa dakika nne tu hadi uwanja wa ndege na hatuoni dalili ya upepo kwenye skrini zetu.”

“Sijali mnaona nini kwenye skrini. Nakuambia wewe…” Halafu sauti yake ikapanda. “Mayday! May..”

Kwenye jengo la uongozaji ndege uwanjani walitazama kwa mshtuko kadri alama ya radar ilivyopotelea kwenye skrini.

Manhattan, New York

ALFAJIRI, ENEO MOJA karibu na daraja la Manhattan unapopita mto wa mashariki kulikuwa na umati wa askari polisi waliovalia sare zao na wapelelezi kadhaa ambao hawakuwa na sare. Wote walikuwa wamekusanyika kutazama maiti iliyokuwa pembeni ya ukingo wa mto. Ni kama mwili ulikuwa umetupwa.

Asakari kiongozi wa zamu, Earl Greenburg, kutokea kikosi cha upelelezi wa mauaji Manhattan alikuwa amemaliza kutoa maelekezo ya awali. Hakuna mtu kuusogelea na kuugusa mwili hadi utakapopigwa picha, aliandika maneno fulanifulani kwenye notebook huku askari wengine wakijaribu kutafuta kama kuna ushahidi wowote. Mikono ya ile maiti iliyokuwa imekwatwa ilikuwa imewekwa kwenye mfuko wa plastiki.

Daktari Carl Ward, alimaliza uchunguzi wake wa awali. Alisimama na kujipangusa uchafu kwenye suruali yake. Akawatazama askari wapelelezi waliokuwa zamu. Wa kwanza, Greenburg, huyu alikuwa mzoefu. Halafu mpelelezi wa pili alikuwa ni Robert Praegitzer, mzee ambaye umri wake uliashiria ameona mengi sana.

Ward alimgeukia Greenburg, “Maiti ni mali yako kuanzia sasa.”

“Umegundua nini?”

“Chanzo cha kifo ni shingo iliyochomwa ncha kali kwenye mshipa wa Carotid. Magoti yake yamevunjika pia. Na mbavu kadhaa pia. Inaonesha kuna bwana alimshughulia kwelikweli.”

“Na muda aliofariki?”

Ward aliitazama maiti. “Ni ngumu kusema, pengine walimtupa hapa usiku wa manane. Ila nitakupa ripoti kamili mwili wake ukifika hospitali kwa uchunguzi zaidi.”

Greenburg aligeuza macho yake kuitazama maiti. Koti la kijivu, suruali ya bluu mpauko, na saa ya bei ghali kwenye mkono wa kushoto.

Greenburg alipiga magoti na kuanza kukagua mifuko ya koti ya ile maiti.

Kwenye mfuko mmoja alikuta kikaratasi, alikivuta halafu akakisoma. Kilikuwa kimeandikwa: Washington jumatatu saa nne asubuhi. Prima.

Alikiangalia kile kikaratasi bila kuelewa chochote.

Kwenye mfuko mwingine alikuta kikaratasi kingine. “Hii imeandikwa kwa kiitalia.” Alizungusha macho yake halafu akaita, “Gianelli!”

Mmoja kati ya maafisa alimwendea. “Naam, mkuu.”

Greenburg alimpa ile karatasi. “Unaweza kunitafsiria?”

Gianelli alisoma kilichoandikwa huku akitafsiri: Nafasi ya mwisho. Tukutane Pier Seventeen ukiwa na mzigo uliobakia au utajikuta unaogelea kama samaki.”

Robert Praegitzer alisema kwa mshangao. “Hili ni tukio la genge la kihalifu? Kwanini sasa walikuja kumtupa hapa? Sehemu ya wazi kama hii?”

“Swali zuri.” Greenburg alikuwa anaendelea kukagua mifuko ya marehemu. Alipata waleti na kuifungua. Ilikuwa imejaa pesa za noti nyingi. “Bila shaka waliofanya hivi hawakuwa na shida na hela zake.”

Alitoa kadi kwenye waleti, “Anaitwa Richard Stevens.”

Praegitzer alitetemeka, “Richard Stevens… Hilo jina kama tumelisoma juzijuzi tu kwenye magazeti.”

Greenburg alisema, “Mke wake ni Diane Stevens. Na anatoa ushahidi kwenye kesi ya mauaji ya Tony Altieri.”

Praegitzer alisema, “Ndiyo. Anatoa ushahidi dhidi ya capo di capos.”

Halafu wote wakageuka kuutazama mwili wa Richard Stevens.

TUMEANZIA HAPA .

HAKIKISHA UNASOMA KWA MAKINI. NA UKIPENDA KUSOMA TENA NITAFUTE NIPACHIKE TENA.

Mpangilio wa miji, lugha na mtiririko Dope, let's go

Sent from my TA-1053 using JamiiForums mobile app
 
THE SPIRIT THINKER.
SEHEMU YA TATU.

3

Berlin, Ujerumani.

KAMANDA WA POLISI, Otto Schiffer akiwa na maafisa wa polisi wawili waliokuwa ndani ya sare zao, na msimamizi wa jengo lenyewe, Herr Karl Goetz, walikuwa wanaushangaa mwili wa maiti ya mwanamke- ukiwa uchi- uliokuwa umelala ndani ya beseni la kuogea lililokuwa linavujisha maji. Uvimbe kidogo ulikuwa umezunguka shingo ya mwanamke huyo.
Kamanda wa polisi alinyoosha kidole chake hadi kwenye mkono wa bomba lililokuwa linatoa maji. Akamaliza akanusa chupa ya kilevi iliyokuwa wazi pembeni kidogo ya beseni lile la kuogea halafu akamgeukia yule msimamizi wa jengo, “Jina lake?”
“Sonja Verbrugge. Mume wake anaitwa Franz Verbrugge. Ni mtafiti wa mambo ya kisayansi.”
“Marehemu alikuwa anaishi na mume wake?”
“Ndiyo. Wameishi hapa kwa miaka saba na walikuwa ni wapangaji wazuri. Kodi walikuwa wanalipa kwa wakati sahihi. Sikuwahi kupata shida nao. Kila mtu alipenda...” Yule msimamizi aligundua alikuwa anataka kusema nini kwahivyo akanyamaza.
“Kwani Sonja alikuwa anafanya kazi gani?”
“Alikuwa na kazi Cyberlin internet cafe, sehemu ambayo watu wanalipa ili...”
“Nini kilikufanya ukagundua kuna maiti humu?”
“Ni kwa sababu ya hilo bomba linalovujisha maji. Huwa ni bovu na nimejaribu kulirekebisha mara kadhaa ila halijakaa vizuri.”
“Kwahivyo?”
“Kwahivyo asubuhi mpangaji wa ghorofa ya chini alilalamika maji yanachuruzika kutoka juu. Ndiyo nikaja huku, nikagonga mlango, na nilipoona sijibiwi nikaufungua na funguo zangu. Nikaingia mpaka bafuni na kukuta...” Sauti yake ikakwama.

Mwanaume mwingine alikuwa ameingia mule bafuni. “Hakuna chupa za vilevi kwenye kabati au chumbani, kuna waini tu.”
Kamanda wa polisi alitikisa kichwa halafu akamgeukia tena Karl Goetz. “Unaweza ukawa unafahamu alipo Franz Verbrugge?”
“Hapana. Huwa namuona asubuhi tu akiwa anatoka kwenda kazini, lakini...” Halafu akaonesha alama ya kutokuwa wa msaada zaidi.
“Leo asubuhi haujamuona?”
“Hapana.”
“Unaweza ukawa una taarifa kwamba Franz Verbrugge alikuwa na mpango wa kusafiri labda?”
“Hapana. Sina hiyo taarifa.”
Kamanda alimgeukia yule mwanamume mpelelezi aliyekuwa ameingia muda sio mrefu. “Ongea na wapangaji wengine. Chunguza kama Sonja Verbrugee alionekana kuwa na mawazo siku za hivi karibuni, au kama yeye na mume wake walikuwa na ugomvi, na kama alikuwa ni mlevi wa pombe. Tafuta kila taarifa unayoweza kuipata.”
Halafu akamgeukia tena Karl Goetz. “Tutamcheki mume wake. Kama utakumbuka jambo lolote linaloweza kuwa la muhimu...”
Carl Goetz alisema kwa mashaka, “Sijui kama hili lina umuhimu au msaada, lakini kuna mpangaji mmoja aliniambia kuna ambulance ilionekana imeegeshwa nje, na aliniuliza kama kuna mgonjwa. Wakati ambao nilifika nje kuona nini kilikuwa kinaendelea, ile ambulance ilikuwa tayari imeondoka. Inaweza kuwa na msaada hiyo taarifa?”
Kamanda alisema, “Tutacheki pia.”
“Na vipi... Vipi kuhusu mwili wake?” Karl Goetz aliuliza kwa uoga.
“Mtu wa hospitali anakuja kufanya uchunguzi. Kwa sasa hivi uachwe hapohapo tu.”

4

SEHEMU YA NNE.
THE SPIRIT THINKER.

NINA HABARI MBAYA... Ameuawa jana usiku... Mwili wake umekutwa chini ya daraja...
Muda, kwa Diane Stevens, ulikuwa umesimama. Alikuwa anatembeatembea kwenye nyumba yake iliyojawa kumbukumbu nyingi. Nyumba haikuwa na amani tena bila Richard. Haikuwa nyumba tena ila mkusanyiko wa tofali tu. Hakuna siku nyumba ile itakuja kuwa hai tena.
Diane alikaa kwenye sofa moja wapo na kufumba macho yake. Richard mpenzi, siku tulipofunga ndoa uliniuliza ninataka zawadi gani. Nilikujibu sitaki kitu chochote ila uwepo wako tu. Ila sasa hivi kuna kitu nakitaka.
Rudi kwangu. Haijalishi kwamba sitaweza kukuona tena. Ila nataka unikumbatie mikononi mwako. Najua upo hapa. Nahitaji kujihisi unanigusa angalau mara moja tu. Nataka nihisi ninaweza kuisikia sauti yako ikisema ninajua kupika paella kuliko mtu yeyote duniani. Nataka nisikie sauti yako ikiniambia kwamba unanipenda. Alijaribu kuzuia machozi ambayo tayari yalikuwa yanatiririka, lakini hakuweza.

Kuanzia wakati ambao Diane aligundua kuwa Richard alikuwa amekufa, alitumia muda wa siku zake akiwa amejifungia ndani ya nyumba yake, bila kupokea simu au kufungua mlango ulipobishwa. Alikuwa kama mnyama aliyeumia akiwa kajificha.
Alitaka kuwa peke yake na maumivu yake. Richard, kuna nyakati nyingi sana nilitamani nikuambie nakupenda ili ujibu unanipenda pia. Lakini sikutaka kuonekana kama nina uhitaji sana. Nilikuwa mjinga.
Hatimaye simu zilipozidi sana, na mlango ulipogongwa sana, Diane aliamua kufungua mlango.
Carolyn Ter, mmoja kati ya marafiki zake wa karibu alikuwa amesimama mlangoni. Alimtazama Diane na kusema, “Umetupatia wasiwasi sana. Kila mtu anakupigia simu haupokei.”
“Samahani, Carolyn, lakini siwezi...”
Carolyn alimshika Diane mkono, “Nafahamu. Lakini unao marafiki wengi sana wanataka kukuona.”
Diane alitikisa kichwa kukataa. “Hapana. Ni...”
“Diane, maisha ya Richard yameisha, lakini yako bado hayajaisha. Usiwafungie milango watu wanaokupenda. Acha nipige simu kuwataarifu watu upo salama.”

Rafiki za Diane na Richard wakaanza kupiga simu na kuja nyumbani, na Diane akajikuta akisikiliza misemo ileile kuhusu kifo:
“Ifikirie hivi, Diane. Richard ana amani huko aliko..”
“Mungu kampenda zaidi...”
“Najua Richard yupo mbinguni anakuangalia...”
“Ameenda sehemu bora zaidi...”
“Ameungana na malaika...”
Kila mara Diane aliposikia hiyo misemo alitamani kulia kwa nguvu.
Lakini mnyororo wa wageni haukuisha. Paul Deacon, yule mmiliki wa jumba la maonesho ya kazi za sanaa alikuja pia. Alianza kuongea, “Nimejaribu kukutafuta, lakini...”
“Nafahamu.”
“Kwanza pole kuhusu Richard. Alikuwa ni mwanaume bora, lakini Diane hauwezi kukaa hivi siku zote. Watu wanatamani waendelee kuona kazi zako.”
“Siwezi kuendelea na kazi. Haina umuhimu wowote tena kwangu, Paul.”
Ilikuwa ni ngumu kumshawishi.

Siku iliyofuata kengele ya mlango ilipogongwa, Diane alienda kufungua mlango. Alichungulia kupitia kitundu kidogo mlangoni, na palionekana kama kuna kundi kubwa la watu nje.
Akiwa na mshtuko, Diane alifungua mlango. Kulikuwa na kundi la vijana nje. Mmoja kati yao alikuwa ameshika maua.

“Shikamoo, Mrs. Stevens.” Aliongea huku akimpatia yale maua Diane.
“Ahsante.” Akawakumbuka wale vijana walikuwa ni akina nani. Walikuwa ni vijana ambao Richard alikuwa anawafundisha mpira.
Kiukweli, Diane alikuwa amepokea maua yasiyo na idadi, bahasha za pole na barua pepe nyingi, lakini hii ndiyo ilikuwa zawadi iliyougusa moyo wake kuliko zote.
“Ingieni ndani,” Diane alisema.
Wale vijana walivamia sebule. “Tulitaka kukuambia tumejisikia huzuni sana.”
“Mume wako alikuwa mtu mzuri.”
“Na alikuwa ni kocha mzuri.”
Kitu pekee alichoweza kusema Diane kuzuia machozi yake ilikuwa ni, “Asante.” Halafu akaongeza, “Mngependelea vinywaji gani?”
Tim Holm alijibu kwa niaba ya wenzake, “Hapana, Asante. Tulikuja kukuambia tu tutammiss mwalimu. Na wote tulichangia kununua hayo maua.”
Diane aliwatazama na kusema kimyakimya, “Asanteni sana.”
Aliwasindikiza na kuwatazama wakiondoka. Wakati huo Diane alianza kukumbuka mara ya kwanza alivyoshuhudia Richard akiwafundisha. Akakumbuka hiyo ndiyo siku aliyoanza kumpenda Richard.

Diane alisikia muungurumo wa radi kwa nje na manyunyu yalianza kushuka kama machozi ya Mungu akihuzunika naye. Mvua! Akaikumbuka siku moja ya mapumziko walipokuwa na Richard...
“Unapenda picnic?” Richard aliuliza.
“Nazipenda ndiyo.”
Richard alitabasamu. “Nilijua. Nitaandaa picnic kwaajili yetu. Nitakupitia mchana wa kesho.”

Kesho yake ilipofika ilikuwa nzuri, yenye hali ya jua na Richard aliandaa picnic kama alivyomuahidi Diane. Kulikuwa na vikapu viwili. Diane alipoona kilichokuwemo aliishia kucheka. Kulikuwa na nyama ya kukaanga ya ng’ombe na chipsi na sahani mbili kubwa na mkusanyiko wa vinywaji kadhaa na vitinda mlo.
“Chakula kingi! Kuna watu wengine tunaungana nao”
Richard alikuwa anamuangalia. “Upo sawa?”
Nipo sawa? Sijawahi kujihisi raha hivi. “Ndiyo, Richard. Nipo sawa.”
“Hatutawasubiri wanaokuja kuungana na sisi. Tuanze kula.”
Wakiwa wanakula waliongea mengi na kila neno liliwafanya wawe na ukaribu zaidi. Kulikuwa na nguvu ya ajabu iliyokuwa inaaongezeka kati yao – kama sumaku iliyowekwa karibu na chuma, na kila mmoja aliihisi. Halafu katikati ya siku yenye anga la jua mvua ikaanza kunyesha. Ndani ya dakika moja tu walikuwa wamelowana chapachapa.
Richard alisema, “Pole sana. Sikujua hali ya hewa itabadilika – Utabiri wa hali ya hewa jana hawakutabiri mvua. Pole sana hii mvua imeharibu...”
“Imeharibu?” Diane aliuliza kwa sauti ya chini.
Na kabla Richard hajajibu, Diane alikuwa amejitupa kifuani mwake na kumkumbatia. Aliyahisi mapigo ya moyo ya Richard yakienda kasi. Alipojiachia aliongea, “Itabidi tubadilishe hizi nguo zilizolowana.”
Richard alicheka, “Upo sawa. Tunaweza kuugu..”
Diane alisema, “Kwako au kwangu?”
Hapo Richard akabaki ameganda. “Diane, una uhakika? Ninauliza kwa sababu... Isije ikawa ni tendo la moja tu.”
Diane alijibu, “Ninafahamu.”
Na nusu saa baadae walikuwa nyumbani kwa Diane, wakiwa wanavua nguo huku mikono yao ikitalii mwili wa kila mwenza katika sehemu zenye kusisimua, na hatimaye uvumilivu uliwashinda wakapanda kitandani.
Richard alikuwa mtaratibu na mkorofi na mwenye hamu na aliyeridhika, na kila kitu kilikuwa ni miujiza. Ulimi wake uligusana na mwili wa Diane ukitambaa hapa na pale na hatimaye alimwingia.
Waliutumia mchana wote, na karibu usiku wote wakiongea na kuoneshana ufundi, na wakafungua mioyo yao kupena nafasi. Na ilikuwa ni faraja kuliko maneno yanavyoweza kueleza.
Asubuhi wakati Diane akiandaa kifungua kinywa, Richard aliuliza, “Naomba nikuoe, Diane?”
Diane aligeuka akamwambia. “Hauhitaji kuomba. Sema lini?”

Na ndoa yao ilifungwa mwezi mmoja baadae. Sherehe ilifaana huku marafiki na familia zikiwapongeza wanandoa wapya. Diane aliutazama uso wa Richard na kuyakumbuka maneno ya uongo ya yule mnajimu msoma nyota na kutabasamu.
Fungate yao walipanga ifanyike Ufaransa wiki moja baada ya ndoa, lakini Richard alimpigia Diane simu kutokea kazini. “Kuna project mpya imekuja ofisini na siwezi kutoka. Unaonaje tukifanya fungate baada ya miezi michache? Samahani, mpenzi.”
Diane alijibu, “Usijali, mpenzi.”
“Ungependa tupate chakula cha mchana pamoja leo?”
“Ndiyo.”
“Kuna mgahawa unapika mapishi mazuri ya ufaransa. Nitakupitia twende tukale hapo baada ya lisaa limoja.”
Nusu saa baadae, Richard alikuwa nje akimsubiri Diane. “Za kushinda, mpenzi. Kuna mteja wa ofisini mmoja namsindikiza. Anaenda Ulaya. Tutaagana naye halafu tutaendelea na ratiba zetu.”
Diane alimkumbatia. “Sawa.”
Walipofika uwanja wa ndege wa Kennedy Airport, Richard alisema. “Jamaa ana ndege binafsi. Tutakutana naye kwa ndani.”
Mlinzi aliwaruhusu wapite kuelekea eneo ambalo ilikuwa ni marufuku kupita, ambako ndege aina ya Challenger ilikuwa imeegeshwa. “Jamaa hajafika. Itabidi tumsubirie ndani ya ndege.”
“Sawa.”

Walipiga hatua kupanda ngazi na kupanda ndege hiyo ya kifahari. Injini ilikuwa inaunguruma.
Mhudumu wa ndege alikuwepo karibu na mlango. “Habari za asubuhi.”
“Nzuri.” Richard alisema.
Diane alitabasamu, “Nzuri.”
Waliingia ndani na kumtazama mhudumu akifunga mlango.
Diane alimgeukia Richard. “Huyu mteja wenu atatumia muda kiasi gani kufika?”
“Haitomchukua muda mrefu.”
Mlio wa injini uliongezeka na ndege ikaanza kupaa.
Diane alichungulia dirishani, na uso wake ukabadilika rangi. “Richard, Ndege inaondoka.”
Richard aligeuka kumtazama Diane kwa mshtuko, “Una uhakika?”
“Angalia nje ya dirisha.” Halafu akaongeza, “Mwambie rubani.”
“Nimwambie nini rubani?” Richard aliuliza.
“Mwambie ashushe ndege chini, sisi sio abiria wake.”
“Siwezi. Ashapandisha ndege.”
Kulikuwa na ukimya halafu Diane akamtazama Richard, macho yake akiwa kayakodoa. “Tunaenda wapi?”
“Oh, sikukuambia? Tunaenda Paris. Si huwa unapenda mapishi ya ufaransa.”
Diane alishtuka. Muonekano wake ukabadilika. “Richard, Siwezi kwenda Paris sasa hivi. Sina nguo. Sijafanya make-up. Sina...”
Richard akasema, “Kuna mtu aliniambia Paris kuna maduka mengi tu ya hivyo vitu.”
Diane alimtazama kwa muda, halafu akarusha mikono yake kumkumbatia. “Nakupenda sana, Richard.”
Richard akaguna, “Ulitaka fungate. Ndiyo hii sasa.”

SEHEMU YA TANO INAANDALIWA.UNAWEZA KUNISHAWISHI ILI NIANDIKE KWA HARAKA ZAIDI. NIANDIKIE HAPA CHINI.
 
SEHEMU YA TANO.
THE SPIRIT THINKER

5

Walipofika Orly, Gari la kifahari aina ya limousine ilikuwa inawasubiria kuwapeleka ilipo Hotel Plaza Athenee.
Walipofika meneja wa hoteli alisema, “Chumba chenu kipo tayari.”
“Asante.”
Walikuwa wamewekewa chumba namba 310. Meneja aliufungua mlango na Diane na Richard waliingia. Karibu nusu ya dazani ya michoro ya Diane ilikuwa inaning’inia ukutani. Diane aligeuka akamtaza Richard. “Hii michoro imefikaje?”
Richard alijibu kwa upole, “Hata mimi sijui. Labda meneja ni shabiki yako.”
Diane aligeuka na kumbusu Richard shavuni.
Paris ilikuwa furaha tupu. Mahemezi yao ya kwanza waliyafanya Givenchy, kununua nguo kwaajili ya kila mmoja wao. Halafu wakaelekea Louis Vuiton kununua mabegi kwaajili ya kubebea nguo zao.
Walitembea matembezi ya kifahari kuanzia Champs-Elysees mpaka Place de la Concorde, walienda kuiona Arc de Triomphe, na Palais-Bourbon, na la Madeleine. Walizungukia Musee Rodin na walikula vyakula vya jioni kifahari.
Yote yalikuwa ni ya kuvutia, ila jambo moja lililomtatanisha Diane ni simu alizokuwa akipokea Richard katika masaa ya ajabu.
“Huyo alikuwa ni nani?” Diane aliuliza usiku mmoja, saa tisa usiku Richard alipomaliza kuwasiliana.
“Mambo ya kibiashara tu.”
Usiku wa manane?

“DIANE! DIANE! DIANE!”
Alishtushwa kutoka kwenye kumbukumbu zake. Carolyn Ter alikuwa amesimama mbele yake. “Upo sawa?”
“Nipo sawa.”
Carolyn alimsogelea. “Baada ya muda kidogo tu utakuwa sawa.” Halafu akaongeza, “Umejipanga vipi kuandaa msiba?”
Msiba. Neno linaloonesha huzuni kuliko maneno yote kwenye lugha zote za dunia. Neno lililobeba sauti ya kifo na mwangwi wa majonzi.
“Sijafikiria kuhusu hilo.” Anna alijibu.
Kwa umakini kidogo Carolyn aliongea, “Naweza kukusaidia. Niruhusu nikuchagulie jeneza...”
“Hapana.” Diane alisema kwa sauti yenye hasira kuliko alivyotegemea.
Carolyn alibaki anamtazama akiwa kashtuka.
Diane alipoongea tena, sauti yake ilikuwa ya kutetemeka. “Hauelewi? Hili ndilo jambo la mwisho ninaloweza kufanya kwaajili ya Richard. Ninataka msiba wake niuandae mwenyewe. Najua huko aliko atafurahi kuwaona marafiki zake wamekuja kusema kwaheri.”
Machozi yalikuwa yanachuruzikia mashavuni mwa Diane.
“Diane.”
“Pia ninatakiwa kulichagua jeneza la Richard mimi mwenyewe ili apumzike kwa amani.”
Hakukuwa na neno lingine ambalo Carolyn angesema.

Mchana huohuo, Mpelelezi Earl Greenburg alikuwa ofisini kwake simu yake ilipoita.
“Diane Stevens anataka kuongea na wewe.”
Greenburg alilikumbuka kofi la Diane ile siku alipokutana naye mara ya kwanza. Anataka nini? Aliipokea simu. “Hello.”
“Diane Stevens hapa. Nimekupigia kwa sababu mbili. Kwanza nataka kuomba msamaha. Nilionesha tabia mbovu na ninajuta kusema kweli.”
Greenburg alishtuka, “Hauna haja ya kuomba msamaha. Ninaelewa ulikuwa unapitia wakati mgumu sana.”

Akasubiria. Kulikuwa na ukimya.
“Umesema umepiga kwa sababu mbili?”
“Ndiyo. Mume wangu..” Akajizuia kulia na kuendelea, “Mwili wa mume wangu unashikiliwa na polisi. Nawezaje kuupata kwa sababu ninaandaa msiba wake na mochwari ya Dalton.”
Uchungu kwenye sauti ya Diane ulimfanya Greenburg afumbe macho kabla ya kuongea, “Mrs. Stevens, Ninahuzunika kusema kuna red tape na mpaka ofisi ya upelelezi iandike ripoti ya majibu ya chanzo cha kifo halafu ni muhimu idara fulani zi...” Hapo akatulia kwanza, na kuamua asiongee kwanza. “Najua una mambo mengi akilini sasa hivi. Niruhusu nitakusaidia mwili kuhamishwa ndani ya siku mbili zijazo.”
“Oh. Nashukuru sana.” Sauti ya Dean ilipaliwa na mawasiliano yakapotea.

Earl Greenburg alibaki akitafakari kuhusu Diane na wakati mgumu anaopitia. Halafu akaendelea na kazi yake.

MOCHWARI YA DALTON ipo upande wa mashariki mwa Madison Avenue. Ni jengo lenye ghorofa mbili liliopambwa kwa rangi za kuvutia.
Diane alimwambia mtu wa mapokezi, “Nina miadi na Jones. Mimi ni Diane Stevens.”
Yule mtu wa mapokezi alinyanyua simu na kuongea, na muda kidogo meneja wa mochwari alifika. Alikuwa ni mzee.
“Naitwa Ronin Jones. Tuliongea kwenye simu. Naelewa ni kiasi gani mambo huwa yanakuwa magumu nyakati kama hizi, na kazi yetu ni kuhakikisha tunakusaidia mzigo ulionao. Tuambie ni nini unataka na sisi tutahakikisha mahitaji yako yanatimizwa.”
Diane alisema ghafla, “Si- Sijui hata nataka nini.”
Jones alitikisa kichwa, “Labda nikufafanulie, Huduma zetu zinahusisha jeneza, kusimamia huduma ya marafiki na ndugu kumuaga marehemu, kupata eneo la makaburi, na kuzika.” Halafu akasita kabla ya kuongeza, “Kutokana na nilichokisoma kwenye magazeti kuhusu kifo cha mumeo, Mrs. Stevens, ningeshauri jeneza lake liwe limefunikwa kipindi chote cha msiba.”
“Hapana!”
Jones alimwangalia kwa mshangao, “Lakini...”
“Nataka jeneza liwe wazi. Nataka Richard aweze kuwaona wote watakaopita kumuaga kabla haja...” Sauti yake ilikwama.
Jones alikuwa anamtazama kwa huzuni. “Naona. Basi ikiwa hivyo hapa ofisini tunaye mtu wa vipodozi anayeielewa kazi yake ikiwa...” Aliyasema maneno yake kwa uangalifu, “Ikiwa atahitajika. Hiyo ni sawa.?”
Richard asingekubali, lakini – “Ni sawa.”
“Jambo moja la mwisho. Tutahitaji nguo ambazo ungependa mume wako azikwe nazo.”

Diane alimtazama kwa mshtuko, “Nguo?” Diane alihisi sio sawa mtu mwingine tu kuuchezea mwili wa mumewe hata akiwa marehemu.
“Mrs. Stevens.?”

Ninapaswa nimvalishe Richard mimi mwenyewe. Lakini siko tayari kumuona kwenye hali hiyo. Ninataka...

“Mrs. Stevens.”
Diane alimeza mate, “Sikuwa nimefikiria kuhusu hilo.” Sauti yake ilikuwa kama ya mtu aliyenigwa. “Samahani.” Hakuwa tayari tena kuendelea.

Jones alibaki anamtazama Diane akiinuka na kuondoka nje ambako alipanda taxi kwenda nyumbani kwake.

Alipofika ndani aliliendea moja kwa moja kabati la nguo la Richard. Kulikuwa na vyumba viwili vilivyojaa suti. Kila nguo ilibeba kumbukumbu. Ile suti ambayo Richard alikuwa amevaa siku walipokutana kwenye nyumba la maonesho ya sanaa ilikuwepo. Ninapenda michirizi yako. Ina ladha ya Rossetti au Manet. Angeiruhusu kweli hiyo iondoke? Hapana.

Vidole vyake viliigusa nguo iliyokuwa inafuata. Ilikuwa ni koti ya kijivu Ile nguo aliyokuwa amevaa Richard siku waliponyeshewa mvua.
Kwako au kwangu?
Hili sio tukio la mara moja tu.
Najua.

Ingewezekana vipi aruhusu hiyo iondoke?

Suti iliyofuata ilikuwa ni ile yenye mistarimistari. Unapenda chakula cha ufaransa?
Iliyofuata ilikuwa ni ya bluu... Diane aliikumbatia. Siwezi kuruhusu yeyote kati ya hizi ipotee. Kila moja ilikuwa inabeba kumbukumbu fulani ya maana.

“Siwezi.” Alisema huku akilia. Halafu akachukua suti nyigine tu iliyokuwepo humo kabatini na kuondoka.

Mchana wa siku iliyofuata, kulikuwa na ujumbe wa sauti kwenye simu ya Diane. “Mimi ni afande Greenburg. Nilitaka kukuambia kila kitu kipo tayari. Nimekwishazungumza na mochwari. Upo huru kuendelea na ratiba zako...” Halafu utulivu kidogo. “Nakutakia kila la kheri. Kwaheri.”

Diane alimpigia simu Ron Jones. “Naelewa kwamba mwili wa mume wangu umewasili hapo.”
“Ndiyo, Mrs. Stevens, tayari kuna mtu wa vipodozi anaushughulikia na nguo ulizotuma tumekwishazipata. Asante.”
“Nilikuwa najiuliza, hatuwezi kuuweka msiba ijumaa hii.”
“Ijumaa itapendeza. Kufika hiyo siku kila kitu tutakuwa tumeshughulikia ipaswavyo. Ninashauri mazishi yaanze saa tano asubuhi.”

Ndani ya siku tatu mimi na Richard tutatengana milele. Au mpaka nitakapoungana naye.

Hatimaye ilifika Alhamis. Asubuhi ya siku hiyo Diane alikuwa anamalizia mipango midogomidogo ya msiba, akithibitisha orodha ndefu ya waalikwa na wabeba jeneza, simu yake ilipoita.
“Mrs. Stevens?”
“Ndiyo.”
“Ron Jones hapa. Nilitaka kukutaarifu nimepokea nyaraka na barua yako na nimefanya marekebisho kama ulivyotaka.”
Diane alistuka, “Barua?”
“Ndiyo. Kuna taarishi aliileta jana.”
“Sijatuma kitu...”
“Kiukweli, hata mimi nilishangaa, lakini mwisho wa siku ilibidi niheshimu uamuzi wako.”
“Uamuzi wangu?”
“Tumeuchoma mwili wa mumeo lisaa limoja lililopita.”
 
SEHEMU YA SITA.
THE SPIRIT THINKER.

6

Paris, Ufaransa
Kelly Harris alikuwa ni mshumaa wa kirumi uliolipuka kwenye ulimwengu wa mitindo ya nguo. Ndiyo kwanza alikuwa na miaka ishirini na kitu tu. Msichana wa ki Afrika mwenye mchanganyiko wa Marekani. Rangi ya ngozi yake ilikuwa ni kama rangi ya asali. Alikuwa na sura ambayo mpiga picha yeyote angetamani aipige picha. Alikuwa na macho ya kahawia, midomo ya kuvutia iliyojaa, miguu ambayo wataalamu huita miguu ya bia, na umbo ambalo lilikuwa linamuahidi mwanaume yeyote raha. Nywele zake zilikuwa fupi zilizokatwa kwa ustadi kuongeza mvuto wake.

Na mapema mwaka huo, wasomaji wa magazeti ya Elle na Mademoiselle walikuwa wamempigia kura Kelly kama msichana mrembo zaidi duniani.

Alipokuwa akimaliza kuvaa, Kelly alizungusha macho kuangalia jumba la kifahari alimokuwamo na kubaki na mshangao tu. Jumba lenyewe lilikuwa ni zuri. Lilikuwa limejengwa mjini Paris. Chumba alimokuwamo kulikuwa na mlango ulioelekea hadi sebuleni ambako palikuwa na mchanganyiko wa samani za thamani sana za ufaransa. Ungesimama kibarazani mwa hili jumba, ungeiona Notre-Dame kwa uzuri kabisa.

Kelly alikuwa anaisubiria kwa hamu sana mwisho wa wiki hiyo. Mark alikuwa anakuja kumpeleaka sehemu kwaajili ya kujiachia.

Nataka uvae upendeze kabisa, mpenzi. Nina imani utavutiwa na sehemu tunapoenda.
Kelly alitabasamu. Mume wake alikuwa ni mwanaume bora duniani. Kelly aliitazama saa yake ya mkononi na kuguna. Bora nianze kwenda, alijisemea. Onesho linaanza baada ya nusu saa. Dakika chache baadae alikuwa anakiacha chumba chake kwenda ilipo lifti. Akiwa anaondoka, mlango wa jirani kwenye chumba kingine ukafunguliwa na Josette Lapointe akatoka nje koridoni.
“Shikamoo.”
Josette alitabasamu, “Marhaba. Umependeza kama kawaida yako.”
“Asante.” Kelly alijibu na kubofya kidude kwaajili ya lifti.
Umbali mdogo kidogo kulikuwa na mwanaume mmoja akiwa ndani ya mavazi ya kazi akishughulikia ukuta. Aliwatazama wanawake wale walioingia, halafu akageuza kichwa chake haraka.
“Unaendeleaje na kazi?” Josette aliuliza.
“Naendelea vizuri.” Kelly alijibu.
“Nitakuja kwenye onesho lako hivi karibuni.”
“Nitafurahi sana.”

Lifti ilipofika, Kelly na Josette waliingia ndani. Yule mwanaume aliingiza mkono mfukoni na kutoa kisimu kidogo na kuongea harakaharaka, halafu akaondoka kwa kasi.

Mlango wa lifti ulipoanza kufunga, Kelly alisikia simu inaita kutokea chumbani kwake. Alisita.
Alikuwa na haraka, lakini wenda aliyekuwa anapiga simu ni Mark.

“Tangulia,” Alimwambia Madame Josette.

Halafu akatoka nje ya lifti, akachukua funguo na kukimbia hadi ndani ya chumba chake. Aliikimbilia simu iliyokuwa inaita.
“Mark?”

Sauti ngeni ilisikika masikioni mwake., “Nanette?”
Kelly alighadhabika, “Nous ne connaissons pas la personne qui respond a ce nom.?”

“Pardonnez-moi. C’est une erreur de telephone.”

Amekosea namba. Kelly aliishusha chini kwa nguvu. Wakati ilipofika chini mlio mkubwa uliotetemesha jingo lote ulisikika. Dakika chache baadae kulikuwa na vilio na kelele za ukungu.
Wasiwasi ukiwa umemshika, alikimbia hadi nje kuona nini kimetokea. Sauti zilikuwa zinatokea chini. Kelly alikamata ngazi, na alipofika katikati akaendelea kusikia sauti zinatokea chini. Akaendelea kushuka na alipigwa na butwaa na kubaki amesimama alipouona mwili wa Madame Josette Lapointe ukiwa umesiginwa na lifti ile iliyovurugika. Kelly alijisikia kukosa nguvu... Maskini. Dakika moja iliyopita alikuwa hai na sasa... Na mimi ningelikuwa humuhumu kama sio ile simu.

Kadamnasi ya watu ilikuwa imekusanyika kuizunguka ile lifti, halafu ving’ora vya polisi vikaanza kusikika kwa mbali. Nibakie hapa, Kelly aliwaza. Alihuzunika, lakini ilikuwa ni lazima aondoke.

“Pole sana, Madam.” Alinong’ona na kuondoka.

Wakati anafika kwenye ukumbi wa maonesho, mwandaaji alikuwa mlangoni akimsubiria.

Alianza kubweka, “Kelly! Kelly! Umechelewa! Show imeanza na...”
“Nisamehe,Pierre. Kulikuwa na ajali mbaya sana.”

Alimtazama kwa mshtuko. “Umeumia?”
“Hapana.” Kelly alifumba macho yake kwa muda kidogo. Wazo la kuingia kufanya kazi baada ya tukio aliloshuhudia isingependeza. Lakini hakuwa na chaguo. Yeye ndiye alikuwa nyota wa onesho lenyewe.

“Wahi.” Pierre alisema. “Vite!”

Kelly alianza kutembea kwenda kilipo chumba cha kubadilishia nguo.

Tamasha lenyewe lilikuwa linafanyika Rue Cambon, kwenye jingo la Chanel. Waandishi wa habari walikuwa wamejiweka viti vya mwanza karibu na jukwaa. Kila kiti kilikuwa kimechukuliwa, na nyuma kulikuwa kumejaa watu waliosimama wakisubiria kuona mitindo mipya. Ukumbi wenyewe ulikuwa umepambwa kwa maua na maurembo mengine, lakini hakuna aliyejali sana kuhusu hayo mapambo. Vivutio halisi vilikuwa viko ndani – kama mito ya rangi zinazotembea, uzuri na staili. Kwa nyuma muziki ulikuwa unacheza ukiendana na mwendo uliokuwa ukioneshwa jukwaani.

Kwa kadri wanamitindo walivyoingia na kurudi, walisindikizwa na sauti ya mtangazaji kwenye spika akitoa maelezo ya mitindo yao.

Msichana mwenye asili ya Asia alikuwa anatembea: “Amevaa Jaketi ya sufi, suruali aina ya georgette na blauzi nyeupe...”
Msichana mwingine mwembaba aliingia jukwaani: “... Cashmere nyeusi na suruali nyeupe...”
Akaingia msichana mwingine mwenye swaga: “Mkoti mweusi wa leza na suruali nyeusi na shati nyeupe inayofunga mikanda...”
Mwanamitindo wa Ufaransa: “Jaketi aina ya angora la vifungo vitatu tu, mtandio wa shingo rangi ya pinki na suruali nyeusi...”

Halafu ukafika wakati ambao kila mtu alikuwa akiusubiria. Wanamitindo wote walikuwa wamemaliza ngwe zao na jukwaa lilikuwa tupu. Sauti ilitoka kwenye spika. “Na kwakuwa msimu wa kuogelea umefika, hatuna budi kuonesha mitindo mipya ya mavazi ya ufukweni.”

Kulikuwa na kila aina ya mtindo, halafu Kelly Harris akaibuka kinara. Alikuwa amevaa bikini nyeupe, na sidiria ambayo ni kama hakuwa amevaa chochote ikiyaacha matiti yake yawe kama yapo wazi tu. Kulikuwa na shangwe kubwa.

Kelly aliachia tabasamu la shukrani, akazunguka kurudi na kupotelea mbele ya macho ya mashabiki.

Nyuma ya jukaa, kuna wanaume wawili walikuwa wanamsubiria.
“Mrs. Harris, tunaweza kupata wasaa..?”
“Samahani,” Kelly alisema. “Nahitaji kubadilisha nguo.” Alianza kupiga hatua.
“Subiri! Sisi ni askari. Naitwa Inspector Dune na huyu ni Inspector Steunou. Tuna mazungumzo na wewe.”
Kelly alisimama. “Polisi? Mazungumzo kuhusu nini?”
“Wewe ni mke wa Mark Harris, sio?”
“Ndiye.”
“Basi ninahuzunika kukuambia kuwa mume wako ali – alikufa usiku uliopita.”
Mdomo wa Kelly ukakauka. “Mume wangu? Kivipi?”
“Inavyoonekana ni kama amejiua.”
Alikuwa haelewi nini yule inspekta alikuwa anasema.
“Kwenye mnara wa Eiffel... Usiku... Kibarua... Anajutia... Majonzi.”

Hayo maneno hayakuwa halisia. Bali ni vipande vya sauti tu visivyokuwa na maana yeyote.
“Mmekosea,” Kelly alisema. “Mark hawezi.”
“Ninasikitika sana. Pole.” Inspekta alisema. “Upo sawa?”
“Ndiyo.” Isipokuwa maisha yangu yamefika mwisho.

Pierre alitokea akiwa anakimbia kuja alipo Kelly huku akiwa kashika bikini nyeusi yenye mistarimistari. “Cherie, badilisha haraka. Hatuna muda wa kupoteza.” Aliiweka ile bikini mikononi mwa Kelly. “Vite! Vite!”

Kelly aliiacha ikaanguka chini. “Pieree?”
Pierre alikuwa anamwangalia kwa mshangao, “Oui.”
“Hiyo utavaa wewe.”

Haikuchukua muda Kelly alirudishwa nyumbani akiwa kwenye gari. Meneja wa ukumbi alitaka kumpatia mtu wa kumfariji, lakini Kelly alikataa. Alitaka awe peke yake. Na wakati huu alipokuwa akiingia ukumbini alimuona Philippe Cendre, na mwanaume mwingine aliyevalia ovaroli, wakiwa wamezungukwa na kundi la wapangaji.
Mpangaji mmoja alisema, “Maskini Madame Lapointe kapatwa na ajali mbaya sana.”
Yule mwanaume aliyevalia ovaroli alinyanyua nyaya mbili juu. “Haikuwa ajali, kuna mtu kwa maksudi kabisa alikata breki za lifti.
 
SEHEMU YA SABA.
BLACK LIST
THE SPIRIT THINKER.

7

Saa kumi alfajiri, Kelly alikuwa amekaa kwenye kiti, akiangalia nje ya dirisha, akili yake ikiwa inafanya kazi. Tupo na polisi. Tunahitaji kuongea. Mnara wa Eiffel.. barua.. Mark kafa... Mark kafa... Marka kafa. Yale maneno yalikuwa kama mwangwi unajirudia kwenye akili ya Kelly.

Alianza kuuona mwili wa Mark ukishuka chini, chini, chini... Alikinga mikono ili amdake na tayari Mark alikuwa amejipiga chini. Je, ulikufa kwa sababu yangu? Kuna jambo nilifanya? Au kuna jambo sikufanya? Niliongea neon baya? Au kuna neon sikuwahi kukuambia? Kipindi unatoka nyumbani nilikuwa nimelala na sikupata hata nafasi ya kukuaga, au kukubusu na kukuambia nakupenda kwa kiasi gani. Nakuhitaji sana. Siwezi bila wewe, Kelly aliwaza. Naomba nisaidie Mark, Nisaidie. Aliegemea sofa na kukumbuka siku zilivyokuwa chungu kabla Mark hajaja kwenye maisha yake.

Kelly alikuwa amezaliwa Philadelphia, mtoto wa haramu wa Ethel Hackworth, mwanamke mweusi ambaye ambaye alikuwa anafanya kazi kwenye jumba la familia moja ya kitajiri ya watu weupe. Baba wa ile familia alikuwa ni Jaji. Ethel alikuwa na miaka kumi na saba na alikuwa ni mrembo. Na Pete alikuwa ni kijana wa miaka ishirini. Kijana mkubwa kwenye familia ya Turner, na alikuwa amevutiwa na Ethel. Alimtongoza, na mwezi mmoja baadae Ethel aligundua ana mimba.

Alipomwambia Pete, alisema. “Ni habari njema.” Halafu akakimbia na kwenda kumwambia baba yake habari ile mbaya.

Asubuhi ya siku iliyofuata Jaji Turner alimuita Ethel na kusema, “Siwezi kuruhusu kahaba na Malaya kufanya kazi nyumbani kwangu. Umefukuzwa.”
Bila ya pesa na bila elimu yeyote wala ujuzi wowote, Ethel alikubali kufanya kazi ya kusafisha viwanda, huku akishughulika kwa muda mrefu ili aweze kumlea mtoto wake. Miaka mitano baadae, Ethel alikuwa ametunza akiba ya kutosha kumuwezesha kununua kibanda ambacho kiligeuka nyumba ya wanaume. Ethel aliigawa ile nyumba kuwa sebule, chumba cha kulia, vyumba vya kulala vidogovidogo vinne, na chumba kingine kidogo zaidi ambao ndipo Kelly alilala.

Kuanzia hapo na kuendelea, wanaume walikuwa wanakuja na kuondoka.

“Hawa ni wajomba zako,” Ethel angemwambia. “Usiwasumbue.”

Kelly alifurahi kuona ana familia kubwa kiasi kile hadi siku moja alipokuwa na kugundua wote wale walikuwa ni watu baki tu.
Kelly alipokuwa na miaka nane, alikuwa amelala kwenye chumba chake kidogo chenye giza. Alishtuka baada ya kusikia sauti nzito ikimwambia kwa kunong’ona, “Shhh! Usipige kelele.”

Kelly alihisi gauni yake ya kulalia ikifunuliwa, na kabla ya kukataa chochote, mmoja kati ya ‘wajomba’ zake wengi alikuwa amempandia kwa juu huku kamfunika mdomo. Kelly alisikia akipanuliwa miguu yake kwa nguvu. Alijaribu kujinasua, lakini alizidiwa nguvu. Alihisi uume wa mjomba wake ukilazimisha kumuingia, na akaanza kuhisi maumivu. Lakini mjomba hakuona huruma, alikuwa akilazimisha kuzama zaidi na zaidi, ndani kabisa. Kelly alijihisi damu inamtoka. Alikuwa anapiga kelele isiyotoka akihofia angelikufa au kuzimia. Alikuwa amenaswa katikati ya chumba chake chenye giza.

Hatimaye, baada ya kilichoonekana kuwa milile, alimsikia ‘mjomba’ wake huyo akiguna na kujichomoa.
Alinong’ona “Ninaondoka. Lakini kama utamwambia mama yako hizi habari, nitarudi na kumuua.”
Na ‘mjomba’ aliondoka.

Wiki iliyofuata tangu hilo tukio ilikuwa ngumu. Alikuwa akilia kila muda licha ya kwamba alikuwa amejitibia mwili wake kwa kadri alivyoweza na hatimaye maumivu yakapungua.
Alitamani amwambie mama yake kuhusu lile tukio, lakini hakuthubutu. Lakini kama utamwambia mama yako hizi habari, nitarudi na kumuua.

Ingawa tukio lilikuwa lilitokea ndani ya dakika chache tu, ila lilibadilisha maisha ya Kelly. Alibadilika kutoka kwenye msichana mdogo aliyekuwa na ndoto za kupata mume na watoto hadi kuwa mtu ambaye alijihisi ameonewa na kudhalilishwa. Aliamua hatowahi tena kuruhusu mwanamume amguse tena.

Na kuna jambo jingine pia lilikuwa limebadilika kwa Kelly.

Tangu usiku ule, alianza kuliogopa giza.
 
SEHEMU YA NANE
BLACK LIST
THE SPIRIT THINKER.

8

Kelly alipofikisha umri wa miaka kumi, Ethel alimpa majukumu ya kusaidia. Kelly angeamka saa kumi na moja kila asubuhi kusafijsha vyoo, kudeki jiko na kuandaa kifungua kinywa.
Baada ya shule alifua nguo, kudeki sebule, na kusaidia kuandaa chakula cha mchana. Maisha yake yaligeuka kuwa na ratiba inayochosha.
Alikuwa anajitahidi kumsaidia mama yake akitegemea kupokea neno la pongezi au shukrani. Lakini hakuwahi kulisikia. Mama yake alikuwa bize na wajomba kujali sana kuhusu binti yake.

Kelly akiwa binti mdogo, ‘Mjomba’ mmoja mwenye moyo wa kipekee aliwahi kumsomea kisa cha ‘Alice Adventures in Wonderland,’ na Kelly alifurahishwa sana na sehemu ambapo Alice alitoroka kupitia shimo la sungura la kimuujiza. Hicho ndicho ninachohitaji, Kelly aliwaza, namna nitakavyotoroka. Siwezi kuishi maisha yangu yote nikideki vyoo na sakafu na kusafisha uchafu wa watu ambao hata siwafahamu.

Na siku moja, kweli Kelly alilipata shimo lake la sungura la kimuujiza. Ilikuwa ni uwezo wake wa kufikiria, ambao ungeweza kumpeleka popote anapotaka. Hivyo aliyaandika maisha yake upya.

Alikuwa na baba yake, na mama na baba yake hao wote walikuwa ni weusi. Hawakuwahi kumkaripia. Waliishi kwa amani kwenye nyumba yenye furaha. Baba na mama yake walimpenda. Baba na mama yake walimpenda. Baba na mama yake walimpenda...

Kelly alipofikisha miaka kumi na nne, mama yake aliolewa na mmoja wa wale ‘wajomba’, Mhudumu wa bar moja aitwaye Dan Berke, mwanamume mmoja mchungu ambaye kila kitu kwake kilikuwa ni kibaya. Hakuna jambo ambalo Kelly angefanya likamfurahisha Dan.
“Chakula cha hovyo...”
“Hilo gauni halikupendezei...”
“Kuna kile kidude chumbani kwangu nilikuambia ukirekebishe...”
“Bado tu haujamaliza kusafisha choo...”

Dan alikuwa ni mlevi wa kutupa. Na ukuta uliotenganisha chumba cha Kelly na kile cha mama na baba yake huyo wa kambo, Dan, ulikuwa ni mwembamba, na kila usiku baada ya usiku, Kelly angesikia sauti ya kipigo na vilio. Na asubuhi mama yake angeamka akiwa na make up nyingi usoni ambayo hata hivyo ilishindwa kuficha uvimbe wa kipigo.

Kelly angehuzunika. Inatakiwa tuondoke hapa, angejisemea.

Usiku mmoja, Kelly akiwa amelala, alisikia sauti kutokea chumba cha pili. “Kwanini haukutoa mimba kabla huyu mtoto hajazaliwa?”
“Nilijaribu, Dani. Lakini sikufanikiwa.”
Kelly alijihisi kama amepigwa ngumi nzito ya tumbo. Kumbe mama yake hakuwahi kumtaka. Kumbe hakuna mtu yeyote aliyewahi kumtaka!

Lakini Kelly alipata njia nyingine ya kutoroka uhalisia wa maisha yake: Aligeukia kuwa mpenzi wa vitabu. Alitumia muda mwingi maktaba akisoma hiki na kile kwenye maktaba.

Kwa bahati mbaya hakuwa na pesa ya kuendelea kulipia huduma ikabidi atafute kazi ya u-Yaya, kulea watoto siku za mwisho wa wiki. Mara nyingi aliishia kushikwa wivu alipoyaona maisha ya familia zenye furaha.

Muda ulisonga na Kelly alifikisha miaka kumi na saba. Tayari muonekano na uzuri wa mama yake alipokuwa umri huo vilikuwa vimehamia kwake. Wavulana shuleni kwake walianza kumtokea. Na wote aliwakatalia.

Jumamosi, akiwa haendi shuleni angeenda maktaba na kutumia muda mwingi kujisomea.

Lisa Marie Houston, msimamizi wa maktaba, alikuwa ni mwanamke mwenye akili na huruma. Kumuona Kelly mara kwa mara maktaba kuliibua maswali kichwani kwake.

Siku moja alifungua maongezi, “Ni vizuri sana kuona kijana anafurahia kusoma sana kiasi hiki. Unatumia muda mwingi sana hapa.”

Ilikuwa ni karata ya kutengeneza urafiki. Na kadri wiki zilivyoenda Kelly alifunguka hofu zake, ndoto zake na kila kitu chake kwa yule msimamizi wa maktaba.

“Unatamani ufanye jambo gani kwenye maisha yako?”
“Natamani niwe mwalimu.”
“Nadhani utakuwa mwalimu mzuri sana. Ni kazi nzuri kuliko zote duniani.”

Kelly alianza kuongea, halafu akatulia. Alikuwa anakumbuka maongezi fulani aliyoyafanya na baba yake asubuhi moja ya wiki iliyopita. Kelly alikuwa amesema, Nahitaji kujiunga na chuo. Nataka kuwa mwalimu.

Mwalimu? Berke aliangua kicheko. Hilo ni wazo la kipuuzi sana.
Sanasana labda ufagie na kudeki tu choo. Hata hivyo, mimi na mama yako hatuna hela ya kukupeleka chuo.

Ila nimeambiwa nitasomeshwa na...
Kwahivyo? Utapoteza miaka minne bure. Kwa muonekano wako? Bore ujitembeze tu.

Kelly alinyanyuka na kuondoka mezani.

Baada ya kumbukumbu hiyo, Kelly aligeuka kumwambia Mrs. Houston. “Kuna tatizo moja. Wazazi wangu hawatoniruhusu kujiunga elimu ya juu. Nitaendelea kufanya ninachofanya mpaka nitakapokufa.”
“Una miaka mingapi?” Houston aliuliza.
“Ndani ya miezi mitatu nitakuwa na miaka kumi na nane.”
“Muda si mrefu utakuwa huru kikatiba kufanya maamuzi yako mwenyewe. Wewe ni msichana mrembo sana, Kelly. Unalifahamu hilo.”
“Hapana.” Kelly aliongea na kuongeza, “Ninayachukia maisha yangu. Ninatamani niondoke kwenye huu mji,” Alikuwa anajitahidi sana kuzizuia hisia zake.”Sitawahi kupata nafasi ya kufanya jambo lolote ninalotaka.”
“Kelly..”
“Ningejua nisingewahi kusoma hivyo vitabu.” Sauti yake ilikuwa imejaa uchungu.
“Kwa sababu vimejaa uongo mtupu. Hizo sehemu zote nzuri zinazotajwa na miujiza...” Kelly alitikisa kichwa. “Hakuna miujiza.”

Mrs. Houston alimtazama kwa muda. Ni wazi Kelly alikuwa amepoteza uwezo wa kuiona thamani yake. “Kelly, miujiza ipo. Ila kwanza unatakiwa kuwa mwanamiujiza. Wewe ndiye anatakiwa ufanye miujiza.”
“Kweli?” Sauti ya Kelly ilitoka. “Nitawezaje?”
“Kwanza, unatakiwa kujua ndoto zako. Wewe ndoto zako ni kuwa na maisha yenye kufurahisha na uwe sehemu nzurinzuri. Wakati mwingine utakapokuja nitakuonesha jinsi ya kufanikisha ndoto zako.”
Muongo.

Wiki moja baada ya Kelly kuhitimu, alirudi tena maktaba. Mrs. Houston alianza kuongea, “Kelly, unakumbuka mara ya mwisho nilikuambia jinsi ya kutengeneza miujiza yako.”
Kelly alisema kwa kusita, “Ndiyo.”
Mrs. Houston aliingiza mkono kwenye droo yake na kutoa rundo la magazeti: COSMOgirl, Seventeen, Glamour, Mademoiselle, Essence, Allure. Youte alimpatia Kelly.
Kelly aliyatazama. “Niyafanyie nini haya?”
“Umewahi kufikiria kuwa mwanamitindo”
“Hapana.”
“Yapitie hayo magazeti halafu unambie kama yanakupa mawazo ya muujiza unaoweza kubadilisha maisha yako.”
“Asante, Mrs. Houston, Nitafanya hivyo.”
Itabidi nianze kutafuta kazi, Kelly alijiwazia. Na aliporudi nyumbani aliyaweka yale magazeti kwenye kona ya kitanda chake na kuyasahau. Alitumia muda mwingi wa jioni yake kufanya shughuli za nyumbani.
Usiku alipokuwa akipanda kitandani kulala, Kelly aliyakumbuka yale magazeti. Alichukua machache na kuanza kupitia moja moja. Ulikuwa ni ulimwengu mwingine. Wanamitindo walikuwa wamevaa nguo za kuvutia, wanaume kwa wanawake wazuri. Walikuwa London, Paris na karibu sehemu zote nzuri duniani. Kelly alihisi uhitaji fulani. Alivaa gauni lake fulani na kutembea kwa mwendo wa cat walk kuelekea bafuni.
Alijitazama kwenye kioo. Alihisi pengine ana mvuto. Karibu kila mtu alikuwa amemuambia hivyo, lakini hata kama ni kweli hakuwa na uzoefu wowote. Aliyafikiria maisha yake ya Philadeliphia na kujitazama kwenye kioo tena. Kila mtu lazima aanzie mahali fulani.... Inatakiwa kuwa mwanamiujiza. Na uufanye muujiza utokee.

Asubuhi iliyofuata, Kelly alifika maktaba kumuona Mrs. Houston.

Mrs. Houston aliangalia juu, akiwa na mshtuko kumuona Kelly asubuhi na mapema kiasi kile. “Kelly, ulipata nafasi ya kupitia yale magazeti?”
“Ndiyo.” Kelly alivuta pumzi ndefu. “Ningependa kujaribu kuwa mwanamitindo, lakini tatizo ni kwamba sijui wapi pa kuanzia.”
“Ninafahamu uanzie wapi. Nimeangalia orodha ya taasisi kubwa za wanamitindo New York na ninayo orodha na namba zao za simu.” Mrs. Houston alisema huku akimpa Kelly kikaratasi.

“Hiyo karatasi ina orodha ya taasisi za wanamitindo na namba zao. Anzia hizo za juu.”
Kelly alistuka, “Sijui niseme vipi asante yangu.”
“Usiniambie asante kwa maneno. Ila hakikisha siku moja naiona picha yako kwenye moja ya haya magazeti.”

Ilipofika jioni wakati wa chakula, Kelly alisema, “Nimeamua nitakuwa mwanamitindo.”
Baba yake, Dan, aling’aka. “Hilo ndilo unaona wazo zuri. Una matatizo gani? Wanamitindo wote ni malaya tu.”

Mama yake aliguna pia, “Kelly, usifanye kosa nililofanya. Mimi pia nilikuwa na ndoto kama zako. Kumbuka wewe ni mweusi na ni maskini. Hauendi popote.”

Na huo ndio muda ambao Kelly alifanya maamuzi yake. Asubuhi ya kesho yake saa kumi na moja alfajiri, Kelly alibeba kibegi chake kidogo cha nguo na kuelekea stendi ya mabasi. Kwenye mkoba wake alikuwa na dola mia mbili tu ambazo alizikusanya kwenye kazi yake ya kulelea watoto.

Safari ya basi hadi Manhattan ilichukua masaa mawili, na muda wote Kelly alikuwa anafikiria maisha yake yajayo.
Alikuwa anaenda kuwa maarufu na mwanamitindo mashuhuri. Na jina Kelly Hackworth halikuonekana kama linafaa.
Ninajua nitakachokifanya. Nitatumia jina langu la kwanza tu. Alijiambia akilini mara kwa mara. Na huyu ni mwanamitindo wetu, Kelly.

Basi lilipofika alichukua chumba kwenye nyumba ya wageni ya bei rahisi na saa tatu asubuhi alikuwa yupo mlangoni mwa taasisi moja ya wanamitindo iliyokuwa juu ya orodha kwenye karatasi aliyokuwa amepewa na Mrs. Houston. Hakuwa na make up wala nguo nzuri.

Hakukuwa na mtu yeyote kwenye meza ya mapokezi. Alipita na kuingia hadi ofisi moja ambako alikutana na mwanamume mmoja akiandika kitu.
“Samahani,” Kelly alisema.
Yule mwanaume aliguna bila kuinua macho.
Kelly alisita, “Nilikuwa nauliza kama mnahitaji mwanamitindo.”
“Hapana. Hatuna nafasi.”
Kelly aliguna. “Asante.” Aligeuka na kuanza kuondoka.

Yule mwanaume aliinua uso wake na sura yake ikabadilika. “Subiri. Subiria dakika moja. Rudi mara moja.” Alisema huku akisimama.
“Mungu wangu. Umetokea wapi?”
“Philadelphia.”
“Namaanisha ulikuwa mwanamitindo wapi kabla?”
“Sijawahi.”
“Haijalishi. Utajifunzia hapahapa.”
Kelly alistuka, “Unamaanisha nitakuwa mwanamitindo?”
“Labda niseme tuna wateja ambao wakikuona watafurahi sana.”
Kelly hakuamini. Hii ilikuwa ni moja kati ya taasisi kubwa na walikuwa wanampa...
“Mimi naitwa Bill Lerner. Ndiye mkurugenzi hapa. Jina lako ni nani?”

Huu ndio wakati ambao Kelly alikuwa akiutazamia. Huu ndiyo wakati ambao angetumia jina lake jipya. Lerner alikuwa anamtazama. “Haulifahamu jina lako?”

Kelly alijinyoosha na kuongea kwa kujiamini, “Nalifahamu. Kelly Hackworth.”
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom