Msaada: TRA wanaruhusiwa na Sheria ipi kuchukua Mali za Mtu?

Kng barn

Member
Jul 14, 2019
9
12
Wadau habari, mimi nataka kuuliza.

Ikiwa ulikua ni mfanya biashara wakati na ulikua unalipa kodi vizuri tu TRA bahati mbaya biashara zikaenda mlama ukafilisika ukawa na deni kubwa TRA licha ya kuandika barua za kujitetea na kupewa mikataba mingi jinsi ya kulipa deni lakini ikawa umekwama bado unadaiwa labda mil 50 na huna unalazimishwa ulipe deni hilo kwa awamu 4 maana 12.4milion lakin bado huwezi.

Je, TRA wanarusiwa kwa sheria ipi kuchukua mali za mfanyabiashara huyo maana wananiambia watachukua mali zangu na kuna kipindi walifunga gari yangu mnyororo lakini baada ya kuwasemelea kwa wakubwa wakafungua mnyororo sahivi wanantishia tena.
 
Habari mkuu,
Ni sheria ya Usimamizi wa kodi sura namba 438 kifufungu namba 61 kinampa mamlaka kamishna mkuu kuzuia mali za mdaiwa wa kodi, Na kifungu cha 62 kimemruhusu kamishna mkuu kuuza mali hizo.
 
Ongea na meneja wa huo mkoa ikishindikana nenda kwa kamishina wa walipa kodi za ndani kama nadhani atakupa barua ambayo itaonyesha umefirisika ikitoka kwa kamishina Mkuu,kama unafanya biashara utakubaliana kiwango ambacho unaweza kulipa hao wahuni wadogo wadogo wanataka rushwa na ndio hao wanafanya uwekewe kiwango ambacho hauwezi kukilipa ili uonekane Mkaidi wapitishe barua haraka haraka wachukue mali zako ni mlolongo sana mpaka ikifikia hivyo...harafu usiogope ofisi za TRA nenda makao makuu waeleze shida yako wapo wanodaiwa Mabilioni na wanapeta wakianza biashara wanaaza kulipa usiwasikilize wachimba chumvi watakutisha kwa vitu ambavyo havipo...
 
ooh shukran kwa ushauri mzuri
 
ooh shukran kwa ushauri mzuri
Kamishina wa TRA ndio mwenye madaraka ya mali ya mtu ipigwe mnada sio hao vijana wanaotaka rushwa kwako na wengine ikifika hatua hiyo wanaenda Mahakamani harafu kisheria unaruhusiwa mpaka kesi iishe ndio mambo ya kodi yaendelee unakumbuka mpaka mzee Magu wahuni walimchezea ishu ya mahakamani mpaka akawa anaomba kesi za Wafanyabiashara ziishe mapema...
 
Habari mkuu,
Ni sheria ya Usimamizi wa kodi sura namba 438 kifufungu namba 61 kinampa mamlaka kamishna mkuu kuzuia mali za mdaiwa wa kodi, Na kifungu cha 62 kimemruhusu kamishna mkuu kuuza mali hizo.
Sasa Mtu Kesha filisika si waachane nae tu,au huo mtaji alipewa na TRA!!??

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Habari mkuu,
Ni sheria ya Usimamizi wa kodi sura namba 438 kifufungu namba 61 kinampa mamlaka kamishna mkuu kuzuia mali za mdaiwa wa kodi, Na kifungu cha 62 kimemruhusu kamishna mkuu kuuza mali hizo.

Halafu bado kuna mtu anahoji kwann Africa ni maskini?
Unamuuzia mtu mali yake, unaenda kununulia V8 ya wazir
 
Ukishaanza kutoa virushwa vya m2-3 kwa hawa wadogo matatizo huanzia hapo. Hawatakuacha. Usitoe Rushwa. Watatuliza ikipita miez kadhaa linaibuka tena. Bora hiyo Rushwa uilipe serikalini kuonyesha unajaribu kadri uwezavyo.

Nenda straight juu kabisa jaribu kusolve suala lako, hakikisha lipo viral ndani ya hizo ofisi kiasi kwamba kila afisa wa chini alione file lako halina maslahi.
 
Back
Top Bottom