Msaada... Tofauti Ya Vipimo Vya Malaria

bryan2

JF-Expert Member
Jun 8, 2016
3,321
4,671
HALLO!Wanajukwaaa Msaada juu ya hili.Kuna uwezekano wa Majibu ya Malaria Rapid Diagnostic Test (MRDT) na Blood Slide for Malaria(BS) Nazungumzia kwa Darubini Yakawa Tofauti.?

Mfano ukapima Mrdt ikawa Negative then BS ikaonyesha Malaria Parasites Seen???

Karibuni Kwa michango.
 
Yeah, MRDT ni vipimo ambavyo sivipendi hata kuviona machoni pangu, ni sawa sometimes vinaonyesha positive, lakini B/s ndio njia ambayo naiamini 1000000%

Ubovu wa MRDT ni pale tu inapoonyesha negative wakati kiuhalisia huyo mtu anamalaria, na hii inatokana na kiasi cha antibodies kuwa kidogo mnooo baada ya huyo mtu kuwa na malaria, hali ambayo inafanya hicho kipimo kisiweze kudetect hizo antibodies, hadi tu pale antibodies zinakapokuwa kiasi fulani ndipo MRDT inaweza ikasoma positive lakini ikiwa ni weak-positive
 
Hoo kwa hiyo is like Determine kwa Hiv mpaka zile Window period 3 months zipite ndo iweze kusoma Reactive Siyo.

Point ni kwamba anaweza kuja mgonjwa anadalili zote za malaria ila ukipima kwa Mrdt Negative na hapo vipimo vingine vyote vinasoma Nad kama vile UA,Stool,Widal test even Brucella test.
 
Yeah, MRDT ni vipimo ambavyo sivipendi hata kuviona machoni pangu, ni sawa sometimes vinaonyesha positive, lakini B/s ndio njia ambayo naiamini 1000000%

Ubovu wa MRDT ni pale tu inapoonyesha negative wakati kiuhalisia huyo mtu anamalaria, na hii inatokana na kiasi cha antibodies kuwa kidogo mnooo baada ya huyo mtu kuwa na malaria, hali ambayo inafanya hicho kipimo kisiweze kudetect hizo antibodies, hadi tu pale antibodies zinakapokuwa kiasi fulani ndipo MRDT inaweza ikasoma positive lakini ikiwa ni weak-positive
Nje mada: Mtu anaweza kuwa na parasite ila asiwe amekuwa mgonjwa.
Malaria kama ugonjwa mtu inabidi awe na homa na dalili zingine then awe aonekane ana wadudu.

Labda matatizo ya vitendea kazi lakini kwa ukweli asilimia kubwa majibu ya mrdt yaendane na bs.
 
Hapo kwenye Parasites Mrdt haina uwezo wa kuonyesha idadi ya Parasites yenyewe itasoma positive au Negative.

Na kuhusu mtu kuwa na parasites ila hakuna ugonjwa nafikiri ni vizuri kupitia Incubation period ya Malaria parasites na pia lifecycle
 
Nami naombeni kuuliza Mimi nikitumia dawa sp kutibu malaria natokwa na vidonda mno puani usoni mdomoni maumivu makali nikitumia hii mseto ndiyo basi iliwahi nitia ukiziwi mwaka mzima. Sasa nauliza nisaidiwe ni dawa ipi inafaa kutibu malaria bila kuleta alerge kwa mgonjwa ili niitumie hiyo.
 
Blood slide ndio golden standard ya kupima malaria parasite na ndio maana hata mrdt ikiwa positive lazima urudi kwenye b/s ku prove na kucount,kwanini mrdt wengi wanazilalamikia katika malaria parasite counting tuna high parasitemia, medium parasitemia na low parasitemia mara nyingi mrdt ina fail kwenye mtu mwenye low parasitemia yani less than 10 malaria parasites na pia kufail kwengine kwa mrdt itategemea na bland na jinsi ilivyohifadhiwa,japo pia unaweza kuwa na dalili zote za malaria parasite lakini isionekane kwenye njia zote mbili,hii itatupa picha kwamba huwenda malaria parasites unao ila wapo kwenye ini wanapoanzia mzunguko wake bado hawajaingia kwenye blood stream tukaweza kuwaona kwa njia zetu hizi mbili yaani mrdt na b/s.
 
Mrdt ni kipimo cha biashara tuu lkn c cha maralia,ni kheri utumie b/s kuliko hiyo coz hata maralia parasite wakiwa chin ya 50 haiwezi kuditect,yaan c kipimo kabisa
 
Back
Top Bottom