Fahamu kuhusu Kipimo cha Malaria maabara BS/MRDT

Bonge La Afya

Member
Dec 19, 2016
31
71
BS/MRDT: Umefika hospitali daktari kakusikiliza kisha kwenye fomu yako kaandika ukapime BS/MRDT unashindwa kuelewa ila kwa sababu unaumwa unaenda kupima. Hii BS/MRDT ni nini? Leo acha nikujuze.

MRDT ni kifupi cha Malaria Rapid Diagnostic Test (kipimo cha haraka cha ugunduzi wa vimelea viambukizavyo Malaria). Kipimo hiki kinausisha utambuzi wa antibodies za Malaria (kinga za mwili zinazotengenezwa baada ya kuugua).

Mwili huchukua mpaka siku saba ndipo hutengeneza kinga (antibodies) ambazo ndio hutambuliwa na kipimo hiki cha MRDT. Hivyo ukienda hospitali kabla kinga hizi hazijatengenezwa utapima na kuonekana huna Malaria.

Lakini pia, kipimo hiki kwa watu ambao wametumia dawa kipindi cha wiki mbili nyuma huendelea kuonekana wana Malaria kupitia kipimo hiki kwani kinga huendelea kukaa kwenye mzunguko kuhakikisha hakuna mdudu mwingine atakayekudhuru.

BS ni Blood slide/Smear hiki ndio kipimo gold standard kwa upande wa malaria, kinahusisha uchakataji wa seli nyekundu za damu kuangalia kama ndani yake kuna vimelea vya malaria kwani mdudu anapoingia mwilini hukaa ndani ya seli nyekundu ambako huzaliana zaidi.

Ni kipimo kinachochukua kuanzia dakika 30 mpaka 40, Daktari huomba kipimo hiki kama confirmatory test pale anapohisi mgonjwa ana malaria. Kwa wagonjwa wa haraka huomba MRDT kwani huchukua muda mfupi.

Hospitali nyingi hupendelea BS kwani gharama zake za uendeshaji upande wa maabara ni nafuu japo kuna wataalamu kutokana na kukosa ujuzi huaibisha taaluma kwa kushindwa kufanya kipimo hiki na kuishia kusema mtu ana malaria.

Tuwasikilize madaktari wetu, kutokana na historia yako wao hujua ni kipimo gani kinakufaa. Usiende maabara ukiwa na majibu yako kichwani subiri vipimo kwani sio kila homa ni Malaria.

images%20(35).jpeg
images%20(36).jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sawa mtaalam ila kumbuka sio reagent zote zinachukua 30-40 minutes mfano field stain mkuu. pia hata giemsa dilution ndio itakuongoza utumie dakika ngapi? maana hotplate ipo ko kukausha sio ishu ukiwa na field stain ndani ya dakika 7 usha soma majibu
 
Back
Top Bottom