Bila shaka hiyo simu ni Tecno, maana hili tatizo huwa linazikumba sana simu za Tecno. Sababu ya hilo tatizo silijui ila fuata njia hizi kutatua;
-Nenda kwenye Settings za simu yako
-Nenda kwenye Apps
Hapa utaweza ku-manage applications za simu yako
-Chagua option ya Show system
Hapa utaruhusu kuona System apps, yaani zile built-in apps
-Shuka chini kutafuta Media Storage
Zikionekana system apps tafuta iliyoandikwa Media Storage halafu ifungue
-Clear Data za Media Storage
Hapa utafuta taarifa zote zilizohifadhiwa na Media Storage zinazohusiana na Picha, Video n.k. Usihofu hautapoteza data zako.
-Clear Data za Gallery/My Pictures
Hatua hii utafuta data za kwenye gallery itategemea kwenye simu yako gallery imepewa jina gani, futa hizo data hii pia haina madhara kwenye ma-file yako
-Restart simu yako
Hatua ya mwisho restart simu yako mpaka hapo ni 100% tatizo lako litakuwa limeisha bila kupoteza ma-file yako.
Nipo hapa kwa msaada zaidi...