Msaada: Tatizo la picha kujirudia rudia (Multple photos) katika simu

Biisa

JF-Expert Member
Jan 13, 2019
426
500
Habari waungwana, kuna changamoto ya kujirudia rudia kwa picha na ma file mengine katika simu hasa "Audio" na "Video".

Msaada :
1. Naomba kujuzwa ni kitu husababisha kujirudia rudia (Multiple) kwa mafile katika simu, yaani audio zinakuwa mbili mbili, au folder za mapicha zinakuwa mbili mbili.

2. Nawezaje kuondoa tatizo hilo, maana iliwahi kutokea siku za nyuma, nikajaribu kufuta folder moja, ila kilichotokea lile folder lingine nalo likawa lipo tu, ila uki select picha uione unakuwa huoini tena na katika audio files nako ndiyo hivyo hivyo, yaani ukifuta audio moja ni sawa unefutwa zote, yaani hiyo iliyo baki inakuwa hai "play".

Natanguliza shukrani.
 
Forgotten

JF-Expert Member
Jul 20, 2018
658
1,000
Bila shaka hiyo simu ni Tecno, maana hili tatizo huwa linazikumba sana simu za Tecno. Sababu ya hilo tatizo silijui ila fuata njia hizi kutatua;

-Nenda kwenye Settings za simu yako

-Nenda kwenye Apps
Hapa utaweza ku-manage applications za simu yako

-Chagua option ya Show system
Hapa utaruhusu kuona System apps, yaani zile built-in apps

-Shuka chini kutafuta Media Storage
Zikionekana system apps tafuta iliyoandikwa Media Storage halafu ifungue

-Clear Data za Media Storage
Hapa utafuta taarifa zote zilizohifadhiwa na Media Storage zinazohusiana na Picha, Video n.k. Usihofu hautapoteza data zako.

-Clear Data za Gallery/My Pictures
Hatua hii utafuta data za kwenye gallery itategemea kwenye simu yako gallery imepewa jina gani, futa hizo data hii pia haina madhara kwenye ma-file yako

-Restart simu yako
Hatua ya mwisho restart simu yako mpaka hapo ni 100% tatizo lako litakuwa limeisha bila kupoteza ma-file yako.

Nipo hapa kwa msaada zaidi...
 
Shukrani sana kaka, simu ni tecno kwelu kama ulivyo sema.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom