Msaada tatizo la maumivu ya vidole vya mkono hadi kushindwa kuandika.

Nkondo 2

Senior Member
Oct 10, 2016
163
127
Ndgu wana jukwaa, mdogo wangu wa kike ambaye yupo kidato cha sita kwa sasa amekumbwa na tatizo la maumivu makali ya vidole vya mikono hali inayopelekea kushindwa kuandika vzr ktk masomo yake nahivyo kushusha maendeleo yake kitaaluma kwan ktk kujibu mitihan yake hawez kumaliza kujibu maswali yote kutokana na maumivu hayo yanayosababisha speed ya uandishi iwe ndogo sana.

Ugonjwa huu umemuanza takriban miez nane iliyopita, hatua tuliyochukua n kumpeleka hospital ya Bugando, ambapo baada ya vipimo vya mifupa ilionekana hana tatzo lolote, hivyo docta alitueleza huenda tatzo lipo ktk mfumo wa neva, na akatupatia dawa za kutumia kwa matazamio(Valparin chrono 500, pamoja na Neurobian forte).

Mwisho, Tunaomba msaada wa tiba na ushaur kwa yeyote mwenye uzoefu na hali kama hiyo kwan hali inazidi kuwa mbaya pamoja na matibabu hayo aliyopewa hosipital.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom