Msaada, Tatizo la low voltage

Msaada, Tatizo la low voltage

Kyenju

JF-Expert Member
Joined
Jun 16, 2012
Posts
5,143
Reaction score
2,547
Habari Wanabodi!

Niende moja kwa moja kwenye mada.
Kama wiki tatu zilizopita niliunganishiwa umeme na TANESCO, ila kumekuwa na tatizo la low voltage hasa kuanzia saa moja usiku hadi saa tano au sita usiku ndiyo unalejea kwenye voltage ya kawaida.
Nyumba ilikuwa na wire ring imekaa muda mrefu bila kutumika.

Amekuja fundi kurekebisha ila bado hajafanikiwa.

Karibu wadau.
 
Shida inaweza kuwa sio hapo kwenye nyumba yako ila TANESCO, tumewai pitia hii shida kipindi cha nyuma huko nyuma sana nikiwa bado O-level nafikiri na ilikuja isha yenyewe, cha msingi uliza majirani zako wakwambie wao vipi.
 
Majirani umeme unawaka vizuri kabisa.
 
Majirani umeme unawaka vizuri kabisa.
Basi achana na Fundi wako huyo aweza kua fundi maiko piga namba yao ya dharula, sijui ulipo ila hapa mtaani kwetu within 1-2 days huwa wanafika, wao itakua rahisi zaidi kujua shida ikowapi.
Au piga hii namba bure 118 waeleze uskie.
 
Habari Wanabodi!

Niende moja kwa moja kwenye mada.
Kama wiki tatu zilizopita niliunganishiwa umeme na TANESCO, ila kumekuwa na tatizo la low voltage hasa kuanzia saa moja usiku hadi saa tano au sita usiku ndiyo unalejea kwenye voltage ya kawaida.
Nyumba ilikuwa na wire ring imekaa muda mrefu bila kutumika.

Amekuja fundi kurekebisha ila bado hajafanikiwa.

Karibu wadau.
Hili ni janga! Binafsi nilifungiwa mita miaka miwili iliyopita na kila jioni ikifika umeme unakatika. Nimepiga simu Tanesco mpaka nimechoka, wanakuja mafundi wakitoka tu, umeme unakatika wakati nyumba za jirani zina umeme - mpaka AIBU. Siku moja mtu wa huduma kwa wateja alinipa namba nyingi za kuingiza kwenye remote, lakini tatizo linaendelea, nilikasirika nikawambia waje waondoe mita yao nitafute solar. Ni shida! Ukipata suluhu tushirikishe
 
Pole hiki kisanga kimewai tukuta kanisani, tuli hustle hatari ni kama sijui hua na wao hawajui shida ilipo au vipi. Umeme ukikata utarudi kwa wengine kwanza then baada ya masaa ma4 ndo urudi kanisani ilikua balaa hasa ikitokea siku ya ibada.
 
Hili tatzo liliwah kutokea nyumban kwetu,tulikuwa tunawapigia simu kama wasukuma wanapokosea namba,yaan kila mtu alikuwa anawapigia simu pale nyumban,lakin tatzo ilikuwa ni transformer ya pale mtaan,walihangaika kubadilisha hatimae tatzo likaisha
 
Okay! Ila hapa kwetu majirani umeme unawaka vizuri, kwa maana kwamba hii siyo issue ya transfoma.
 
Habari Wanabodi!

Niende moja kwa moja kwenye mada.
Kama wiki tatu zilizopita niliunganishiwa umeme na TANESCO, ila kumekuwa na tatizo la low voltage hasa kuanzia saa moja usiku hadi saa tano au sita usiku ndiyo unalejea kwenye voltage ya kawaida.
Nyumba ilikuwa na wire ring imekaa muda mrefu bila kutumika.

Amekuja fundi kurekebisha ila bado hajafanikiwa.

Karibu wadau.
Nikadhani....dah.
 
Hapo ni meter mkuu, umeme ukiwa mdogo meter hairuhusu umeme kuingia, nina tatizo kama hlo jambo huwa halichukui zaid ya dk mbili umeme ukikatika na kurudih,

eneo ulipo kuna shida ya umeme kuwa mdogo, na meter yako ni ya kisasa hairuhusu umeme kuingia kama ni low voltage, inakukinga na uharibifu wa vitu vyako vinavotumia umeme japo kwako ni kero, hao jirani zako ambao wana umeme muda wote meter zao ni zile za kizamani hata kukiwa na low voltage yenyewe yanapuyanga tu.

tanesco hawawezi kukuambia ukwel kwa sababu wanaujua, mafundi wa kitaa wengi hawajui kuwa hapo ni meter inakataa kuruhusu umeme mdogo kuingia, wale wanaojua hawakuambia kwa sababu ukiwaita wanapata chochote.

labda ukutane na mtu mwema tanesco akufanyiwe mpango wa yale mameter ya zamani la sivo ni kisanga maana eneo ulipo liko na shida ya low voltage.
 
Sijasoma advance Mkuu, ndiyo maana nikalileta tatizo kwako uliyesoma unisaidie.
Tumia kanuni ya V=IR yaan
V ni voltage
I ni carrent
R ni Resistance
Hapo sasa chukua R zidisha na I hapo voltage utapata ya kutosha sana mkuu
 
Hapo ni meter mkuu, umeme ukiwa mdogo meter hairuhusu umeme kuingia, nina tatizo kama hlo jambo huwa halichukui zaid ya dk mbili umeme ukikatika na kurudih,

eneo ulipo kuna shida ya umeme kuwa mdogo, na meter yako ni ya kisasa hairuhusu umeme kuingia kama ni low voltage, inakukinga na uharibifu wa vitu vyako vinavotumia umeme japo kwako ni kero, hao jirani zako ambao wana umeme muda wote meter zao ni zile za kizamani hata kukiwa na low voltage yenyewe yanapuyanga tu.

tanesco hawawezi kukuambia ukwel kwa sababu wanaujua, mafundi wa kitaa wengi hawajui kuwa hapo ni meter inakataa kuruhusu umeme mdogo kuingia, wale wanaojua hawakuambia kwa sababu ukiwaita wanapata chochote.

labda ukutane na mtu mwema tanesco akufanyiwe mpango wa yale mameter ya zamani la sivo ni kisanga maana eneo ulipo liko na shida ya low voltage.
Eleza kitalam toa na equation mkuu
 
Okay! Ila hapa kwetu majirani umeme unawaka vizuri, kwa maana kwamba hii siyo issue ya transfoma.
Hata sis ilikuwa hvyo hvyo,yaan mtaa wenye nyumba kama ishirin lakin ya kwetu inakuwa na umeme mchana ikifika jion unakata unarud saa 6 usiku

Na sio kwamba majiran tulikuwa nao mbali sana la hasha,yaan jiran yupo mita tano 5 lakin umeme kwake upo sawa
 
Hapo ni meter mkuu, umeme ukiwa mdogo meter hairuhusu umeme kuingia, nina tatizo kama hlo jambo huwa halichukui zaid ya dk mbili umeme ukikatika na kurudih,

eneo ulipo kuna shida ya umeme kuwa mdogo, na meter yako ni ya kisasa hairuhusu umeme kuingia kama ni low voltage, inakukinga na uharibifu wa vitu vyako vinavotumia umeme japo kwako ni kero, hao jirani zako ambao wana umeme muda wote meter zao ni zile za kizamani hata kukiwa na low voltage yenyewe yanapuyanga tu.

tanesco hawawezi kukuambia ukwel kwa sababu wanaujua, mafundi wa kitaa wengi hawajui kuwa hapo ni meter inakataa kuruhusu umeme mdogo kuingia, wale wanaojua hawakuambia kwa sababu ukiwaita wanapata chochote.

labda ukutane na mtu mwema tanesco akufanyiwe mpango wa yale mameter ya zamani la sivo ni kisanga maana eneo ulipo liko na shida ya low voltage.
Shukurani kwa mchango wako Mkuu, ila siyo kwamba meter inakata umeme kabisa, hapana unaingia ila taa zinawaka dim, huwezi kuona bila kutumia nishati mbadala.
 
Back
Top Bottom