Msaada tafadhari

ziloi

JF-Expert Member
Apr 15, 2018
758
1,063
Mtoto kabadili password kwenye simu yangu sumsang s8 plan

Naomba msaada jinsi ya ku unlock bila kufuta taarifa zangu zozote yaani bila ku restart simu sababu ni za mhimu sana

Nakumbuka Email address na password yake tu.
 
Yani mtoto akabadili passwords maana yake alikumbuka password zako kisha akajaza za kwake tena kwa kuzirudia marambili kwa usahihi halafu baada ya hapo akazisahau

😂😂😂😂😂😂 lipo jambo hapa
 
Yani mtoto akabadili passwords maana yake alikumbuka password zako kisha akajaza za kwake tena kwa kuzirudia marambili kwa usahihi halafu baada ya hapo akazisahau

lipo jambo hapa
Mwenyewe sielew kawezaje japo si mtoto sana kama unavyodhania almost standard six. Na anajua kutumia simu tena zaid yangu
 
Kama umemgombeza umeharibu, muache atulie ongea nae vizuri akumbuke aliyoweka. Tulia kubali ni mjanja zaidi yako, na atakusaidia. Kelele zingine zinaogopesha watoto na kuwanyima kuwa wao.
 
Yah kweli mkuu, yaani hapa ingekuwa haina mambo yangu ningeweza ku restart kwa njia zetu zile za kufoji ila sasa duh!
 
Vipi kichapo umeshamtembezea kwanza akili imkae sawa au umekuja kuuliza kwanza?

Huyo atakuwa anaelewa alichofanya mbaya zaidi ana uelewa na simu kuliko wewe hapo ndio tatizo lilipo
 
Hahaha mie kuchapa siyo rahisi kihivyo. Sema kwa jinsi nilivyobadilika kashapotea mazingira yangu muda tu
 
Mtoto kabadili password kwenye simu yangu sumsang s8 plan

Naomba msaada jinsi ya ku unlock bila kufuta taarifa zangu zozote yaani bila ku restart simu sababu ni za mhimu sana

Nakumbuka Email address na password yake tu.
Simu ipo connected na internet? Ukikosea sana itakupa option ya kuweka email na password
 
Mtoto kabadili password kwenye simu yangu sumsang s8 plan

Naomba msaada jinsi ya ku unlock bila kufuta taarifa zangu zozote yaani bila ku restart simu sababu ni za mhimu sana

Nakumbuka Email address na password yake tu.
Unaweza jaribu kutumia chimera tool nazani uki2mia credit na ikiwa pto account inaweza zisoma hizo pass
 
Kweli wanaume wameisha unakuja kulialia ishu za password kwenye mtandao.

Dah aisee... Bagosha
 
Hahaha! Ziloi nimecheka kweli kweli, fuata ushauri wa Chief-Mkwawa. By the way mtoto wa standard 6 anasahau vipi passwords?

Nakumbuka akaunti yangu ya Facebook nimefungua nikiwa standard 5 na passwords sikusahau. Embu mtulize akumbuke kwa uzuri.
 
Nakuona upo nyuma ya keyboard unaaminisha watu kwamba wew ni mwanaune. Hongera sana
 
Hahaha! Ziloi nimecheka kweli kweli, fuata ushauri wa Chief-Mkwawa. By the way mtoto wa standard 6 anasahau vipi passwords?

Nakumbuka akaunti yangu ya Facebook nimefungua nikiwa standard 5 na passwords sikusahau. Embu mtulize akumbuke kwa uzuri.
Siku zote huwa hazifanani mkuu, mwenyew mara kibao password za mambo yangu huwa nasahau hadi nirudishiwe kwa email mbadala.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom