kama kichwa cha habari kinavyosema nahitaji support ya kufungua blog hatua kwa hatua maana kila nikijaribu nashindwa wadau
ahahhahaaKumbe unafungua blog kwa Tecno ndio maana haikubali
sasa hapo mbona umefikia pazuri, click hapo BLOG MPYA then utachagua jina la blog, na address ambayo ipo AVAILABLEahahhahaa
nishapita hatua hizo zote mpaka inaandika hv
Hujambo mjukuu wangukama kichwa cha habari kinavyosema nahitaji support ya kufungua blog hatua kwa hatua maana kila nikijaribu nashindwa wadau
Ndugu hata mbuyu huanza kama mchicha, si mbaya kuanza kufungua blog kwa techno tunapishana uwezo..Kumbe unafungua blog kwa Tecno ndio maana haikubali
Inabidi uwe umechangua jina ambalo ni unique au nunua domain itakusaidia au Fanya Promo via Fb & Twitter au online ads yoyote itafanya Search Engine Optimization kuwa kubwa.Nifanyeje ili post za blog ziweze kutoa kwenye matokeo ya google pindi mtu akitafuta habari ambayo ipo ndani ya blog yangu?
Sio jambo jepesi hivyo... ningekuwa na muda ningeeleza kirefu kidogo!Nifanyeje ili post za blog ziweze kutoa kwenye matokeo ya google pindi mtu akitafuta habari ambayo ipo ndani ya blog yangu?
Sio jambo jepesi hivyo... ningekuwa na muda ningeeleza kirefu kidogo!
Kwanza kabisa make sure unatengeneza Keywords kwa posts zako. Three Keywords zinatosha for one post.
Kwa mfano, unaandika juu ya kilimo cha nyanya; unaweza kuwa na sentensi kama:
Nyanya ni moja ya MAZAO YA BUSTANI yanayostawi vizuri mkoani Morogoro. Ingawaje kuna mbegu za aina mbali mbali, lakini MBEGU BORA ZA NYANYA ni tomato source...
Maneno ya herufi kubwa ni KEYWORDS! Why Keywords? Tunatarajia somewhere, any day mtu akitaka kutafuta mbegu mzuri ya nyanya ata-Google maneno "MBEGU BORA ZA NYANYA...!" Na kv wewe content/post yako ina hiyo Keyword basi possibly itatokea kwenye Search Results!
But REMEMBER, kuna blog zingine vile vile ambazo zina article kama and probably with the same Keyword. This means, ya kwako na hizo zingine zitatokea kwenye search results. Now the question is: ya kwako wewe itatokea kwenye page ya ngapi?! Page ya 1, 2, 4 or?
Miongoni mwenu aliyefanya kazi ya kutosha ya Search Engine Optimization (SEO) ndie possible people kutokea kwenye First Page of Search Results and the one with poor SEO practices, atakuwa wa mwisho!
Remember, pamoja na Keywords; TITLE & Description navyo ni muhimu sana tena sana!
In short, good articles with proper keywords and title with SEO Practices ndizo zitkupeleka kwenye First page of search results and probably at the top of the first page! Hiyo kitu inahangaikiwa na sio jambo jepesi kama kutengeneza blog yenyewe!
Kwahiyo usichoke kuandika articles mzuri with KW na baada ya muda utafanikiwa lakini siku moja au wiki...it can take months! Lakini ikiwa blog yako unatumia Kiswahili, inaweza kuwa rahisi zaidi compared to English blog!
SEO ni mada pana sana ambayo wala huwezi kuielezea sehemu kama hii na ikawa na impact.Mjukuu wangu chige ukipata Muda ningependa utujuze mawili matatu kuhusiana na swala zima la SEO. (Search Engine Optimization)
1. Ni nini??
2. Faida zake ni nini??
3. How do i Practise it??
Swali langu jingine pia je Naweza ingiza baadhi ya Keywords kwenye Source codes za Website yangu ili kuweza ongeza results kwenye hyo SEO?? (nisahihishe kama nimekosea )
Nawasilisha
Babu Kifimbo cheza
SEO ni mada pana sana ambayo wala huwezi kuielezea sehemu kama hii na ikawa na impact.
Labda nizungumzie umuhimu wake ili wadau nao waone umuhimu wa kuifahamu SEO. Endapo zamani ungetakiwa kuandika historia ya Che Guevara ungelazimika kwenda kushinda maktaba kupitia machapisho mbali mbali lakini siku hizi utaingia to Google au Yahoo au Bing na ku-search info za Che! Kama nilivyogusia jana na ndivyo tufanyavyo, utatumia KEYWORDS ku-search.
Unapo-search familiar subject lazima itatokea search results ndefu sana; inaweza kufika zaidi ya pages 15 Google wakitoa results zao.
Ktk hali ya kawaida, wewe mafuta habari utaanza na page ya kwanza ambayo inaweza kuwa na entries zaidi ya 10. If you are smart, kabla ya kufungua link yoyote utaanza kwanza kuperuzi kinachoonekana. Kwa mfano, je TITLE inaendana na unachotafuta? Good title nayo ni part of SEO practices. Aidha utaangalia ikiwa description yake ina-reflect unachotafuta! DESCRIPTION nayo ni part of SEO Practice.
Ukiona yote hayo yana-reflect unachotafuta, ndipo bila shaka utafungua link husika or else utahamia kwenye second entry kwenye page hiyo hiyo ya kwanza ya Google search results.
Katika hali ya kawaida, uta-click kwenda second page endapo tu kile unachotafuta umeshindwa kukipata kwenye page ya kwanza vinginevyo utaishia kwenye page ya kwanza tena possibly kwenye first to fifth entry!
Sasa kazi ya SEO ni kuifanya blog au website yako itokee kwenye first page tena top of other search results iwe Google, Yahoo or Bing. Kwamba, mimi niki-type AFRICAN UNIVERSITIES kwenye search bar na ikiwa blog yako nayo umeshapata kuandika content/article kuhusu Universities in Africa; basi nikisha-click SEARCH, aim ya SEO ni kuifanya blog yako itokee kwenye first page tena iwe top of the first page!
Na endapo Title itakayotokea ita - reflect ninachotafuta; obvious nitafungua hiyo link ya blog yako... you're main objective ni ku-drive traffic to your blog na tayari utakuwa umeshani-drive!
Hiyo ndio SEO na umuhimu wake but kusema how to practice, hiyo ni mada ndefu sana.
Lakini kwa kuanzia, emphasize iwe kwenye contents na use of great keywords, titles and description. Hii ni simple practice inayoweza kufanywa na any blogger. Na kv lengo kuu ni ku-drive traffic to your blog, then baada ya kazi yote hiyo lengo la pili ni kwamba hizo traffic utazozi-drive to your blog ziwe reliable blog visitors.