babakijanju
Member
- May 22, 2014
- 13
- 2
Wanajamvi,
Baada ya mihangaiko ya muda mrefu ya maisha hatimae nimebahatika kupata pesa nyingi sana kupitia machimbo ya dhahabu ambayo ni zaidi ya miaka mitano nahangaika kuchimba,naposema nimepata pesa ni pesa kweli si mchezo.
Nina mke wangu aliyenivumilia miaka mingi sana na hajawahi kunitenda pamoja na shida zote,sasa eneo ninaloishi la Msalala mkoani Geita nilidharaulika sana na watu.
Nataka kufunga ndoa ikifuatiwa na sherehe ya adabu ambapo nimetenga milioni 30 ili watu wale na kunywa bure,nataka ktk ndoa yangu niwasili eneo la sherehe na helkopta ili watu waniheshimu maana walinidharau sana.
Anayejua helkopta ilipo na inakodishwa kwa sh ngapi kutoka hapa Mwanza hadi Msalala tafadhali anisaidie ili niwaone wahusika na helkopta yenyewe.
TAHADHARI: Matapeli kaeni mbali msidhani mimi ni mshamba wa kuweza kunitapeli,nipo makini sana kuliko kawaida.
Kwa sasa nipo Kampala,natarajia kuwa Mwanza Mjini Jumatatu ya tarehe 4.
Sitaki dharau ktk kunisaidia kupata hiyo helkopta,kama huwezi pita kimya tafadhali sana.
Me nadhan wakuache tu na hela zako manaake daah!!! Hizo hela ni zako kama huna cha kumshauri jamaa basi just shut up ur poor mouth....me sioni tatizo hapo kwa mtu kutumia mihela yake!!!! Mumuwacheeeeee