Msaada tafadhali; Nahitaji Helkopta ya kukodi Mwanza

Ciprofloxacin.

JF-Expert Member
Joined
Apr 15, 2015
Posts
1,583
Reaction score
2,702
Wanajamvi,

Baada ya mihangaiko ya muda mrefu ya maisha hatimae nimebahatika kupata pesa nyingi sana kupitia machimbo ya dhahabu ambayo ni zaidi ya miaka mitano nahangaika kuchimba,naposema nimepata pesa ni pesa kweli si mchezo.

Nina mke wangu aliyenivumilia miaka mingi sana na hajawahi kunitenda pamoja na shida zote,sasa eneo ninaloishi la Msalala mkoani Geita nilidharaulika sana na watu.

Nataka kufunga ndoa ikifuatiwa na sherehe ya adabu ambapo nimetenga milioni 30 ili watu wale na kunywa bure,nataka ktk ndoa yangu niwasili eneo la sherehe na helkopta ili watu waniheshimu maana walinidharau sana.

Anayejua helkopta ilipo na inakodishwa kwa sh ngapi kutoka hapa Mwanza hadi Msalala tafadhali anisaidie ili niwaone wahusika na helkopta yenyewe.

TAHADHARI: Matapeli kaeni mbali msidhani mimi ni mshamba wa kuweza kunitapeli,nipo makini sana kuliko kawaida.

Kwa sasa nipo Kampala,natarajia kuwa Mwanza Mjini Jumatatu ya tarehe 4.

Sitaki dharau ktk kunisaidia kupata hiyo helkopta,kama huwezi pita kimya tafadhali sana.
 
Eneo unaloishi ulidharaulika,maana yake hukuwa na nyumba ya maana pia
Kabla ya kukuelekeza sehemu ya kukodi helcopter tuma kwanza pic ya mjengo wa maana unaomiliki baada ya kupiga bingo
 
Kila kitu kina side effect zake.
Ukiwa masikini kuna tatizo lake.

Na ukipata pesa za mkupuku kama hivyo zinakurusha akili.
Nakushauri onana na mwanasaikolojia haraka sana,ungekuwa Dodoma ningekuambia uende pale Mirembe wanasaikolojia wapo wengi sana.
Ni kwamba una ugonjwa ila hujagundua unaumwa nini.Kweli pesa umepata lakini zimekufanya upate ugonjwa unaoitwa kitaalam Moneyphobia ambapo wewe unaona upo sawa lakini kiuandishi tu unahitaji tiba haraka sana.

Ni ushauri tu.
 
Tuma laki tisa ya maelekezo fasta
 
Maskini akipata ma.tako hulia pwaa

Mzee Makosa
Iringa
 
Eneo unaloishi ulidharaulika,maana yake hukuwa na nyumba ya maana pia
Kabla ya kukuelekeza sehemu ya kukodi helcopter tuma kwanza pic ya mjengo wa maana unaomiliki baada ya kupiga bingo

Mjengo tayari mkuu,sijajenga nimefanya kununua kabisa wa mil 130 mwanza mjini kapripoint.
 
Kila kitu kina side effect zake.
Ukiwa masikini kuna tatizo lake.

Na ukipata pesa za mkupuku kama hivyo zinakurusha akili.
Nakushauri onana na mwanasaikolojia haraka sana,ungekuwa Dodoma ningekuambia uende pale Mirembe wanasaikolojia wapo wengi sana.
Ni kwamba una ugonjwa ila hujagundua unaumwa nini.Kweli pesa umepata lakini zimekufanya upate ugonjwa unaoitwa kitaalam Moneyphobia ambapo wewe unaona upo sawa lakini kiuandishi tu unahitaji tiba haraka sana.

Ni ushauri tu.

Mkuu mi ni mzima kabisa,usidhani eti nitaishiwa tayari nimenunua nyumba kadhaa,na nimefungua biashara za maana kabisa,ambazo kwa siku sikosi laki 3,kwa mwezi mil 9,sasa sioni tatizo hapo ila nataka tu harusi yangu ifane sana na heshima irudi haraka,
 
Kuna jamaa yangu alibahatika kupata mzigo wa kutosha wa Tanzanite enzi hizo alikodi chopa kutoka Arusha hadi nzega kwa mama wa kambo alipokuwa akidaiwa ng'ombe aliochukua kwa ajili ya kulipa mahari.Aliwalipa pesa ya ng'ombe saba na zawadi za kutosha kisha akaenda kuishi Nairobi Hotelini kwa muda wa zaidi ya miaka 10 huku akiendelea kununua dhahabu.Kwa sasa amelosti na ilibidi arudi Kahama na kupanga kabla hajajenga nyumba yake kwa msaada wa mzungu aliyemzalisha mtoto.Naomba tu utulie kidogo usiwe na papara kwani hiyo pesa unamzidi Bakhresa?Kama huwezi kuulia tafuta psychologist akusaidie "kiroho safi tu"
 
Kila kitu kina side effect zake.
Ukiwa masikini kuna tatizo lake.

Na ukipata pesa za mkupuku kama hivyo zinakurusha akili.
Nakushauri onana na mwanasaikolojia haraka sana,ungekuwa Dodoma ningekuambia uende pale Mirembe wanasaikolojia wapo wengi sana.
Ni kwamba una ugonjwa ila hujagundua unaumwa nini.Kweli pesa umepata lakini zimekufanya upate ugonjwa unaoitwa kitaalam Moneyphobia ambapo wewe unaona upo sawa lakini kiuandishi tu unahitaji tiba haraka sana.

Ni ushauri tu.

Mkuu mi ni mzima kabisa,usidhani eti nitaishiwa tayari nimenunua nyumba kadhaa,na nimefungua biashara za maana kabisa,ambazo kwa siku sikosi laki 3,kwa mwezi mil 9,sasa sioni tatizo hapo ila nataka tu harusi yangu ifane sana na heshima irudi haraka,Na nipo kibajeti,sitakodi helkopta zaidi ya mil 5.ikizidi hapo naacha,usidhani mimi ni juha natumia tu pesa kijinga eti kisa nimepata pesa,nipo makini,nimeamua kufanya hivyo kwa kuwa mke wangu alinivumilia sana.
 
Mkuu jiyahidi kuwa mkweli, naanza kuungana na wanaosema unahitaji mwanasaikolojia.
Mwanzoni tu ulisema ulikuwa baba kabwela na ulikuwa tayari na "mke", , vipi unataka kuoa tena?
Unanikumbusha kitabu cha zamaaani"DARUBINI-UJINGA WA MWAFRIKA"
 
Hivi we jamaa unahela kuliko mimi, mana mimi nimefisadi somewhere kitu kama cha 8.4 bilion halafu nipo kimya kimya tu.
 
nenda pale nyegezi stand kwa juu the way to majengo kuna jamaa nae alikua ggm akapga ela akanunua hua anakodisha anaitwa TANO
 
Wanajamvi,

Baada ya mihangaiko ya muda mrefu ya maisha hatimae nimebahatika kupata pesa nyingi sana kupitia machimbo ya dhahabu ambayo ni zaidi ya miaka mitano nahangaika kuchimba,naposema nimepata pesa ni pesa kweli si mchezo.

Nina mke wangu aliyenivumilia miaka mingi sana na hajawahi kunitenda pamoja na shida zote,sasa eneo ninaloishi la Msalala mkoani Geita nilidharaulika sana na watu.

Nataka kufunga ndoa ikifuatiwa na sherehe ya adabu ambapo nimetenga milioni 30 ili watu wale na kunywa bure,nataka ktk ndoa yangu niwasili eneo la sherehe na helkopta ili watu waniheshimu maana walinidharau sana.

Anayejua helkopta ilipo na inakodishwa kwa sh ngapi kutoka hapa Mwanza hadi Msalala tafadhali anisaidie ili niwaone wahusika na helkopta yenyewe.

TAHADHARI: Matapeli kaeni mbali msidhani mimi ni mshamba wa kuweza kunitapeli,nipo makini sana kuliko kawaida.

Kwa sasa nipo Kampala,natarajia kuwa Mwanza Mjini Jumatatu ya tarehe 4.

Sitaki dharau ktk kunisaidia kupata hiyo helkopta,kama huwezi pita kimya tafadhali sana.

Sijaelewa mkuu, ni mke wako ila unataka kufunga ndoa?!
 
Duuuh hiyo bei ya 130m huwezi pata nyumba capripoint itakua umevuta y tabora

Unachekesha kweli wewe,nyumba zote za kapripoint zinalingana bei? Unajua huyo aliyeniuzia kwa nini kauza kwa bei hiyo? Ana mgonjwa mke wake yu mahututi sana anatakiwa kuwahishwa India kwa matibabu nyumba ilikuwa mil 220 hadi akalegea nikatoa hiyo 130 cash,walikosekana wa kumpa zote cash ikabidi awe mpole,jaribu kuwa na akili wewe,ukiwa na shida na una nyumba ya mil 350 huwezi kuiuza kwa bei hiyo lazima ishuke,wewe umekulia dunia ipi?
 
Back
Top Bottom