Isikupe shida sana wala usishangae kuona anatumia Free of charge
Receiver inaweza kuwa DVB-S ambayo ni MPEG2 au hata DVB-T2(Nafikili mara nyingi vile vya terestrial kama startimes ya antenna) na yenye uwezo mkubwa ni DVB-S2 ambayo sana sana tunaita MPEG4
Channel za satellite ziko za aina tofauti tofauti kuna ambazo ni FTA(Free to air) hizi hauitaji kulipia hata senti zaidi wewe uwe na dish na receiver husika mara nyingi ni vema iwe receiver ya MPEG4 maana kuna channel ni FTA lkn bila MPEG4 hauwezi zifungua
Pia kuna ambazo ziko ENCRYPTED/LOCKED yaani hizi ili uzifungue lazima uwe na funguo/Keys/Control word walizozifungia hamna cha funguo malaya hapa...
Lakini katika huu ufungaji kuna Keys hazibadiliki hata baada ya miezi na hapa ndo tunapata matumii ya vitu kama BISS KEYS ambazo ukiwa nazo unaona channel bila shida e.g IRIB na TV3 ambazo uonesha soccer kwa asilimia fulani zimefungwa kwa BISS keys hivo ziki leak uwa mtandaoni na kama una MPEG4 ambayo ina uwezo wa kuwekewa Keys basi utaweza kuziona bila shida
Ufungaji wa pili ni kama unaotumika na DSTV,AZAM etc ambazo funguo/keys/control word zake zinabadilika kila mda hivo vigumu kabisa kuziona bila kulipia(lakini siku zote hamna SYSTEM ILIYO 100% SECURE) ukitaka kujua namaanisha nn tembelea Hii link ujionee
Jipatie DSTV kwa kutumia AZSKY Dongles - Page 2