Msaada tafadhali,Kipato cha binti cha mtoa nduki jamaa..! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msaada tafadhali,Kipato cha binti cha mtoa nduki jamaa..!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Cantalisia, Nov 23, 2011.

 1. Cantalisia

  Cantalisia JF-Expert Member

  #1
  Nov 23, 2011
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 5,229
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Habari zenu wapendwa,
  Kuna mkaka ni mkazi wa dar ila anafanya kazi mgodini huko mwanza huku anakuja kila baada ya miezi miwili,Alikutana na mdada huko mwanza Mdada anafanya kazi huku dar kule alienda kikazi,wakapeana kontakt, na mawasiliano yakaendelea na wakawa wapenzi.

  Kwa kipindi cha miezi minne ya mahusiano yao hakuna aliyekua anajua kwa mwenzie,basi wakapanga jamaa atakapokuja dar wakaoneshane makwao,basi jamaa akarudi dar ijumaa iliyopita km kawa wakakutana na jmosi jamaa kampeleka mdada kwake tabata wakashinda huko wakapika na kupakua.

  Jpili mdada naye akampeleka jamaa kwake maeneo ya Sinza hapo ndio balaa lilipoanzia kwan muda wote wakiwa pale yule mkaka alikuwa hana raha mwenzie akamuliza kulikon mbona ulikuja vizuri,yy akamuuliza pale anaishi na nani akamwambia mbona nilishakwambia naishi peke yangu.

  Akamwomba amwonyeshe slip yake ya mshahara mdada akapigwa butwaa ila akamwonyesha kumbe kaharibu jamaa kanyanyuka na kuondoka akiwa amekasirika mdada hakumwelewa akambembeleza bila mafanikio,usiku wake jamaa akamtumia bint msg kuwa hamtaki tena,kwa sababu anahisi huyo mdada atamtawala maishani kwa vile kwanza ana kipato kikubwa,na ameshajijenga sana kimaisha,hivyo ni rahisi yeye kutokuwa na sauti ndani ya nyumba,au huyo dada anaweza kumwaga wakati wowote na kutoka na wenye uwezo km yy.

  Mpaka ninavyoandika huu uzi jamaa hapokei simu na jana kaondoka kurudi mwanza,dada watu kachanganyikia alishampenda jamaa kupita kiasi hata hajui cha kufanya!

  Asa mi nauliza hivi nyie wanaume hivi binti kuwa na kipato kikubwa kuliko mwanaume ni kweli ni tatizo kwenye mahusiano?
  Na dada afanyaje ili jamaa aelewe na waendelee?
   
 2. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #2
  Nov 23, 2011
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Hampendi huyo aachane naye
   
 3. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #3
  Nov 23, 2011
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,676
  Trophy Points: 280
  Huyo jamaa ni aina ya wanaume aliowasema Bishanga,ila sio WANAUME aliowasema Aspirin,huyo jamaa hajiamini kabisa na hafai kuitwa mwanaume,hebu huyo binti akutane na MWANAUME kama mimi,lazima kwa kuunganisha nguvu tungekua na mjengo kama wa NSSF!!
   
 4. Zanta

  Zanta JF-Expert Member

  #4
  Nov 23, 2011
  Joined: Apr 4, 2011
  Messages: 2,017
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Mambo ya kurudi usiku na kuambiwa kalale huko huko huko hapa kwangu usikanyage nani anataka?
  Asikwambie mtu, kutokana na mfumo tunaoishi kwa asilimia kubwa bado wanaume hawajaweza kua na imani ya kupendwa na kuheshimiwa na Mwanamke mwenye kipato kikubwa sana. Mimi kama mimi civil servant nalamba laki tatu, halafu mpenzi wangu yupo kwenye Shirika kubwa analamba Million tano, kwa kweli hapa nadhani Imani lazima isiwepo, maana kitu kidogo tu mwanaume atahusisha na kipata then maelewanoi ndani ya nyumba hayata kua mazuri.
  Mkaka ana haki ya kula kona kwa kweli mi hata simshangai.
   
 5. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #5
  Nov 23, 2011
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Kwa hiyo jamaa amesha kula mzigo tayari?
   
 6. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #6
  Nov 23, 2011
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Hahahaha hapa mzazi umemaliza ni kheri mwanaume awe na pesa au kipato kikubwa na si mwanamke, wanawake wana dharau sana wakiwa wanamake mihela mingi hajali kama wewe ni mme wake licha ya kukaa kwenye nyumba yake.
   
 7. Zanta

  Zanta JF-Expert Member

  #7
  Nov 23, 2011
  Joined: Apr 4, 2011
  Messages: 2,017
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Kupenda nako kunachangiwa na mambo mengi,
  Mfumo wetu bado haujakaa sawa sawa kwa kweli
   
 8. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #8
  Nov 23, 2011
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Huwa mnakuwa madikiteta wa mapenzi madikiteta wa mahusiano madikiteta wakila kitu.
  Mwanamke mwenye pesa/nazo namuogopa kama ukoma na ukimwi hafai heshima ndani ya nyumba inapotea.
   
 9. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #9
  Nov 23, 2011
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,933
  Likes Received: 2,084
  Trophy Points: 280
  Ni tabia/akili ya mtu tu. Hata mwanaume akiwa na pesa/kipato kikubwa kuliko mwanamke bado inaweza kuleta shida/matatizo katika mahusiano.
   
 10. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #10
  Nov 23, 2011
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Mwanamke wa kibongo awe anamiliki bingo kubwa kuliko mwanaume mbona utanyanyasika utasikia hizo gari nimenunua mimi wewe unapanda na malaya wako mara sijui nini nawaona washkaji wanavyo nyanyasika na wanawake wenye pesa kwa kweli kibongo bongo hawafai.
   
 11. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #11
  Nov 23, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 279
  Trophy Points: 180
  Mkuu si ulisikia walipika na kupakua huko tabata!
   
 12. laussane

  laussane JF-Expert Member

  #12
  Nov 23, 2011
  Joined: Oct 8, 2009
  Messages: 255
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  always pointless
   
 13. Zanta

  Zanta JF-Expert Member

  #13
  Nov 23, 2011
  Joined: Apr 4, 2011
  Messages: 2,017
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Kweli Mzazi, asilimia kubwa ndo hivyo, unajua haya mambo bado yanenda na mfumo uliopo ndo maana hata hapa ukiuliza mabinti wenyewe hua wanasema wanapenda kuolewa na Mtu alie mzidi umri, na sababu wanasema mwanaume ndo kichwa cha Familia sasa wewe na laki tatu zako unaleta dagaa wakati mama anapitia super market kila siku?
   
 14. Zanta

  Zanta JF-Expert Member

  #14
  Nov 23, 2011
  Joined: Apr 4, 2011
  Messages: 2,017
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Kwani shida ikwapi hapo?
   
 15. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #15
  Nov 23, 2011
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Inategema labda demu alibana masaburi wakapime ngoma si unajua mademu wa kibongo mapenzi ya isidingo mnaweza lala hata wiki na asikupe mzigo mpaka mkapime ngoma Angaza
   
 16. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #16
  Nov 23, 2011
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,676
  Trophy Points: 280
  Maneno ya wasiojiamini hayo!
   
 17. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #17
  Nov 23, 2011
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Haya mama
   
 18. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #18
  Nov 23, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 279
  Trophy Points: 180
  Tena hawachelewi kukwambia eti 'wewe ni mwanaume suruali tu'. nani anataka huo ujinga, akhaaaaaaaaaaa! Mwishowe unakuja kutumwa kwenda sokoni kununua viungo vya pilau. Acha kabisa hawa mademu wa kibongo wenye nazo, utazodolewa mwanaume mpaka utamani ardhi ipasuke.
   
 19. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #19
  Nov 23, 2011
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Asubiri mwenye kipato kumshinda yeye...... huyo amuwache aambae.

  Yanini kuishi na jamaa hajiamini?
   
 20. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #20
  Nov 23, 2011
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Hahahaha mzee unalipwa kima cha chini cha JK unaleta matembele mama anapitia super market mshahara wake mnono na malupu lupu lazima usepe machafu anaweza kwambia acha kazi uwe unasimamia shughuli za kila siku hapa nyumbani.
   
Loading...