Msaada Tafadhali:Hivi huwa ni Kuoa;Kuolewa au Kuoana??

Sijawahi kuhudhuria ndoa za kiislam...kumbe wote kwa pamoja huwepo kukubaliana kuungana(kuoana)


Katika Uislaam, muhimu ni sharia na kanuni za ndoa. Ndoa ni mkataba baina ya wanao oana, kuoana kwa maana ya kuwa "pair", hamuwezi kuoana kama hamjakubaliana kuoana na hayo makubaliano yenu ni lazima yajumuishe anaewafungisha hiyo ndoa, mashahidi, na ma/wakala wanaokubalika kisheria wanaowakilisha kila upande. Kuna haki za msingi na vigezo vya Kiislaam ambavyo hivyo haviepukiki na kuna makubaliano ya ziada ambayo hayakiuki sheria za Kiislaam amma yanaweza kuwekwa kwa maandishi amma yanaweza kutangazwa mbele ya mashahidi na mawakala.

Kiislaam, mwanamme huulizwa peke yake mbele ya mashahidi na mawakala kama amekubali kuoana na fulani na mwanamke huulizwa peke yake mbele ya mashahidi na mawakala kama amekubali kuoana na fulani. Hii inatoa fursa ya wanaooana kuwa na uhuru bila ya shinikizo kwa yeyote kati yao.

Na sheria nyingine za nchi ambazo hazipingani na sheria za Kiislaam nazo hufatwa, kwa mfano kutangazwa kwa nia ya kuoana kabla muda fulani wa siku ya ndoa.

Uislaam pia hauruhusu uchumba wa kuishi pamoja na kugegedana kabla ya ndoa, wafanyao hivyo ni wazinifu na watoto wataopatikana hapo ni wa nje ya ndoa hata ikiwa watu hao watakuja kuoana baadae. Watoto wa nje ya ndoa Kiislaam hawawezi kumrithi "baba" wanaweza kumrithi "mama" tu na pia hawawezi kutumia ubini wa "baba".
 
Mwanaume anaoa na mwanamke anaolewa, au wanaoana. Kama mwanaume ni alosto kama bin fulani anaolewa...yaani wapenda dezo akina yahaya
 
Back
Top Bottom