Liverpool_Jr
JF-Expert Member
- Sep 7, 2019
- 1,220
- 1,411
Iko hivi
Kifupi nilianza kuajiriwa private nikiwa na Diploma, na kwasababu ya njaa ya kusoma nilitafuta kazi serikalini ili nipate ruhusa ya kusoma (Bachelor na Masters) maana private sector walinibaniaga (nilifanya ofisi 3 tofauti na zote walinibania kusoma).
Nilivyohitimu Masters yangu niliachana na serikali (lengo lilikuwa ni kusomeshwa tu).
Na kwasababu ya kupenda kusoma nilionaga fursa kwenye makala fulani hivi ya biashara, hivyo nilivyoacha kazi serikalini nilijiajiri humo.
Kwasasa biashara ni bora na nzuri. Ashukuriwe Mungu.
Ila tatizo linakuja hapa:
Kifupi napenda sana na kila siku kwenye shughuli zangu nisipokuwa kwenye biashara basi nipo juu ya PC nasoma au namfanyia mtu academic activities (research, business plan, proposal, etc).
Na hata kwenye biashara nikiwa bored huwa nachomoa simu na kuanza kusoma google au vitabu (PDF).
Sasa tokea nihitimu Masters yangu mwaka juzi (MSc. Finance) nimekuwa bado natamani kusoma tena Masters ya Uchumi (MSc. Economics)
Yaani mwaka jana na hasa wiki hii ninavyoona watu wana hitimu Masters zao roho inaniuma balaa.
Nina BSc. Economics & Finance, MSc. Finance na bado natamani MSc. Economics.
Wapo wanaonishauri "niachane na kusoma kwa vile nimejiajiri, Eti kusoma kuna maliza pesa" Huwa nawajibu "Tunatafuta pesa ili kufurahisha moyo"
Wapo wanaosema niende nikasomee nje (Ilaya au USA) ila tatizo nikitoka biashara zangu zitayumba.
Wakanishauri nioe kwanza then nimuachie mke asimamie biashara halafu mimi niende kusoma nje, hili pia hapana maana kwanza, sina mpango wa kuoa leo wala kesho na pia huwa siamini mtu kabisa asimamie biashara zangu.
Sasa wana JF hebu nisaidieni niweze kutoa hii njaa maana huwa inatesa sana.
Moyo unaniuma Masters ya pili naitaka na huku sometimes sielewi.
Aliyepataga njaa kama hii alitumia njia gani aka escape?