Msaada: spare za magari yalisitiswa uzalishaji

WENYELE

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
1,415
1,379
Wakuu kwema humu?

Naomba msaada wa elimu na ufahamu kidogo? Hivi spare za magari ambayo makampuni ya magari yashasitisha uzalishaji wake huwa zinakua sokoni hadi muda gani zinakua hazipatikani tena?

Mfano umenunua gari leo afu baadaye unagudua hizo gari hazizalishwi tena, je spare hupatikanaje?

Wale wa magari ya zamani km 1997 hadi leo wanayo, hutumia spare ganii?

Magari ya miaka ya 80s huko ambayo yapo hadi leo spare hutoa wapi?
 
Wanakata spear za aina ya gari yako iliyopo jifia.. Labda pia kuna special order ( sina hakika) ila pia zinakuwepo zinazo ingiliana
 
Mkuu umetafuta spare ya gari gan ukakosa? Bedford ya mzee wangu ya mwaka 1962 bado spare zake zinapatikana, Peugeot 402,404,405, Toyota Staut, Ford Anglia, Themes, Zephyr 6, Land Rover 108, 109, 110, VW Kobe na nk spare bado zinapatikana sasa sijui wewe gari yako ni nini na ya mwaka gani!
 
Mkuu nilikua naulizia kupata ufamu tu; km spare zinapatika huchukua muda gani kuadimika?
 
Spea zingine sometimes zikikosekana kabisa zinaenda kuchongeshwa kwenye workshop za kuchongesha vipuri,unachofanya unakwenda,na spea halisi iliyokufa,wanakuchongeshea,mfano kule Morogoro Mzinga Holdings ambayo ni kampuni ya Jwtz wana workshop ya hivyo,sijui mikoa mingine
 
Asante sana mkuu; nimepata idea mpya pia
 
Spea zipo

busworldtanzania_20210204_132649_0.jpg
 
Back
Top Bottom