Msaada: Siri ya Physics advance

edgar90

Senior Member
Joined
Jun 18, 2016
Posts
145
Reaction score
116
Naomba kujua siri ya kufaulu ili somo kwanza nahitaji kujua ni vitabu gani vya kusoma? Harafu pia nitapata wapi solved practicals za physics? Hivi ni kweli ili ufaulu physics inabidi ufoji practicals yaani utumie forging equations?
 
Naikumbuka kanuni T square=4# square x l over g

sasa kupata slope=4 pie square over g sasa pie square na g(gravit) ni the same hivyo unazicancel

sasa tena slope inakua s=4l kujaza table inakua rahisi l ina kuwa known kwa sababu ni length ya FROM BOB TO THE ATTACHMENT OF THE STRING
 
Soma vitabu vifuatavyo at least 5 visipungue chini ya hapo
1😛rinciples of physics by Chands
2:advance lev phys by roger muncaster 4th edition
3:advanced lev phys by Tom duncan 5th edition

4:modern abc
5:advanced lev phys by nelkon & parker 7th edition
6:new understanding phys
7:calculation for alev phys volume 1&2
8:contemporary phys by kiiza
9😛hys necta question(review) plus other past papers

unaposoma reviews, solve tu maswali na kuyatafutia majibu katika vitabu vingine nilivyokutajia hapo juu, usipende kuchukua majibu ya hizo reviews kwa sababu wamekosea baadhi ya maswali
 
kufaulu phys ni very simple tu mdogo wang kwa sababu always principles of phys never contradict tofauti na masomo mengine kama chem, ambapo baadhi ya principles zinakubali sehemu fulani ila kwengine zinakataa, cha muhimu fanya yafuatayo
1:itengee muda mwingi wa kujisomea at least 4 hours per day, everyday
2:jijengee tabia ya kupitia yale uliofundishwa siku hiyohiyo,usilaze vitu hata siku moja kwa kuwa ukipitia tena utaona vitu kama vipya kabisa
3:ukifundishwa kitu nenda extra miles kwa kupitia vitabu sehemu zinazoelezea part hiyo hiyo,jitahidi upitie hata vitabu vitatu katika part hiyo hiyo moja
4:hakikisha unapitia examples za kutosha sanasana kwenye kitabu cha principles of phys cha chands
5:hakikisha definition zote zipo kwenye fingertips pamoja na SI units
6:jitahidi unajua derivation za equations nyingi kadri uwezavyo ,usikubali kushindwa ku derive equation hata moja,
7:solve past papers za kutosha hakikisha hukosi swali,
8:jijengee tabia ya kuchora diagrams pamoja na kupangilia kazi yako katika mtililiko mzuri,hata kama unalijua hakikisha una record data zako vizuri , andika equation itakayotumika mwishoni ndio una pachika data zako, hii itasaidia kukupa baadhi ya marks hata kama final answer sio correct
 
kuhusu mambo ya forgery hapo ni kwamba ina faida zake na hasara zake, faida zake ni kama ifuatavyo

1:itakusaidia kumaliza maswali katika muda mfupi na kukupa muda wa kutosha wa kuchora graph
2:graph yako itakuwa ni sahihi kwa kiasi kikubwa kwa kuwa utajua slope inayotakiwa pamoja na X na Y intercepts
3:unaweza kuandika practical report bila ya kugusa kifaa hata kimoja
4:inasaidia sana sana pale vifaa vinapokugomea, mfano prack za umeme zinasumbua sana kwa hiyo ukijua jinsi ya kuforge itakusaidia sana

Hasara za kuforge
1:inabidi uwe smart sana kwenye mathematics bila hivyo utapata majibu ya ajabu sana kwa kuwa ukikosea step moja tu kwenye ku derive forgery equation basi ushaenda na maji

2:kuna forgery equations nying sana mfano kwenye mechanics zipo si chini ya hamsini, hapo bado umeme ingawa prack za heat forgery equations zake ni chache

3:baraza la mitihani wanasahihisha mitihani kulingana na majibu yaliyoletwa na lab tech katika shule husika, hivyo basi kama utaforge inamaana utapata majibu ya peke yako kwa kuwa lab tech ataandika prack report kulingana na alivyoiandaa yeye kwa hiyo kama utaforge itakuwa ni rahisi kujulikana hivyo basi prack report yako yote itakatwa

5:ukizoea ku forge utapata majibu ambayo ni very exactly kwa hiyo utagundulika kuwa ume forge kwa kuwa si rahisi ukapata jibu kama lilivyo kwa kuwa wakati wa kufanya practicals kuna errors nyingi sana kama vile hali ya hewa pamoja na vifaa husika


Kwa hiyo basi kwa ushauri ni kwamba usipende kujizoesha ku forge, inachotakiwa ni wewe kuelewa concept darasani kwa hiyo ukienda lab haita kusumbua kwa kuwa kwenye prac kila kitu unaelekezwa jinsi ya kufanya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…