Msaada: Sina msingi mzuri wa kufanya presentation, napata shida

Kapepo

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2015
Posts
1,078
Reaction score
1,227
Wakuu habari zenu humu, mimi ni mwanafunzi wa chuo kikuu mwaka wa tatu sasa tatizo linalonisumbua ni kwamba sina msingi mzuri katika maswala ya presentation tangu o-level hadi hapa chuo huwa siwezi nkafanya presentantion kabisa nakuwa muoga kuongea mbele ya umati wawatu nashindwa kuelewa tatizo nini nashindwa kujiamniani. Nilikuwa naomba msaada wenu nini cha kufanya ili niweze kuongeza kujiamini katika kufanya presentation kwani niko mwaka wa mwisho sasa na kuna presentation nyingi sana ili niweze kupata degree yangu ya kwanza naombeni ushauri wenu wakuu
 
Tumia kiroba Original dakika 30-45 kabla ya presentation... Utapiga kikristo mpaka mwenyewe utajikataa... watu wana acknowledge kiroba kwenye dissertations
 
Chukua bangi usitoe mbegu piga ile kitu ani hata mbele ya magufuli unaeza dai haki yako..... Hata mbele ya obama unaongea pia utapata uwezo wa kunena kwa lugha zote
 
sasa mpaka umefika mwaka wa tatu huko mwanzo ulikua unafanyaje we msomi? au mmeanza kupresent mwaka wa tatu? Tatizo ni nini lugha au unaogopa nini??
 
Wakuu habari zenu humu, mimi ni mwanafunzi wa chuo kikuu mwaka wa tatu sasa tatizo linalonisumbua ni kwamba sina msingi mzuri katika maswala ya presentation tangu o-level hadi hapa chuo huwa siwezi nkafanya presentantion kabisa nakuwa muoga kuongea mbele ya umati wawatu nashindwa kuelewa tatizo nini nashindwa kujiamniani. Nilikuwa naomba msaada wenu nini cha kufanya ili niweze kuongeza kujiamini katika kufanya presentation kwani niko mwaka wa mwisho sasa na kuna presentation nyingi sana ili niweze kupata degree yangu ya kwanza naombeni ushauri wenu wakuu
Kinachokufanya utetemeke ni yai hakuna au ni kitu gani?
 
Kujiamini ni inborn thing Mkuu na kamwe usitegemee kama Mababu na Mabibi zako wa Koo zako zote mbili katika Kipindi chao walikuwa waoga wa kutukuka basi Wewe sijui Mjukuu au Kitukuu au Kilembwe utakuwa mjanja sana sana na Wewe utapita tu mule mule walikopita wao. Siku zote maji hufuata mkondo Mkuu!
 
Mkuu iyo haihitaji kiroba wala bangee!

Jiandae vizuri akikisha unauelewa wa kutosha juu ya mada utakapresent.
Hii itakuongezea confidence kwani utakua na uhakika na kile unachokisema mbele za watu

Nenda makbata, google na usome content uelewe vizuri utafanikiwa!
 
assante wadau kwa ushauri naendelea kusoma maoni yenu ili niyafanyie kazi
 
Mkuu ushamaliza chuo ndo unakuja kuomba ujuzi

Bapa moja itakutosha kupresent vizuri
Tumia 1x1
 
Kwanza tayarisha presentation yako na uwe na hakika na ulichokiandika. Pili tafuta rafiki kutoka darasani kwako na kutumia vigezo vya muda na pia aina ya presentation (karatasi au PPT) fanya mock presentation. Siku ikifika panda stage anza kupresent angalia watu kama msitu bila kuona mti mmoja mmoja unapoanza halafu jinsi unavyoendelea piga eye contact na malizia.
Record maswali utakayoulizwa na jibu accordingly. Ukirudia mara mbili tatu utakuwa fit. Zoezi kama hili chukulia ya kuwa ni kama matayarisho ya Interview huko mbeleni.
 
Wakuu habari zenu humu, mimi ni mwanafunzi wa chuo kikuu mwaka wa tatu sasa tatizo linalonisumbua ni kwamba sina msingi mzuri katika maswala ya presentation tangu o-level hadi hapa chuo huwa siwezi nkafanya presentantion kabisa nakuwa muoga kuongea mbele ya umati wawatu nashindwa kuelewa tatizo nini nashindwa kujiamniani. Nilikuwa naomba msaada wenu nini cha kufanya ili niweze kuongeza kujiamini katika kufanya presentation kwani niko mwaka wa mwisho sasa na kuna presentation nyingi sana ili niweze kupata degree yangu ya kwanza naombeni ushauri wenu wakuu
Nilikuwa na tatizo kama lako, mimi ni mtu wa aibu lakini nilianza kuongea kanisani kulinisaidia sana.
 
Pole aisee,

ila hatua hii tu ya kuleta mada yako hapa inakupatia ufumbuzi

1. Andaa kazi yako wewe mwenyewe ili uweze kuelewa kila kipengele vizuri. (usiandaliwe kazi na mtu mwingine)
2. Soma kazi yako vizuri na kisha fanya mazoezi binafsi kabla ya kupresent, pia waweza kuwa na kikundi mnachosoma pamoja ikawa ni sehemu mojawapo ya kufanyia majaribu kabla hujafanya presentention

3. Andika hoja zote za muhimu usisome kazi yote unapokuwa una-present [namanisha soma kazi yako, isome kisha andika ufupisho kwa kuchukua poiti za muhimu zinazobeba mada yote itakurahisishia kupresent]

4. Unapo simama mbele za watu usiwaze wanavyokufikilia ama unavyowaona walivyo wengi ama wanavyokukodolea macho ila wewe jikite katika mada yako na present bila wasiwasi.

5. Angalizo,
Kumbuka , usitumie kilevi ama bangi au sembe ili upate kusimama vizuri ama kupresent bila uoga,
Ndugu, utaaibika na kupata alama mbaya sana bure kwa kujitakia
Ufumbuzi wake ni wewe kujiandaa na kufanya mazoezi. Utaweza.

6. Pia, jitahidi kila presentation hakikisha unapata mada ama mada ndogo ya kupresent usiwe msindikizaji kwa kazi zile za kufanya kama kundi (group presentation)

6. Mwisho, waweza ni PM nikuelekeze zaidi kama utaona umuhimu wa kufanya hivyo.

Nikutakie kila la kheri na mafanikio mema katika maandalizi ya kupata degree yako.

Ahsante sana
 
Mfano, presentation huwa wanatoa , case study, ie kwa education huwa kuna maswali unagawiwa, and then unaanza kujiandaa kwa kwenda library , Onyo usitumie wekipidia, soma vitabu, lekebisha grammar and tense, tatizo la confidence ni, psychological problem, na pia unaweza kuli clear, mfano jiamini, ondoa woga,
Mda wa presentation usiwa face client wako usoni utakosa confidence, watazame juu ya vichwa vyao ie avoid kuwaangalia machoni, improve your language, , na kabla ya kufanya presentation fanya majalibio kwenye kioo kikubwa ili uone mistake zao, avoidi fear, usitumie kilevi chochote,
Mwisho, avoid fear, fear create worry
 
Back
Top Bottom