Msaada: Simu yangu haipokei sms

Kikwata

Member
Feb 3, 2015
53
61
Habari wana JF,
Nimepata tatizo moja kwny simu yangu, Samsung Note II ghafla imepata tatizo la kutopokea sms, ukijaribu kutuma sms kwa mtu mwengine zinaenda bila tatizo, shida ni pale mimi ninapotumiwa sms.

Nimejaribu kuchek centre number haina tatizo. Naomba mwenye ujuzi wa tatizo kama hili aweze kunisaidia ufumbuzi.
natanguliza shukrani.
 
Angalia kitu kinaitwa center number... Nenda kwenye sms settings... Hiyo center number ndio inafanyaga simu iweze kupokea ujumbe...
 
wakati mwengine hutokea ukiwa na app nyengine ya sms kama vile hangout hujieka kama default sms app. halafu hio app inakuwa outdated na kuacha kupokea sms. sms zinatoka sababu wakati wa kutuma unatuma na yoyote ila wakati wa kupokea default ndio inapokea.

jaribu kwenda message halafu setting halafu tafuta default sms app hakikisha ni hio inayokuja na simu na sio app nyengine
 
Fungua uwanja wa sms kisha upande wa kulia juu utaona kunavidoti vi3 "Hutegemea aina ya simu uitumiayo" kisha bofya hapo. Pakifunguka nenda kabofye palipoandikwa sms enabled kisha utabofya tena palipo andikwa messaging default.
Mpaka hapo nadhani itakuwa sawa
 
Back
Top Bottom