Msaada: Sijatuma maombi ya JKT mpaka sasa

Bill of Quantity

JF-Expert Member
Dec 2, 2014
1,233
405
wakuu habari za sasa?
mimi ni kijana wa shahada ya kwanza, kutokana na matatizo yaliyo nje ya uwezo wangu, nilishindwa kutuma maombi ya kujiunga na JKT japo siko nje ya muda. tatizo la kwanza nimekosa academic transcripts kutoka chuoni kwangu, wananizungusha jamani. Naombeni ushauri wenu, nawezaje kutuma maombi bila academic transcripts ya chuo?
Karibuni
 
Umechelewa Mzee, watu wadhafanya interview wilayani Na mkoani pia wanasubiri vipimo final Na interview ya mwisho kwa wajeda wanaotoka makao makuu.
 
Umechelewa Mzee, watu wadhafanya interview wilayani Na mkoani pia wanasubiri vipimo final Na interview ya mwisho kwa wajeda wanaotoka makao makuu.
mkuu lakini naona imeandikwa mwisho ni mei 20? inakuwaje hapo nichelewe? msaada wako
 
ungetumia cheti cha form six kwanza ukimaliza kuhenya ndoo unakuja kuchukua cha bachelor hujachelewa tumia plann B
 
mkuu lakini naona imeandikwa mwisho ni mei 20? inakuwaje hapo nichelewe? msaada wako[/QUOTE
mkuu lakini naona imeandikwa mwisho ni mei 20? inakuwaje hapo nichelewe? msaada wako
Hata mimi nashangaa Kufanya usail kabla ya Tarehe ya mwisho wa kutuma maombi kufika Mfano; niliomba Wilaya wa Njombe Lakini sasa walishafanya usaili Tarehe 28/04/2016 Interview na sasa wapo ngazi ya Mkoa!
 
Ingia kwenye WEB yao na waulizie pengine kuna utaratibu mwingine!
Hatujaendelea nchi hii kiasi pawe na taarifa sahihi za wakati huo kwenye mtandao, eti pawe na mtu anayejibu maswali ya wateja mbalimbali kwa wakati - sijaona kwenye website za taasisi zetu. Labda aende physically kwenye ofisi za wakuu wa wilaya akaulize, au apige simu.
 
Back
Top Bottom