Msaada screen flickering Galaxy S4

Msaada screen flickering Galaxy S4

nerilan

JF-Expert Member
Joined
Dec 11, 2013
Posts
469
Reaction score
713
Habari yenu wakuu.

Naomba msaada wenu kwa yeyote anayefahamu utatuzi wa jambo hili.

Ninatumia Galaxy S4, lakini hivi karibuni imeanza pindi unapoweka power saving mode au auto brightness au ukashusha brightness level mpaka kiwango cha chini basi screen huanza kutetemeka mwanga (flickering) kama ilivyo kwenye baadhi ya computer monitors za zamani.

Pia pindi screen inapotaka kujizima baada ya kukaa muda flani bila kutumiaka (idle) huji-dim na pindi hali hiyo inapotokea basi screen flickering hutokea pia.

Cha ajabu, brightness level inapokuwa ya kawaida au screen inapokuwa normal kabla ta kuingia kwenye dimming na kujizima kunakuwa hamna mtetemo wa mwanga wa kioo.

Nimejaribu google na inaonekana ni tatizo kubwa linalokumba watu wanaotumia S4 na wengine wamebadili hata simu ila shida iko palepale, na wengine hata dispay.

Nimejaribu kucheza na settings ila hamna mabadiliko na kadri muda uendavyo naona flickering inazidi. Nimejaribu update software ila bado tatizo lipo..

Naomba msaada wenu wakuu. Kama naweza pata application itakayoweza disable dimming kabla screen haijazima itanisaidia. Pia kama kuna mtu anayejua solution please anisaidie..

Forum ya xda developers wamejadili sana suala hili ila hawahatoa ufumbuzi.

Simu inatumia kitkat 4.4.2 na simu haiko rooted.

Asanteni
 
Msaada wenu wakuu unahitajika. Yeyote mwenye tatizo kama hilo?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom