Kwa kuwa ni mgeni panda Taqwa au Falcon yanayoelekea Zimbabwe yanapita Lusaka nauli ni 90,000 mpaka 80,000 wanakubali ila yanafika usiku sana Tunduma mnalala hapo asubuhi unaendelea na safari hakikisha una kadi ya chanjo wazambia kwenye kugonga passport wanasumbua kama hauna uwape rushwa na sasa hivi safari za bus Zambia ni mchana jioni ya saa kumi na Mbili utakua umefika Lusaka.Wewe una budget ya hotel kiasi gani kwa siku maana kuna blue water ipo njia ya Chawama,Town hapo intercity zipo kama tano hivi Mbili za bei ghari tatu bei ya kawaida ila sio sawa na Dar kwa Nchi za kusini Zambia Hotel zipo juu sana na pia kama kwenda uende na dollar harafu uongee na konda wa bus umpe kama laki au laki Mbili yeye ndio abadilishe hapo Tunduma kwa mgeni watakuchanganyia mahesabu watakuibia tuu wengi wa dasalama wanaibiwa hapo ukiwa mgeni all in all Lusaka gharama za chakula na Tax ni kama bongo tuu...35,000 Zambian Kwatcha Nsima(ugali) na Samaki (Nsomba) Mkubwa...