Msaada: Rais Kikwete na aina ya kufungua Champaigne...

Msaada: Rais Kikwete na aina ya kufungua Champaigne...

Tusker Bariiiidi

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2007
Posts
5,554
Reaction score
2,160
Wadau Salaam! Nimeona picha ya Rais JK katika ukurasa wa mbele katika gazeti la Sauti ya watu Tanzania la leo tarehe 5 June 2009 akivunja chupa ya mvinyo kuashiria kuzindua kivuko kipya cha Mv.Magogoni katika hafla iliyofanyika eneo la Ferry,naomba wadau mnisaidie;Champaigne inavunjwa au inafunguliwa??
 
Last edited:
Wakati wa kuzindua meli mpya champagne huwa inavunjwa kwa kupigwa kwenye meli yenyewe. Tena isipovunjika inaleta bad luck.
3031082145_2acf62d3f4.jpg
 
Mwanawane hii kali, hiyo imani ya bad luck nadhani ni kwa wazungu. Je sisi zamani tulipokuwa tunafungua jahazi jipya enzi za kale tulikuwa tunafanyaje? Au ndo mambo ya kuiga iga. Tudumishe utamaduni wa Mtanzania.🙄
 
Nami pia niliiona picha. Nadhani muungwana alitakiwa avae gloves kwani kuna hatari chupa ingemkata mkononi, halafu ashindwe kusaini mikataba !!
 
Nashukuru Kang kwa maelezo hayo maana kwangu mimi ni MASHOGKHOLO MAGENI... Nikajua JK anapiga Ramli? Vp? Katika vitabu vya dini? Na kwa wale wanovunja nazi NJIA PANDA? Wadau nijuzeni??
 
Mwanawane hii kali, hiyo imani ya bad luck nadhani ni kwa wazungu. Je sisi zamani tulipokuwa tunafungua jahazi jipya enzi za kale tulikuwa tunafanyaje? Au ndo mambo ya kuiga iga. Tudumishe utamaduni wa Mtanzania.🙄

Sisi si tunavunja nazi badala ya Champagne, ama?

Au wadau watasema shirka?
 
Ilitakiwa kuvunja nazi na mayai visa na kupakaza damu ya mbuzi aliyechinjwa kwa kukatwa au kupasuliwa tumbo akiwa hai, kisha kutupa nyama zote kwenye maji au baharini.
 
Back
Top Bottom