Msaada rafiki yangu kaibiwa.

Karot

JF-Expert Member
Mar 6, 2017
1,153
1,303
Habari za majukumu wakubwa na wadogo.

Niende moja kwa moja kwenye mada.

Leo asubuhi mnamo mida ya saa tatu rafiki yangu ameenda maeneo ya Kwerekwe sokoni na kupaki gari yake eneo la dharura. Baada ya kushuka na kuelekea sokoni huku akiacha usafiri barabarani kumetokea wizi wa simu na speaker ndani yake.

Point yangu ni hii... Naomba mwenye utaalam wa masuala ya mitandao amsaidie kujua sim ilipo bila kutumia IMEI namba maana yeye anajua google account na namba ya siri tu. Ikifanikiwa kwa yeyote atakaejitolea nitamuomba rafiki yangu amfikirie aliempa masaada.

Ikiwa kuna njia zingine tofauti na hiyo niliyoitaja naomba share nasi ili tupate kujua jinsi ya kuipata sim hiyo. Nawatakia kazi njema.
 
Aingie Google dashboard atapata hiyo IMEI number ya simu na mara ya mwisho hiyo simu ilionekana sehemu gani.

Endapo imeibiwa na mjanja au akauziwa mjanja, akibadili IMEI number ndo imetoka hiyo.
Si aghalabu kubadili IMEI namba maana bado sana watu wa huku kufanya michezo hiyo kikubwa anatoa line na kuflash basi.
 
Aingie Google dashboard atapata hiyo IMEI number ya simu na mara ya mwisho hiyo simu ilionekana sehemu gani.

Endapo imeibiwa na mjanja au akauziwa mjanja, akibadili IMEI number ndo imetoka hiyo.
mkuu unafanyaje kujua simu ilikoonekania mara ya mwisho kwa kutumia google
tafadhali nipe ujuzi, nimeishaibiwa sana
 
Mpe pole sana. Siku nyingine tumia njia yangu ili kumjua mwizi wa vifaa vya magari pindi unapopaki sehemu hizo. Ukishashuka kwenye gari yako, jifanye unakwenda moja moja sokoni, halafu piga kona jifiche ukiangalia gari yako, haipiti dk 2 tayari kuna mtu anajishughulisha na gari yako. Njia hii nilimpata mwizi wangu akiwa na kifuniko cha mafuta kaweka mfukoni mwake kwa asilimia 100% nilimpa kibao cha nguvu na akalinda gari mpaka nilipomaliza shopping. Nilipomaliza shopping nikampa buku kwa kulinda gari.
 
Hilo wazo hata mimi nilikua nalo ila nitofauti kidogo na wazo lako. Langu ni hili nimepanga nimchukue mtu kwenye gari yangu halafu nimuache sehemu atangulie eneo la tukio. Mimi nikifika niondoke yeye akiwa anaitazama kwa mbali.

Mimi nitaondoka kwenda mishe zangu za kuzugia huku nikijua nafatiliwa ni mwizi namba 2 ambae anasaidiwa na mwizi namba 1 ambae ndo anaetaka kufanya wizi. Ndo hapo utampata mwizi wa vifaa vya magari.
 
Mpe pole sana. Siku nyingine tumia njia yangu ili kumjua mwizi wa vifaa vya magari pindi unapopaki sehemu hizo. Ukishashuka kwenye gari yako, jifanye unakwenda moja moja sokoni, halafu piga kona jifiche ukiangalia gari yako, haipiti dk 2 tayari kuna mtu anajishughulisha na gari yako. Njia hii nilimpata mwizi wangu akiwa na kifuniko cha mafuta kaweka mfukoni mwake kwa asilimia 100% nilimpa kibao cha nguvu na akalinda gari mpaka nilipomaliza shopping. Nilipomaliza shopping nikampa buku kwa kulinda gari.
Kwa hiyo unajisifia kwa kujichukulia sheria mkononi mwako?why hukumpeleka police or call them?mnatuharibia sana nchi yetu mtu kama wewe hizi kangaroo courts hatuzihitaji.
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom