Msaada: Rafiki yangu anasumbuliwa na fangasi ukeni

desmond3076

JF-Expert Member
Jul 29, 2015
278
182
Wapendwa wana Jamii Forums salaam,

Ninaomba msaada wa matibabu au ushauri nini afanye, ndugu yangu huyu na mtu wa karibu, maana najua humu kuna madaktari bingwa wa magonjwa ya kinamama.

Rafiki yangu anasumbuliwa na fangasi ukeni, yaani ameshatumia kila dawa lakini hapati auheni. Hali inakuwa mbaya anapokuwa kwenye hedhi, anawashwa hadi huruma, na maumivu pia makali.

Jamani anayefahamu solution ya hili kiukweli tunaomba ushauli, anateseka sana. Hedhi ikipita anakuwa shwari.

Jamani yeyote anayesoma ujumbe huu msaada kwenye tuta, tumsaidie please. Wataalam wa Afya Msaada.
 
Hospital aende
Huku akiwa anasaka matibabu
Amenye punje 9za vitunguu swaumu avikatekate avinywe kila siku siku 7 aone
 
Amejaribu grisocam?

Kama bado ajaribu hizo
Kidonge kimoja kila siku kwa siku angalau 30
 
Wapendwa wana Jamii Forums salaam,

Ninaomba msaada wa matibabu au ushauri nini afanye, ndugu yangu huyu na mtu wa karibu, maana najua humu kuna madaktari bingwa wa magonjwa ya kinamama.

Rafiki yangu anasumbuliwa na fangasi ukeni, yaani ameshatumia kila dawa lakini hapati auheni. Hali inakuwa mbaya anapokuwa kwenye hedhi, anawashwa hadi huruma, na maumivu pia makali.

Jamani anayefahamu solution ya hili kiukweli tunaomba ushauli, anateseka sana. Hedhi ikipita anakuwa shwari.

Jamani yeyote anayesoma ujumbe huu msaada kwenye tuta, tumsaidie please. Wataalam wa Afya Msaada.

Ni vyema kutokujikita kwenye jibu la fangasi.

Bali kujikita kwenye kueleza dalili za mgonjwa utakapokutana na daktari.
Ni vizuri kumwona daktari bingwa wa magonjwa ya akinamama.

Mfano:
1: Rangi ya ute ikoje
2: Wingi wa ute
3: Uwepo au kutokuwepo kwa hali ya maziwa ya mgando.
4: Harufu ya ute ikoje
5: Aina ya pedi/zipo zinazoleta shida kwa aleji au dawa iliyowekwa.
6: Uwepo au kutokuwepo kwa maumivu wakati wa kujamiiana.
7: Hali yake ya mzunguko wa hedhi
8: Hali yake na yako mahusiano.
9: Daktari ataweza kumkagua na kuomba vipimo zaidi ili kuthibitisha au kuondoa baadhi ya yale aliyong'amua wakati wa maongezi yenu.
10: Daktari atatoa hitimisho nawe mwaeeza kujafiliana.
 
Inakuwa ngumu kuwashauri watoto wa kike maana miaka hii kuna vitu vingi vya ajabu mnafanya na hata mnapokwenda clinic huwa hamsemi. Nitataja baadhi.

Mnaosha huko chini na sabuni za manukato, mnaweka vitu vya ajabu ukeni kama shabu, ndimu, asali etc kwa kufuata ushauri wa hawa wahuni wa mitandaoni kuwaambia kuwa hizo vitu zitawafanya huko chini kuwa kusafi, tight au kuwa kutamu zaidi kama bikra.

Pia kuna swala la mabinti wa sasa kulala na wanaume tofauti kwa nyakati tofauti. Kwa wastani miaka hii ni ngumu sana kukuta binti anayejihusisha na mwanaume m'moja tu lazima atakuwa na mtu mwingine kando sasa hii ni risk kubwa sana sababu hayo si mapenzi bali ni mahusiano ya kingono.

Mahusiano ya ngono ndipo maradhi ya zinaa husambaa. Leo kuna wanaume wanapendelea kufanya ngono kinyume na maumbile. Wanafanya na wanawake na pia wanaume wenzao. Huko sehemu ya nyuma kuna bakteria na virus wa kila aina ambao ikatokea bahati mbaya wameingia kwenye sehemu za siri za mwanamke basi lazima kupatikane infection ya ajabu.

Sasa unakuta binti anakutana na mwanaume wa sampuli hii ambaye anatoka kula tigo dakika chache anakutana nae yaani hata sehemu za siri hazijaoshwa nini kitatokea. Haya mambo yapo ndugu zanguni.

We umeona wapi magonjwa yasiyosikia dawa ghafla yazuke kizazi hiki na siku zote yalikuwa wapi?
 
Wapendwa wana Jamii Forums salaam,

Ninaomba msaada wa matibabu au ushauri nini afanye, ndugu yangu huyu na mtu wa karibu, maana najua humu kuna madaktari bingwa wa magonjwa ya kinamama.

Rafiki yangu anasumbuliwa na fangasi ukeni, yaani ameshatumia kila dawa lakini hapati auheni. Hali inakuwa mbaya anapokuwa kwenye hedhi, anawashwa hadi huruma, na maumivu pia makali.

Jamani anayefahamu solution ya hili kiukweli tunaomba ushauli, anateseka sana. Hedhi ikipita anakuwa shwari.

Jamani yeyote anayesoma ujumbe huu msaada kwenye tuta, tumsaidie please. Wataalam wa Afya Msaada.
Pole sana ila acha kumsingizia rafikiyo! Mficha maradhi......
 
Back
Top Bottom