Msaada pozi gani ni sahihi kwa bwana harusi

Msaada pozi gani ni sahihi kwa bwana harusi

appoh

JF-Expert Member
Joined
Mar 14, 2013
Posts
5,941
Reaction score
3,262
Natarajia kuoa jumapili hii sasa sijajua pozi gani ni sahihi kwa bwana harusi akiwa ukumbini maana nimejaribu ku google nimekosa nimeshuudia mapozi mbalimbali ya mabwana harusi ukumbini kama.

Kuna harusi moja jamaa alikua kanuna mda wote hacheki isitoshe mke wake alikua mwanajeshi yeye ni raia lakini unaweza sema yeye ndio mwana jeshi kiukweli jamaa aliaribu mkanda mzima wa harusi yake tulipokua tunaangalia.

Pozi lingine lilikua ni la jamaa mwenyewe mawazo sana ukumbini na alikua hana furaha sijui alolzimishwa sijui,

Latatu ni jamaa alichangamka muda wote anaruka ruka na kucheka mpaka watu wakawa wanajiuliza katoroka milembe harusi nyingine ni jamaa aliekua analia sijui tatizo nini ,

Nipo katika wakati mgumu sana wa maamuzi ebu wakubwa zangu wazoefu nipeni kidogo pozi lipi litakua linakubalika na wote
 
Hongera kwa kufanya harusi na kwenda ukumbini.
 
pozi la huyo jamaa aliyelia ukumbini ni nzuri sana...
 
Hebu fikiria kuwa ni siku yako special ambayo haiwezi jirudia kila kitu kitajipa chenyewe otherwise umelazimishwa kuoa.
 
Kuwa na pozi la sintofahamu..

2649473-serious-african-business-man-in-suit-and-tie-with-finger-against-face.jpg

cc: appoh
 
hyo haina kujiandaa mkuu, pozi huwa linakuja automatic tu hutegemeana sana na hali ya hewa humo ukimbin.
 
kuwa na pozi ukikumbuka madeni uliyokopa ili kufanikisha harusi yako
 
natarajia kuoa jumapili hii sasa sijajua pozi gani ni sahihi kwa bwana harusi akiwa ukumbini maana nimejaribu ku google nimekosa
nimeshuudia mapozi mbalimbali ya mabwana harusi ukumbini kama
kuna harusi moja jamaa alikua kanuna mda wote hacheki isitoshe mke wake alikua mwanajeshi yeye ni raia lakini unaweza sema yeye ndio mwana jeshi kiukweli jamaa aliaribu mkanda mzima wa harusi yake tulipokua tunaangalia
pozi lingine lilikua ni la jamaa mwenyewe mawazo sana ukumbini na alikua hana furaha sijui alolzimishwa sijui
latati ni jamaa alichangamka mda wote anaruka ruka na kucheka mpaka watu wakawa wanajiuliza katoroka milembe harusi nyingine ni jamaa aliekua analia sijui tatizo nini
nipo katika wakati mgumu sana wa maamuzi ebu wakubwa zangu wazoefu nipeni kidogo pozi lipi litakua linakubalika na wote

Mkuu hongera sana kwa kuamua 'kuasi ukapera'
...
Kuwa ukumbini pale usichukuli poa poa, unahitajika umakini mkubwa sana, otherwise unaweza kujikuta kama unaelea angani! Nilishawahi kuwa bordguard wa bw. Arusi!
...
So, ningekushauri utafute mvinyo (pombe ya zabibu) i hope zinatengenezwa South Afrika but hata supermaket na baadhi ya baa zinapatikana! Ni mzuri, hazina uchungu wa kukera, ukinywa hauwi na maharufu! Aisee unajiskia poa ile mbaya, fulu tabasamu, macho hayalegei, joint za miguu hazipanguki, stimu zake ni tofauti kabisa na konyagi na mawiski mengine!
...
Embu kaitafute uitest kwanza!
 
Dah umenikumbusha nilihudhuria harusi moja sa wakati wakuingia huyo bwana harusi looh! Kunyata si kunyata,tembea si tembea,kuruka siko kakomaza shingo anajitahid kwenda na step waaaaapi!! Dah kanunaaaaaa! Alikuwa kituko + kichekesho!! Harusi zina mambo?haha loh!
 
hilo pozi la jamaa wa tatu aliekuwa anarukaruka ukumbini zuri sana linakufaaa sana
 
Pozi zuri ni la kutembea kijoti wewe na mkeo itabamba sana!
 
navojua mimi unaweza kunogesha sherehe kwa kufanya a right thing at a right time,yan mc akichekesha sio mbaya ukatabasam, na mkeo akikukonyeza respond ucje kumuignore, toa mawazo na weka imani kuwa hilo event halina part two ila usiache kumwomba Mungu awe kiongozi wako
 
Back
Top Bottom